Ufafanuzi tukio lilotokea kwenye Anga la Tanzania, Teknolojia inazidi kukuwa, Watanzania tunaachwa nyuma tunabaki kushangaa

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Siku ya leo jioni kumekuwa na taharuki baada ya watu kuona vitu vilivyopita angani mithiri ya nyota zinazoongozana katika mstari mmoja, wapo waliodhani ni nyota, wapo waliodhani ni vimondo, mpaka waliodhani ni miujiza.

Pia soma > Mliopo Dar es Salaam kuna kitu kinapita maeneo yenu angani


Ukweli ni kwamba hizi zilikuwa ni satelaiti za kampuni ya internet ya starkink inayomilikiwa na Elon Musk.


Internet hii inapatikana hata uwe bondeni, milimani, porini, kijijini, n.k. Internet haina kikomo utatumia unavyotaka (Unlimited), Kuna takribani satelaiti elf 5 za starlink zinazunguka juu ya anga la dunia kuhakikisha internet inapatikana sehemu zote duniani,


Tanzania tulikua moja ya nchi za mwanzo kabisa kuhusishwa na hii internet lakini mpaka leo vibali vinashughulikiwa, Tangu mwaka jana mwezi wa pili Waziri wa Teknolojia, Nnape Nauye amekuwa akisema starlink hawajakamilisha vibali,. >> source <<


Internet hii imepewa vibali nchi nyingi, Nchi jirani zinazofaidi huduma hii ni Kenya, Rwanda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Kwa sasa sisi tutabaki kushangaa hizo satelaiti angani lakini wanaozitumia ni majirani,

 
Zilikuwa kwenye maandamano?
 
hakukuwa na haja ya hii taharuki ya kuonesha ushamba wa wazi wazi kama Nnnape Nnauye anagemruhusu Elon Musk
You mean Nape angeruhusu Starlink hii inamaanisha watu wangeona hizo satellite juu wangejua ni satellite za starlink....HOW??

Unadhani watu ambao hawakujua kinachopira juu ni nini hawajui kuhusu Starlink, Elon, Space X and such stuffs ??

Hakun asiyeju satellite humu wewe umeju hizo satellite za starlink baada ya kusachi tu kama sisi instant ulivyoziona hukujua ni nini
 
Tanzania ukiwa na akili kama za Lucas mwashambwa unakuwa mteule in waiting.

Watu kama kina Mwijaku, Kitenge, Masanja, Dotto Magari, Mpoto, Aristote, Juma Lokole na fananizi nao ndo unaonekana thinktank wa nchi.

Tuendelee kupambania watawala ili watawale vizuri hata kama hawana nia njema na nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…