mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
Non-performing loans (NPL) ni ile mikopo ambayo benki au taasisi ya kifedha imeitoa kwa wateja na wadaiwa wakashindwa kuirudisha kwa wakati uliainishwa kwenye mkataba au makubaliano. Hizo benki ambazo zimewekewa rangi nyekundu ina maana kwamba NPL yao imezid wastani uliowekwa na BoT ambayo 12.52% (standard NPL).
Nini Sababu na Athari za kuwa na NPL iliyozidi wastani uliowekwa?
(A). Sababu zinazoweza kufanya benki ikawa na NPL kubwa kuliko standard?
1. Poor loans screening- ni benki inapotoa mkopo kwa bila kujua huyu mteja amekithi vigezo vya kupata mkopo. Hivyo husababisha mtejea huyo kushindwa kurudisha mkopo kwa wakati uliowekwa au kushindwa kabisa kulipa.
2. Poor follow up of the loans delinquency- hii ni kutokuwa na usimamiz mzuri wa mikopo iliyocheleweshwa kulipwa. Ambayo husababisha mteja kukulipa mkopo aliochukua.
(B) Athari ya kuwa na NPL kubwa zaidi ya kiwango kilichowekwa.
1. Shrink in profitability of the banks- kuwa na NPL hupelekea benki kupata hasara kwa sababu moja ya chanzo kikuu cha pesa za benki ni mikopo hivyo kuwa na NPL kubwa ina maana ina fanya faida kupungua au hasara kabisa kwa mwaka husika wa fedha.
2. Liquidity crunch- hii ni ile hali ya benki kushindwa kufikia mahitaji yake ya kila siku. Kwa sababu matapo yameshuka basi inapelekea kusindwa kufikia mahitaji ya kila siku kama upungufu wa pesa kwenye ATM, mikopo kutotoka kwa wakati n.k. Hii NPL iliathiri benki nyingi mwaka wa fedha 2015/2016 kupelekea faida kushuka kwa benki.
Finally to sum on this...high NPL doesn't mean the revocation of the banks as we know one of the core function of banks is receive deposit and disbursements of loans; therefore the higher NPL will affect banks profitability hence a lead to liquidity crunch. Now those banks are in the warning signs on how they deal with their customes to rescue reputation and income as well. Thank You
Kama kuna sehemu imepungua karibuni wana jamvi muongezeee