Ufafanuzi wa kisheria unahitajika hapa. Wanasheria Njooni

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,891
Ibara number 41 ya katiba ya JMT inazungumzia uchaguzi wa raisi. Ninaomba wanasheria mtusaidie kupata ufafanuzi kifungu cha saba.

(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwaamechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote.

(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.

Ufafanuzi ninaoumba ni kama tangazo la tume juu ya raisi litakuwa na kinga ya kutokuchunguzwa na mahakama yoyote hata pale ambapo maamuzi ya tangazo hilo hayajazingatia matakwa ya Ibara hii ya 41 mfano kama kifungu cha 6 ama chochote kikiwa kimekiukwa.

Kifungu cha saba kinasema wazi "Iwapo mgombea ametangazwa na tume ya uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa raisi kwa mujibu wa ibara hii (ya 41)". Vipi kama kilichotangazwa hakiko kwa mujibu wa ibara hii? Bado tangazo hilo ni legal binding?

Swali lingine, ni chombo gani kinatakiwa kuhakiki compliace ya tume ( iliyopewa nguvu hiyo kwenye) ili kujiridhisha kwamba inachokitangaza kimefanyika inline with stipulations za ibara hii ya 41?

Vipi ikitokea msemaji wa tume, on insanity, corruption, Rebellion, conspiracy, au threat grounds akamtangaza mtu kuwa raisi bila taratibu na mahitaji ya ibara hii ya 41 kufuatwa, bado itakuwa ni lawful, binding and enforceable announcement?

NAOMBA TUJADILIANE NA KUELEIMISHANA KWA HOJA. Na ni vizuri tukiwa tunarejea mfano wa kifungu cha sita hapo juu.
 
Ni swali la kinadharia sana kwani tume inalijua hilo na Tume ikitangaza mgombea ambae atakuwa hajapata kura nyingi zaidi ya wengine kuwa ni mshindi itakuwa imevunja katiba na huo sasa ndio unaitwa mgogoro wa kikatiba....kesi hiyo inaweza kufunguliwa mahakama kuu....ndio maana tume haiwezi kufanya kosa la kutangaza mtu aliyepata kura kidogo ndio mshindi......itakuwa imevunja katiba ya nchi......
"(7) When a candidate is declared by the Electoral Commission to have
been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have
any jurisdiction to inquire into the election of that candidate"
 
Naona tayari umeondoka kwnye mjadala unaleta ulalo. Kujua sheria kwa tume ndiyo defense kwamba hawawezi ku breach?

Unataka kusema wote wanaovunja sheria ni kwa sababu hawajui?

Ulitakiwa pengine kusoma na kuelewa pale niliipoorodhesha mazingira yanayoweza kufanya watu wakaamua kinyume na kweli.

Nani anathibitisha kwamba tume inafanya maamuzi kulingana na ibarah hiyo?

Tafadhali jibu scientifically, kama huna jjibu, usitupoteze, subiri wataalamu waje wenye uwezo wa kuelewa.
 
1.Hakuna cha scince wala nini, ni sheria tu, Mkuu nakuelezea kwa kuzingatia sheria zilizopo na kwa mujibu wa Katiba iliyopo, kama Tume imefuata utaratibu wa kumtangaza mshindi kama ulivyo kwenye Katiba na sheria ya Uchaguzi...na ikamtangaza, akishatangazwa huna jinsi...huyo ndio Rais mteule....
2. Kwa sheria zilizopo na kwa mujibu wa Katiba iliyopo, kama una malalamiko unaweza kuyawasilisha malalamiko yako kabla matokeo hayajatangazwa kwemye tume, na sio pengine, na tume itayatolea uamuzi KABLA hajaitangaza matokeo ya Urais. Hakuna chombo kingine chochote kinachoweza kuhakiki Tume ....ikishatangaza na kama imefuata ule mtitiririko wa ibara ya 41 ndio imetoka hiyo....hakuna wa kuhakiki wala kushtaki......
#. Soma Katiba iliyopo na Soma ile ya Warioba utapata shule kidogo mkuu.....haya ndio mambo Jaji Warioba aliyaona na akapendekeza matokeo ya Urais yaweza kuhojiwa kwenye SUPREME COURT...kenya wanayo, sisi hatuna.....
 
What are you trying not to say here? Kwanza siwezi kuomba ushauri wowote wa kisheria kwako. Subiri wanasheria wanaojua sheria na tafsiri zake waje. You just fumbling around repeating things without any sound clarifications.

It doesn't necessitate any specialization on legal matters to narrate shallow literature like what you are trying to do here. I would ask you to stay out of the position unayolazimisha kujiweka hapa. Ninahitaji wataalamu wanaoweza kuelewa na kutoa tafsiri siyo shallow knowledge kama ya kwako.

Hope it is clear and you will not any more force your low knowledge into my sphere. Good night honey.
 
Wasubiri watakuja kukuridhisha....goodnit sweetie....
 
Dear hivi una kandoa jamani? Kama bado naweza kuwa mchepuko wako? nita attach CV yangu baada ya ombi langu kukubalika!

Sasa na wwe kandoa tena kanatoka wapi hapa tunatafuta muafaka wa kisheria? Hataki kuwa mchepuko kwanza kwao ni tusi. Labda uongee na mumewe.
 
Ukisikia urais umeendelea kubakwa ndio huu 2015 na 2010.Ndugu zangu tutapewa majibu yaleyale kuwa urais hauhojiwi popote kilingana na katiba hata kama makosa yamefanyika akatanganzwa mshindi mtu ambaye ana kura chache kuwa ndie rais kinyume kabisa na ibara ya 41 kifungu 6,Kwa minajiri hiyo rais wa Tanzania kwa tabia hii atalazimishwa atoke ccm hata kama hakushinda kisheria,hivyo basi kama tabia hii ya kutangaza washindwa ndio washindi imezoeleka basi maamuzi ya mwisho ni UMMA wenyewe kama tulivyoona ktk mataifa mengine.
 
Lakini sijawahi kusikia tafsiri ya kisheria ya Ibara ya 41 kifungu cha 7 ambacho kimeweka bayana kwamba kitasimama tu pale ambapo compliance ya ibara yote itakuwa imezingatiwa.

Kinachosemwagwa na yale maneno ya mwisho ya hitimisho bila kuangalia condition ya hitimisho hilo kwamba matokeo hayatahojiwa iwapo ibara nzima itakuwa imezingatiwa.

Ndiyo maana nikaomba wanasheria watoe ufafanuzi pale anapokuwa ametangazwa mtu bila kuzingatia mahitaji ya ibara nzima.
 
Simply,kwa ufahamu wangu wa sheria,ni kwamba mahakama haitoweza kuingilia maamuzi ya tume endapo tu masharti ya iyo ibara ya 41 yamefuatwa kikamilifu na tume,lakini kinyume chake sasa ikiwa tume haitocomply with provisions and requirements set up under article 41 then mahakama itakuwa na mamlaka ya kuingilia uamuzi huo wa tume ambao haujafata masharti hucka kama yanavoelezwa katika ibara 41...

Sasa, endapo mtu atakuwa na sababu za msingi za kupinga uhalali wa uamuzi wowote utaotolewa na tume kwa kurejea ibara iyo ya 41 basi atakuwa na uwezo wa kupeleka complaints mahakamani for respective order! Kwa iyo hii ni kusema kuwa endapo mtu atatangazwa na tume kuwa raisi bila ya kuzingatia mahitaji ya ibara nzima basi ni wazi kuwa uamuzi huo ni batili na mahakama italift up iyo ouster clause iliyowekwa na katiba na kuweza kuingilia maamuzi hayo ya tume ili haki iyonekane kutendeka.
 
Back
Top Bottom