Ufafanuzi Kuhusu Awamu za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MpendaNchi1

Member
Joined
Sep 25, 2021
Posts
7
Reaction score
4
Kuna jambo ambalo watu wengi hawaelewi vizuri — kwamba dhana ya Awamu katika tafsiri ya kisiasa inahusiana moja kwa moja na mtu binafsi, yaani Rais aliyepo madarakani katika kipindi husika. Kwa bahati nzuri, wakati Mheshimiwa Rais alipokuwa akizindua DIRA 2050, alieleza kwa ufasaha mchango wa kila awamu ya uongozi hadi sasa, akitaja mafanikio ya kila moja kati ya awamu hizo sita.

Mimi, kama mwanachama wa kawaida wa kundi hili, naweza kueleza kwa maneno rahisi kuwa:

Awamu ya Urais huanza pale Rais anapoapishwa na hudumu kwa muda wake wa kikatiba. Awamu hiyo hukoma pindi Rais huyo anapomaliza muda wake au kuondoka madarakani. Hivyo basi, mpaka sasa, Tanzania imepita kwenye awamu sita kama ifuatavyo:

Awamu ya Kwanza (1964 - 1985) — Mwalimu Julius K. Nyerere (Miaka 21) — Bara

Awamu ya Pili (1985 - 1995) — Ali Hassan Mwinyi (Miaka 10) — Zanzibar

Awamu ya Tatu (1995 - 2005) — Benjamin W. Mkapa (Miaka 10) — Bara

Awamu ya Nne (2005 - 2015) — Jakaya M. Kikwete (Miaka 10) — Bara

Awamu ya Tano (2015 - 2021) — John P. Magufuli (Miaka 5 na miezi 4) — Bara

Awamu ya Sita (2021 - sasa) — Samia Suluhu Hassan (Miaka 4 na miezi 4 hadi sasa) — Zanzibar

Kwa muktadha wa utamaduni wa CCM wa kupokezana uongozi kati ya Bara na Zanzibar, hata kama nafasi ya urais ingekuwa wazi, kwa desturi, ingepaswa kuchukuliwa na mgombea kutoka Zanzibar.

Mpaka sasa, viongozi kutoka Bara wameiongoza Jamhuri ya Muungano kwa jumla ya miaka 46, huku viongozi kutoka Zanzibar wakiwa wameongoza kwa miaka 14 pekee. Hili, bila shaka, ni miongoni mwa mambo tunayoweza kuyaangalia kama kero za Muungano.

Awamu ya Rais Samia inaendelea rasmi, na itaendelea kuitwa hivyo hadi atakapostaafu mwaka 2030 — Panapo majaaliwa.Muhimu kukumbukwa pia kuwa awamu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya Tanganyika huru (1962) na hadi ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoanza mwaka 1964 fomu ya Urais ilikuwa moja tu ndio ya misingi tuliyokuwa tumejengewa hiyo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ubariki Umoja na Muungano wa Tanzania dhidi ya wote wenye uchu wa madaraka!

Mtambalike

Morogoro
 
kwa nilivyomuelewa humphrey polepole kwa namna ambavyo alijaribu kuelezea, alieleza walau kwa namna ya kutosisitiza sana ya kwamba kuna baadhi ya watu ambao kimsingi kwa desturi za chama cha mapinduzi hawapaswi kuwa marais tena akiwemo waziri mkuu makamu wa rais kwa sababu wao wamekwisha fanya wajibu huo kumsaidia rais kumbe hakuna kitu kipya ambacho wanaweza kukifanya au wakashauri kuleta mabadiliko na mvuto mpya. kwa jinsi hiyo kutokana na utaratibu huo makamu wa rais hapaswi kugombea kuwa rais na ndio maana kama ulimwelewa vizuri, alisema kwamba yeye kuwa madarakani kwa mujibu wa desturi yao na kwa jumla na katiba alipaswa kuingia madarakani baada ya kifo cha rais lakini pili alipaswa kuitisha uchaguzi mara moja ili tupate kiongozi mwingine mpya ambaye angeweza kuendeleza gurudumu hilo lakini na kuiongoza nchi wakati huo kitu ambacho yumkini hakikufanyika kama sikuelewa vibaya. kwa hiyo sasa nadhani waandishi wa habari walishindwa kumuuliza vizuri ni kwa namna gani makamu wa rais waziri mkuu hawawezi wakagombea nafasi ya rais badala yake wakawa wanamuuliza vitu vingine kama vile habari za kutekwa kwa watu kupotea kwa watu na namna gani ambavyo amekidhalisha chama cha mapinduzi. hivyo kusema kweli kuna namna ambavyo alijaribu kulizungumzia hilo kwa ufupi sana akionyesha ni kwa namna gani makamu wa rais alipaswa kuitisha uchaguzi mapema lakini kama makamu wa rais pia kwa mujibu wa desturi zao hakupaswa kuwania uraisi kwa sababu alikwisha huduma pia kama msaidizi mkubwa wa raisi na msaidizi wa karibu wa raisi katika kutekeleza majukumu yake kadha wa kadha.
 
Back
Top Bottom