Kumbe unajua, kwa nini uanze kutukana profession za watu.
Dharau yangu ipo kwa wale wanaopenda kujiita wao wasomi. Wasomi wamesoma nini? Waende zao huko.
Ni ngumu kupata maana halisi ya neno kutoka lugha moja kwenda nyingine.
Si vigumu kama unavyodhani na mnaodhani hivyo mko wengi kweli. Hiyo attitude yenu mimi naiita 'defeatist' attitude.
Anyway, kama wewe unajua lugha ya kiingereza, fahamu ina utajiri wa maneno, tatizo litakuja kutafsiri hiyo rheria kuja kwenye kiswahili ambacho bado hakina maneno mengi.
Kiingereza kimekopa maneno mengi sana toka kwenye lugha zingine. Sasa hivi hata neno "safari" limo kwenye kamusi za Kiingereza.
Hata legalese imejaa maneno kibao ya Kilatini. Kwa hiyo huo utajiri wa maneno wa lugha ya Kiingereza unatokana na watumiaji asili wa lugha hiyo kupenda kuikuza na kuipanua kwa njia na namna yoyote ile.
Kama Kiingereza kimekopa maneno lukuki toka kwenye Kifaransa, Kilatini, Kireno, na hata Kiswahili, kwa nini Kiswahili kishindwe kukopa maneno mengi kutoka kwenye lugha ingine? Inawezekana kabisa sema sisi wenye lugha hatuna 'a can do spirit' na tumetawaliwa na defeatist attitudes.
Sheria zenyewe kumbuka zipo nyingi na nyingine nyingi zinatungwa, ndio maana hata uende India, mahakama zao wanaongea kiingereza unless mahakama za chini.
Mimi sijali kinachoendelea huko India. Najali zaidi kinachoendelea Tanzania. Sheria ni zetu wenyewe Watanzania. Tukiamua tunaweza kabisa kuzitunga kwa kutumia lugha yetu wenyewe. Tatizo ni kwamba wengi mmeshakubali kuwa eti haiwezekani.
Mimi nakataa. Nasema inawezekana kabisa. Kama Wamarekani waliweka dhamira ya kwenda mwezini na kweli wakaenda, sidhani na sisi tukiweka dhamira ya kutunga sheria zetu kwa lugha yetu wenyewe tutashindwa.
Hebu jiulize tu hata wewe. Kipi kigumu - kuunda lidege la kwenda mwezini au sayari zingine au kuandika sheria zetu kwa lugha yetu wenyewe? Kwangu hapo jibu ni dhahiri kabisa kuwa kuunda lidege la kwenda huko outer space ni shughuli pevu haswa!
Nadhani unapata picha halisi, pia we angalia ugumu unaokuja katika elimu kufundisha kiswahili, jiulize Doctors wataweza kubadili maneno ya kiingereza na kilatini yaliyomo kwenye vitabu tunavyovitumia kama mwongozo? Engineers je?
Nadhani jibu ni rahisi sana.
Inawezekana kabisa. Lugha hukuzwa na watumiaji wake. Kama msamiati haupo kwenye lugha basi mnatafsiri hivyo hivyo toka kwenye lugha ingine.
Mbona neno "shule" tumelitoa kwenye Kijerumani ambapo kwao ni "schule"? Au wewe unadhani "shule" ni neno la Kiswahili?
Hakuna ugumu wowote katika kuandika sheria zetu kwa kutumia Kiswahili. Sheria ni zetu wenyewe. Zinatuongoza sisi wenyewe. Sasa kwa nini tuziandike kwa kutumia lugha ya kigeni? Haiingii akilini kabisa. Kama na hili hatuliwezi basi hakuna tutakaloliweza.