UFAFANUZI: Mtume Mohamad amewahi kutenda muujiza gani?

Yani leo ndio nimegundua watu wanajua tu kufika misikitini na makanisani ila kuhusu dini bado safari ni ndefu.Hivi nani aliwambia kuna mtume alitenda muujiza au ni mtume yupi alisema nimekutendea muujiza?

Miujiza yote anayeweza kufanya ni mwenyezi Mungu tu hao wajumbe wake hutumiwa kuonyesha mamlaka ya Mungu au kufikisha ujumbe katika namna rafiki kwa wenye mioyo migumu.Acheni utoto sijui huyu alishusha kitabu mara huyu katenganisha bahari hizo nguvu walizitoa wapi? kwamba walisema ni kazi zao? au nyie kwenye dini mpo daraja lipi?
 
Yani leo ndio nimegundua watu wanajua tu kufika misikitini na makanisani ila kuhusu dini bado safari ni ndefu.Hivi nani aliwambia kuna mtume alitenda muujiza au ni mtume yupi alisema nimekutendea muujiza?
N.B mitume walifanya hayo Bismillah (Kwa kina la Mwenyezi Mungu) Biidhinillah (Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu)
 
Sasa kama Quran ililetwa toka juu, mbona maandiko yake mengi kama Injili, Zaburi,
Ni tofauti kabisa na hivyo vitabu ulivyovitaja:

Lakini Qur'an si kitabu cha sayansi, bali ni kitabu cha ishara. Ukweli mwingi wa kisayansi ambao unaonyeshwa kwa njia fupi sana na ya kina katika mistari yake umegunduliwa tu na teknolojia ya karne ya 20. Ukweli huu haungeweza kujulikana wakati wa ufunuo wa Qur'an, na hii bado ni uthibitisho zaidi kwamba Qur'an ni neno la Mungu.

Ili kuelewa muujiza wa kisayansi wa Qur'an, ni lazima kwanza tuangalie kiwango cha sayansi wakati ambapo kitabu hiki kitakatifu kilifunuliwa.

Katika karne ya 7, wakati Qur'an ilipofunuliwa, jamii ya Waarabu ilikuwa na imani nyingi za kishirikina na zisizo na msingi ambapo masuala ya kisayansi yalikuwa yanahusika. Kukosa teknolojia ya kuchunguza ulimwengu na asili, Waarabu hawa wa mapema waliamini katika hadithi zilizorithiwa kutoka vizazi vilivyopita. Walidhani, kwa mfano, kwamba milima iliunga mkono anga hapo juu. Waliamini kwamba dunia ilikuwa tambarare na kwamba kulikuwa na milima mirefu katika ncha zake zote mbili. Ilifikiriwa kwamba milima hii ilikuwa nguzo ambazo ziliweka kuba ya mbinguni juu.

Hata hivyo, imani hizi zote za kishirikina za jamii ya Kiarabu ziliondolewa na Qur'an. Katika Sura ya 2, aya ya 38, ilisemwa: "Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila msaada wowote..." (Quran, 2:<>). Aya hii ilibatilisha imani kwamba mbingu inabaki juu kwa sababu ya milima. Katika masomo mengine mengi, ukweli muhimu ulifunuliwa wakati ambapo hakuna mtu angeweza kuzijua. Qur'an ambayo iliteremshwa katika wakati ambapo watu walijua kidogo sana kuhusu unajimu, fizikia, au biolojia, ina ukweli muhimu juu ya mambo mbalimbali kama vile uumbaji wa ulimwengu, uumbaji wa mwanadamu, muundo wa anga, na mizani maridadi ambayo hufanya maisha duniani yawezekane.

Sasa, hebu tuangalie baadhi ya miujiza hii ya kisayansi iliyofunuliwa katika Qur'an pamoja.​

  • Hali ya hewa ya dunia
  • Quran juu ya Maendeleo ya Embryonic ya Binadamu
  • Quran juu ya milima
  • Quran juu ya Asili ya Ulimwengu
  • Quran juu ya Cerebrum
  • Qur'an juu ya bahari na mito
  • Quran juu ya bahari ya kina na mawimbi ya ndani
  • Qur'an juu ya mawingu
  • Maoni ya wanasayansi juu ya miujiza ya kisayansi katika Quran Tukufu
  • Muujiza wa Iron
  • Quran juu ya Ulimwengu wa Kupanua na Nadharia ya Big Bang
  • Ushindi wa Warumi na hatua ya chini kabisa duniani
  • Saba ya Dunia
 
Mbona naona wengi hawa masheikh ni waganga.... Na wanakuwa na majini.... Je huu hivi visomo ni vya Mungu kweli

Nachoelewa, kuna watu wanatibu kupitia Quran na kuna masheikh baadhi wanapiga ramli au wanaponya kupitia majini.

Sasa hapa ndipo huwa najitahidi kutofautisha kati ya uislamu na matendo ya muislamu, japo nilisikia msimamo wa waislamu dhidi ya majini ni tofauti na sisi tunaoamini kuwa yote ni mabaya
 
Mbona naona wengi hawa masheikh ni waganga.... Na wanakuwa na majini.... Je huu hivi visomo ni vya Mungu kweli
Watu wanaforce rizki
hao na wauza snake oil makanisani ni fungu Moja.
Usihukumu dini Kwa matendo ya waumini
 
Kuna wengi ni wapigaji.

Wajinga ndiyo waliwao.
 
N.B mitume walifanya hayo Bismillah (Kwa kina la Mwenyezi Mungu) Biidhinillah (Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu)
ndio ila wengi wanadhani kuna mtume kwa nguvu zake mwenyewe au mamlaka yake alitenda muujiza.Miujiza yote ya mitume inabaki kuwa kazi ya mwenyezi Mungu.Na sio kwamba kuwa mtume lazima uje na miujiza sio kweli? miujiza mingi imetendeka tu kuwafanya wenye mioyo migumu kuamini au kurejea katika njia sahihi ambazo mwenyezi Mungu kaziweka
 
Hivi wewe huwa huna bwana? Kutwa nzima uko humu kuandika upuuzi tu na kubishana na wanaume
 
And We have certainly made the Qur'an easy for remembrance, so is there any who will remember?
(Qur'an 54:17).

Achana na hiyo miujiza mingine ya kuhadithiwa ambayo hata babu yako hajayashuhudia. Hii Qur'an ni muujiza tosha ambao hata mtoto mdogo ambaye kiarabu sio lugha yake hadi chini ya miaka 7 anahifadhi.
Ukisikia ile balagha yake ilivyopangiliwa tena imeshushwa kwa maneno bila kuandikwa ndani ya miaka 23 sio mchezo.
Qur'an ambayo tunaona hadi vipofu wanahifadhi kichwani. Hiyo miujiza mingine ulishuhudia wapi zaidi ya kuambiwa kwenye biblia zilizochakachuliwa.


View: https://youtu.be/T9B38w0zrSg?si=0iz5TTcGDDZ4qdOS
 
Hiyo sio miujiza ni namna tunavyoishi tu wajanja wamewaingizia taratibu za namna wao wanavyoishi ebu badirika acha ubishi wa kijinga
 
Barikiwa mno, nimeipenda hii.[emoji120]
 
Mtume huyu alioa katoto. Ukiukaji wa haki za watoto, ndio miujiza yake ni ya dizaini hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…