Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Nimeona ujumbe wa upotoshaji unaozungushwa kwenye mitandao ya kijamii ulioandikwa na Godsen Malisa kuhusu suala la ndege ya ATCL kuja China kuwachukua wanafunzi. Nimeona nitoe ufafanuzi ili umma uwezi kufahamu ukweli na kuachana na upotoshwaji unaofanywa kwa agenda anazozijua mwandishi mwenyewe.
Kweli ule msemo wa waswahili usemao "Tenda Wema, Uende Zako" ni sahihi kabisa. Air Tanzania imefanya kazi nzuri ya kuwarejesha salama watanzania wenzetu waliokuwa wamekwama hapa China. Hakika wanastahili kupongezwa na sio kubezwa.
Yapo mambo ya msingi ambayo ni vizuri yakafahamika ili kuupata muktadha mzima wa safari hiyo ya kuwarejesha watanzania kutoka China.
Tangu kuzuka kwa ugonjwa wa COVID19 mwezi Desemba 2019 usafiri wa kutoka China kwenda sehemu nyingine duniani ulisitishwa kwa asilimia 80. Hadi sasa, ni mashirika ya ndege machache yanayoruhusiwa kufanya safari ya kwenda China. Na hayo mashirika ya ndege machache yaliyoruhusiwa kufanya safari za kuingia China yamepewa masharti mawili makuu:
1) Ruhusa yao ni kufanya safari moja TU kwa wiki;
2) Abiria wa kwenye ndege wanatakiwa wasizidi asilimia 60 ya uwezo wa ndege wa kubeba abiria. Sharti hili linalenga kuzingatia hitaji la "social distance" ndani ya ndege;
Hadi leo huduma ya kutoka China kwenda Afrika (Tanzania) inatolewa na shirika MOJA tu (Ethiopian airlines).
Kutokana na masharti mawili yaliyotajwa hapo juu, ni vigumu sana kupata nafasi katika Ndege ya Ethiopian na pia kumepelekea gharama ya tiketi kupanda juu sana. Tiketi ya daraja ya Economy One way kutoka China kwenda Tanzania ilifikia YUAN 30,000 ambayo ni sawa na USD 4,280. Kiasi hicho kipo juu sana na watanzania wengi waliokuwa wanahitaji usafiri wa kurudi nyumbani walikuwa hawawezi kukimudu. Kwenye hili ni rahisi kupata uthibitisho kama hauamini nilichosema (piga simu ofisi za Ethiopian airlines popote duniani waombe wakupe quotation ya one-way ticket kutoka China kwenda Tanzania).
Ili kukabiliana na changamoto hii- mashirika mawili ya ndege yameanzisha utaratibu wa "Special Flight" ambao unahitaji vibali maalum kutoka kwa Mamlaka za China. Mashirika hayo ni pamoja na QATAR airways na EGYPT AIR. Gharama za tiketi katika ndege hizo (one way economy) ni kati USD 1600 hadi usd 2500 kutegemeana na nchi unayokwenda barani Afrika na uwepo wa Connection kutoka katika HUBS zao ( Cairo kwa Egypt air) na (Doha kwa Qatar) kwenda katika nchi unayokwenda. Baadhi ya wanafunzi ambao Scholarship zao zinajumuisha usafiri wa kurudi nyumbani- wamerejea Tanzania na usafiri huo.
Hivyo- dhana iliyoelezwa na Malisa kwamba watanzania walilazimishwa kupanda Air Tanzania sio kweli. Zilikuwepo options nyingine za usafiri na baadhi ya watanzania waliozimudu walizitumua.
Aidha, madai kwamba Air Tanzania ilitoza fedha nyingi kuliko mashirika mengine ni UWONGO. Katika options zote nilizotaja hapo juu- hakuna iliyokuwa chini ya Bei waliyolipa watanzania waliosafiri na Air Tanzania.
Wakati Ethiopian wanatoza usd 4,280; Egypt Air- USD 1600; Qatar usd 2500- wanafunzi watanzania waliosafiri na Air Tanzania walipewa bei maalum ya usd 1219.
Ndio maana hata jana kwenye taarifa yetu ya tukio hili- tumeishukuru sana Serikali kwa kuwajali wananchi wake kwa kuwapa bei ya chini.... ambayo ni kama kusema bei ya kuchangia mafuta na gharama nyinginezo za uendeshaji.
Kuhusu madai ya kwamba kulikuwa na makosa mengi - na hivyo kutengeneza taswira ya kwamba Air Tanzania ilishindwa kazi - nalo linapotoshwa kwasababu muktadha wake haujaelezwa vizuri.
Ili kupata muktadha Ni vizuri ikaeleweka mambo matatu:
1) Safari hii imefanyika nje ya mfumo wa kawaida wa shirika la ndege kuingia china kama ndege ya biashara. Hii ilikuwa ni SPECIAL FLIGHT ambayo mfumo wake ulikuwa ni wa kiserikali- kwa maana ya kwamba Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wake China imeiomba Serikali ya China kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya China kuruhusu Air Tanzania ilete ndege ya kuwachukua watanzania waliokwama. Na kibali kilitolewa mahususi kwa ajili hiyo. Ndio maana wakati ndege hiyo inakuja China haikuruhusiwa kubeba abiria yoyote- zaidi ya Wanadiplomasia wa Tanzania (wawili na familia zao- jumla (4) waliokuwa wanarejea katika kituo chao cha kazi. Walikuwepo raia wa China waliopenda kupanda ndege hiyo kurejea kwao China- lakini SERIKALI ya CHINA haikuruhusu.
2) Jukumu la kuratibu upatikanaji wa abiria, kusajili abiria; kuhakikisha malipo ya abiria lilikuwa ni la UBALOZI.
Kwa upande wa kutafuta abiria- ubalozi ulifanya kazi hiyo kupitia taarifa kwa umma zilizotolewa kwa watanzania wanaoishi China.
Na kwa upande wa ukusanyaji wa malipo- kwakuwa ubalozi hauna akaunti kwa madhumuni ya kupokelea malipo yasiyohusiana na shughuli za kibalozi- Ubalozi uliiomba Air Tanzania iratibu shughuli hiyo ya kupokea malipo. Hivyo kila malipo yalivyokuwa yanafanywa katika akaunti ya ATCL- ubalozi ulikuwa unapokea uthibitisho kutoka kwa abiria wenyewe na baadaye ulikuwa una cross-check na Air Tanzania kuthibitisha malipo yamepokelewa na hatimaye Ubalozi ulikuwa unatuma majina Air Tanzania kwa ajili ya kutoa tiketi.
Changamoto ya majina kukosewa -ilitokana na teknolojia. Afisa ubalozi wa Tanzani ambaye ni raia wa China (local staff) aliyekuwa anatuma taarifa za waliofanya malipo kwa kutumia mtandao wq mawasiliano wa Kichina WECHAT na kwenye computer yake software zote zipo kwa lugha ya Kichina- lakini alipokuwa anatuma taarifa kwa mpokeaji aliyekuwa Air Tanzania -alikuwa anafanya "Auto-translation" ili mpokeaji apokee kwa lugha ya kiingereza- zoezi hilo ndio lilipelekea baadhi ya makosa yaliyojitokeza. Kwa kuzingatia kwamba orodha ilikuwa kubwa ya majina 252- haikuwa rahisi kwa mtu wa Air Tanzania kubaini kama taarifa alizopokea zilizotafsiriwa kutoka Kichina zilikuwa na makosa.
Makosa yalikuja kugunduliwa na abiria wenyewe walivyopewa tiketi zao. Na wakati huo; muda ulikuwa umekwenda sana- haikuwa rahisi kuyapitia majina yote ili kubaini makosa- ndio maana Ubalozi ukaamua kutengeneza orodha mpya kwa ajili ya kutumiwa kufanya verification wakati wa ku check-in. Nilikuwepo mwenyewe Guangzhou Baiyun Airport wakati wa zoezi la kucheck in. Lilikwenda vizuri saaana. Hapakuwa na tatizo lolote. Kwetu sisi agenda kuu ilikuwa ni kuwawezesha watanzania wenzetu wapate usafiri wa uhakika na nafuu na wafike nyumbani salama. Yote mawili yamefanikiwa.
Nimalizie kwa kuwapongeza sana Air Tanzania kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia na kwa kazi kubwa na nzuri ya kizalendo waliyoifanya ya kuwarejesha watanzania wenzetu.
Mimi sina shaka kabisa na uwezo wao na weledi wao. Wasikatishwe tamaa. Hivi kama ATCL ingekuwa incompetent kiasi hicho- mbona chini ya utaratibu huu wa special flight wamesafirisha abiria kutoka India - zaidi ya mara 3- na hapakuwa na tatizo lolote. Mbali na SPECIAL FLIGHTS walizofanya India kuwarejesha watanzania wenzetu- kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa COVID19- ATCL imekuwa ikifanya safari za kibiashara kwenda India - hatujawahi kusikia majina ya abiria yamekosewa- ndio sasa wakosee leo? Kweli? Mnyonge Mnyongeni- HAKI YAKE MPENI.
Mbelwa Kairuki
Balozi wa Tanzania- China