Ufafanuzi wa kisheria watolewa kufuatia kujiondoa kwa Jaji Elinaza Luvanda kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi wa Freeman Mbowe na wenzake..


Umesikia lakini kuwa Mh. Mbowe alipowasilisha malalamiko yake Jaji aliyaandika kabla ya kutoa uamuzi (ruling)?

Mahakamani kila uamuzi wa jaji au hakimu huenda kwa kifungu cha sheria na wenye kukubali au kukataa hoja husika.

Kujitoa kwa jaji Luvanda kuite wewe usiyejua sheria kwenye kesi yenu ya wizi wa kuku kama unavyotaka. Hakubadilishi kitu.

Kwani pilipili usizozila zikuwashe wewe namna gani bwana mpole mpole?
 
Mtafungwa tu nyie. Ni suala la muda. Mnaleta ukanjanja kwenye weledi. Subiria uone. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Walifungwa kina Mandela, Hakainde, Kenyatta, Odinga, nk.

Waliuawa kina Biko, Mahlangu, Luwum, Aquino, nk.

Walishitakiwa kina Nyerere, Navalny, Kyagulanyi, nk

Lakini bado mapambano yaliendelea.

Vipi "tour de Tanzania" inaendelea je huko?
 
Mimi nilidhani mfano wako utakuwa na jibu! Ungetupa hitimisho la nini kilitokea baada ya kusikilizwa na jaji mwingine.
 

Nchi haiendeshwi kwa sentiments (hisia) kama hizi zako. Nchi huendeshwa kwa mujibu wa katiba.

1. Msajili wa vyama vya siasa ana wajibu gani kwa mujibu wa katiba?
2. Jeshi la polisi lina wajibu gani kwa mujibu wa katiba?
3. Msajili wa vyama siasa asimamishe mikutano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
4. Mkutano wa jeshi la polisi, vyama vya siasa na Msajili wa vyama vya siasa ni kikao kipi kwa mujibu wa katiba?
5. Kwanini ni vigumu kuheshimu katiba?

Hayupo aliye juu ya sheria.

Katiba iheshimiwe.
 
Mtafungwa tu nyie. Ni suala la muda. Mnaleta ukanjanja kwenye weledi. Subiria uone. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mmmh kila usemalo lina kinyume chake

Newton's third lawa of motion

Yawezekana ukafungwa wewe mkuu

Angalia sana, Unaweza wekewa dawa za kulevya nyumbani kwako au Bangi na marafiki Halafu wakakuchoma polisi

Angalia sana maneno yako, Yanaweza yakakutokea wewe na familia yako ikakusahau

Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo katiba ndio inaelekeza kuwe na vikao/mikutano ya kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo au uvunjaji wa sheria/amani, kwahiyo kila aliye na ajenda yake aitishe maandamano. usiwe short cited, Katiba inatoa muongozo wa ujumla wenye nia njema, the rest itakuwa governed na sheria husika kanuni,miongozo,taratibu na busara nyingine.na ndio maana za busara za Jaji Mutungi kukutanisha na kutafuta ufumbuzi na way forward.na ndio mfumo wa utawala bora kwa mujibu wa hiyo hiyo katiba.
 
Cha kufanya ni Mbowe akimaliza kifungo chake cha miaka 30 jela atakayohukumiwa, aache kabisa ugaidi pamoja na wafuasi wake. Akifanya hivyo hakuna atakayemfungulia kesi tena ya ugaidi.
Ninao uhakika hujaelewa ulichoulizwa.
 
Umeshajiuliza kama kuna ushahidi Jamhuri wanasema wanao?, Unafikiri Jaji ageweza kuuacha tu ukaenda na maji?. Jibu ni hapana. Haki ni kwa pande zote mbili haki haipo kwa mshitakiwa tu bali hata mshitaki anayo haki ya kushitaki, unafikiri Jaji angeweza kuivunja iyo haki kirahisi hivyo?

Swali lingine ni mnaposema haki ya Mh. Mbowe imevunjwa ni haki gani hiyo?, Kama ni haki ya yeye kuachiwa huru hiyo haki haiwezekaniki bila Jamhuri kusikilizwa ushahidi wao, sasa utasikilizwaje ndani ya hati ya mashtaka yenye walakini?, Suluhisho ni nini ili Jamhuri asikilizwe?,

Hayo maswali ukiyatafakari utapata standing ya Mh. Luvanda J. wala haitakupa wasi wasi ulio nao sasa ukifahamu kuwa
Popote linapotajwa neno haki ijulikane ni pande mbili sio pande moja Mkuu.
 
Cha kufanya ni Mbowe akimaliza kifungo chake cha miaka 30 jela atakayohukumiwa, aache kabisa ugaidi pamoja na wafuasi wake. Akifanya hivyo hakuna atakayemfungulia kesi tena ya ugaidi.
Umeongea kwa hekima sana.Lakini Mbowe pia ana kesi ya uhujumu uchumi pia
 
Kwa nini serikali imepeleka hati mbovu ya mashtaka?
Maana yake ni kwamba hawana nia ya kumfunga bali kumsumbua kama anavyowasumbua kuandaa makongamano ambayo hawayataki...ni maoni yangu..
 
Ndugu haya maisha yanapita, ombea haki kwa adui na rafiki...
 
Hata sijaelewa umeandika nini. Anyway, walioelewa watanielewesha.
 
Biblia inasema hivi ktk Isaya 1.17 "Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane"

Majaji mmepewa kazi ngumu sana kiimani. Kwa hakika ni bora kujiuzuru ikiwa kama mtatumia nafasi mliopewa kuwaridhisha wateule wenu au watawala.

Sintashangaa kabisa baadhi yenu, mkajauawa hadharani. Neno la Mungu halipiti wakati Ardhi inashuhudia. Tafakarini hayo.
 

Wapi unaposoma popote kwenye bandiko langu haya?:

"katiba ndio inaelekeza kuwe na vikao/mikutano ya kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo au uvunjaji wa sheria/amani,"

Au ni kuota ndoto za mchana ghafla? Au kwenu nyinyi amani na utulivu ni mnapojipa nafasi za kumbambikizia watu kesi kwa raha zenu?

Short cited ni wewe. Kutokuheshimu katiba ndiyo u short cited wenyewe.

Anajuta sasa hivi Alpha Conde kwa kutaka kusigina katiba.

Ukiukwaji Katiba, Tanzania tunafeli Wapi?

Haki, usawa, uhuru na utawala wa kidemokrasia si kwa hisani ya mtu yeyote bali kwa mujibu wa katiba.

Habari ndiyo hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…