Ufafanuzi wa kisheria watolewa kufuatia kujiondoa kwa Jaji Elinaza Luvanda kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi wa Freeman Mbowe na wenzake..

Ufafanuzi wa kisheria watolewa kufuatia kujiondoa kwa Jaji Elinaza Luvanda kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi wa Freeman Mbowe na wenzake..

Kwa vijana wa Chadema, Jaji kujitoa kwenye kesi wanafikiri is a big deal, lakini kumbe ni jambo la kawaida kabisa. Nina rafiki yangu hapa Mwanza ana kesi na mimi ndie mshauri wake kwenye hiyo kesi na wote hatujasomea sheria na hatujui sana sharia, lakini juzi tumepeleka hoja ya kutokuwa na imani na Hakimu na Hakimu amejitoa temepangiwa Hakimu mwingine.

Umesikia lakini kuwa Mh. Mbowe alipowasilisha malalamiko yake Jaji aliyaandika kabla ya kutoa uamuzi (ruling)?

Mahakamani kila uamuzi wa jaji au hakimu huenda kwa kifungu cha sheria na wenye kukubali au kukataa hoja husika.

Kujitoa kwa jaji Luvanda kuite wewe usiyejua sheria kwenye kesi yenu ya wizi wa kuku kama unavyotaka. Hakubadilishi kitu.

Kwani pilipili usizozila zikuwashe wewe namna gani bwana mpole mpole?
 
Mtafungwa tu nyie. Ni suala la muda. Mnaleta ukanjanja kwenye weledi. Subiria uone. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Walifungwa kina Mandela, Hakainde, Kenyatta, Odinga, nk.

Waliuawa kina Biko, Mahlangu, Luwum, Aquino, nk.

Walishitakiwa kina Nyerere, Navalny, Kyagulanyi, nk

Lakini bado mapambano yaliendelea.

Vipi "tour de Tanzania" inaendelea je huko?
 
Kwa vijana wa Chadema, Jaji kujitoa kwenye kesi wanafikiri is a big deal, lakini kumbe ni jambo la kawaida kabisa. Nina rafiki yangu hapa Mwanza ana kesi na mimi ndie mshauri wake kwenye hiyo kesi na wote hatujasomea sheria na hatujui sana sharia, lakini juzi tumepeleka hoja ya kutokuwa na imani na Hakimu na Hakimu amejitoa temepangiwa Hakimu mwingine.
Mimi nilidhani mfano wako utakuwa na jibu! Ungetupa hitimisho la nini kilitokea baada ya kusikilizwa na jaji mwingine.
 
Nafkiri swala la mikutano, wangeheshimu huo wito wa kukutana ma IGP na msajili, kwani unaposema sheria imesema mnapeleka taarifa kwa ocd ni ili kurahisisha mchakato tu lakininuhalisia OCD yupo chini ya RPC na RPC yupo chini ya IJP, hivyo ocd akipigwa stop na wakubwa zake hawezi kukiuka maagizo,hivyo ni vyema mkakutana na top bosses ili kutengeneza namna bora/utaratibu kwa nchi nzima.pia kwa nyongeza ya uelewa mwenye mamlaka na utendaji wa jeshi la polisi ni IJP, hayo mengine ni katika kurahisisha taratibu za utendaji kwani huwezi kutegemea kila kibali/barua zote zielekezwe kwa IJP, ndio maana kuna makamishna,rpcs,ocds,rtos etc

Nchi haiendeshwi kwa sentiments (hisia) kama hizi zako. Nchi huendeshwa kwa mujibu wa katiba.

1. Msajili wa vyama vya siasa ana wajibu gani kwa mujibu wa katiba?
2. Jeshi la polisi lina wajibu gani kwa mujibu wa katiba?
3. Msajili wa vyama siasa asimamishe mikutano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
4. Mkutano wa jeshi la polisi, vyama vya siasa na Msajili wa vyama vya siasa ni kikao kipi kwa mujibu wa katiba?
5. Kwanini ni vigumu kuheshimu katiba?

Hayupo aliye juu ya sheria.

Katiba iheshimiwe.
 
Mtafungwa tu nyie. Ni suala la muda. Mnaleta ukanjanja kwenye weledi. Subiria uone. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mmmh kila usemalo lina kinyume chake

Newton's third lawa of motion

Yawezekana ukafungwa wewe mkuu

Angalia sana, Unaweza wekewa dawa za kulevya nyumbani kwako au Bangi na marafiki Halafu wakakuchoma polisi

Angalia sana maneno yako, Yanaweza yakakutokea wewe na familia yako ikakusahau

Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Nchi haiendeshwi kwa sentiments (hisia) kama hizi zako. Nchi huendeshwa kwa mujibu wa katiba.

1. Msajili wa vyama vya siasa ana wajibu gani kwa mujibu wa katiba?
2. Jeshi la polisi lina wajibu gani kwa mujibu wa katiba?
3. Msajili wa vyama siasa asimamishe mikutano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
4. Mkutano wa jeshi la polisi, vyama vya siasa na Msajili wa vyama vya siasa ni kikao kipi kwa mujibu wa katiba?
5. Kwanini ni vigumu kuheshimu katiba?

Hayupo aliye juu ya sheria.

Katiba iheshimiwe.
Kwahiyo katiba ndio inaelekeza kuwe na vikao/mikutano ya kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo au uvunjaji wa sheria/amani, kwahiyo kila aliye na ajenda yake aitishe maandamano. usiwe short cited, Katiba inatoa muongozo wa ujumla wenye nia njema, the rest itakuwa governed na sheria husika kanuni,miongozo,taratibu na busara nyingine.na ndio maana za busara za Jaji Mutungi kukutanisha na kutafuta ufumbuzi na way forward.na ndio mfumo wa utawala bora kwa mujibu wa hiyo hiyo katiba.
 
Cha kufanya ni Mbowe akimaliza kifungo chake cha miaka 30 jela atakayohukumiwa, aache kabisa ugaidi pamoja na wafuasi wake. Akifanya hivyo hakuna atakayemfungulia kesi tena ya ugaidi.
Ninao uhakika hujaelewa ulichoulizwa.
 
Hali hii hana afya na hasa kwa serikali ya SSH na washirika wake:

1. Jaji kakubaliana na upande wa utetezi kuwa hati ya mashtaka ni batili.
2. Jaji badala ya kutumia busara kuonyesha haki inatendeka kachagua kuwa upande wa mashtaka ili walete nyingine.

Effectively kutokea hapo na katika mazingira haya:

3. Mh. Mbowe yuko ndani pasipokuwa na hati ya mashtaka.
4. Mh. Mbowe yuko ndani kinyume cha sheria na kinyume cha katiba.

Mh. Mbowe kamlalamikia jaji "in person" wasiwasi uliopo kuhusiana na kutenda haki yakiwamo anayotuhumiwa nayo jaji huyu:

5. Jaji kakubaliana na hoja za Mh. Mbowe kujitoa.

Katiba inaendelea kusiginwa chini ya macho ya tuliyempa dhamana ya kuhakikisha inalindwa. Yeye mwenyewe akiwa kwenye "tour" kama zilivyo "Tour de France" au "Tour de Rwanda."

Mwendelezo huu wa kubambikiza watu kesi na kuweka majaji mahsusi wa kuhakikisha mahitajio yenu serikali yanatimilika kinyume cha katiba, kunaendeleza kukuzwa kwa chuki baina ya watu na serikali na baina ya watu na watu.

SSH na washirika wako mnako tupeleka siko tulikokubaliana. Kwamba hamuwajibiki kwetu bali mna ajenda zenu zenye maslahi yenu binafsi?

Hali hii bado tu haiwafikirishi?

Cc: Jumbe Brown zandrano
Umeshajiuliza kama kuna ushahidi Jamhuri wanasema wanao?, Unafikiri Jaji ageweza kuuacha tu ukaenda na maji?. Jibu ni hapana. Haki ni kwa pande zote mbili haki haipo kwa mshitakiwa tu bali hata mshitaki anayo haki ya kushitaki, unafikiri Jaji angeweza kuivunja iyo haki kirahisi hivyo?

Swali lingine ni mnaposema haki ya Mh. Mbowe imevunjwa ni haki gani hiyo?, Kama ni haki ya yeye kuachiwa huru hiyo haki haiwezekaniki bila Jamhuri kusikilizwa ushahidi wao, sasa utasikilizwaje ndani ya hati ya mashtaka yenye walakini?, Suluhisho ni nini ili Jamhuri asikilizwe?,

Hayo maswali ukiyatafakari utapata standing ya Mh. Luvanda J. wala haitakupa wasi wasi ulio nao sasa ukifahamu kuwa
Popote linapotajwa neno haki ijulikane ni pande mbili sio pande moja Mkuu.
 
Cha kufanya ni Mbowe akimaliza kifungo chake cha miaka 30 jela atakayohukumiwa, aache kabisa ugaidi pamoja na wafuasi wake. Akifanya hivyo hakuna atakayemfungulia kesi tena ya ugaidi.
Umeongea kwa hekima sana.Lakini Mbowe pia ana kesi ya uhujumu uchumi pia
 
Kwa nini serikali imepeleka hati mbovu ya mashtaka?
Maana yake ni kwamba hawana nia ya kumfunga bali kumsumbua kama anavyowasumbua kuandaa makongamano ambayo hawayataki...ni maoni yangu..
 
Kwa vijana wa Chadema, Jaji kujitoa kwenye kesi wanafikiri is a big deal, lakini kumbe ni jambo la kawaida kabisa. Nina rafiki yangu hapa Mwanza ana kesi na mimi ndie mshauri wake kwenye hiyo kesi na wote hatujasomea sheria na hatujui sana sharia, lakini juzi tumepeleka hoja ya kutokuwa na imani na Hakimu na Hakimu amejitoa temepangiwa Hakimu mwingine.
Ndugu haya maisha yanapita, ombea haki kwa adui na rafiki...
 
Umesikia lakini kuwa Mh. Mbowe alipowasilisha malalamiko yake Jaji aliyaandika kabla ya kutoa uamuzi (ruling)?

Mahakamani kila uamuzi wa jaji au hakimu huenda kwa kifungu cha wenye kukubali au kukataa hoja husika.

Kujitoa kwa jaji Luvanda kuite wewe usiyejua sheria kwenye kesi yenu ya wizi wa kuku kama unavyotaka. Hakubadilishi kitu.

Kwani pilipili usizozila zikuwashe wewe namna gani bwana mpole mpole?
Hata sijaelewa umeandika nini. Anyway, walioelewa watanielewesha.
 
Kufuatia kujitoa kwa Jaji Elinaza Luvanda anayesikiliza shauri linalowakabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ndugu Freeman A. Mbowe na wenzake watatu katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi iliyoko mahakamu kuu DSM, baada ya mshitakiwa namba 3 Freeman Mbowe kuonesha "kutokuwa na imani" naye, wengi tumekuwa tukitoa maoni yetu hewani bila kuwa na reference ya kisheria....

Katika video hii, mawakili wa mahakama kuu wasomi ndugu Peter Madeleka na Fatuma Karume wanatupa ufahamu wa kisheria jinsi mambo yalivyo na baada ya kuwasikiliza, kila mtu awe huru kutoa maoni yake sasa iwapo ilikuwa ni halali kwa Jaji huyu kujitoa au vinginevyo...
View attachment 1927053
Biblia inasema hivi ktk Isaya 1.17 "Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane"

Majaji mmepewa kazi ngumu sana kiimani. Kwa hakika ni bora kujiuzuru ikiwa kama mtatumia nafasi mliopewa kuwaridhisha wateule wenu au watawala.

Sintashangaa kabisa baadhi yenu, mkajauawa hadharani. Neno la Mungu halipiti wakati Ardhi inashuhudia. Tafakarini hayo.
 
Kwahiyo katiba ndio inaelekeza kuwe na vikao/mikutano ya kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo au uvunjaji wa sheria/amani, kwahiyo kila aliye na ajenda yake aitishe maandamano. usiwe short cited, Katiba inatoa muongozo wa ujumla wenye nia njema, the rest itakuwa governed na sheria husika kanuni,miongozo,taratibu na busara nyingine.na ndio maana za busara za Jaji Mutungi kukutanisha na kutafuta ufumbuzi na way forward.na ndio mfumo wa utawala bora kwa mujibu wa hiyo hiyo katiba.

Wapi unaposoma popote kwenye bandiko langu haya?:

"katiba ndio inaelekeza kuwe na vikao/mikutano ya kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo au uvunjaji wa sheria/amani,"

Au ni kuota ndoto za mchana ghafla? Au kwenu nyinyi amani na utulivu ni mnapojipa nafasi za kumbambikizia watu kesi kwa raha zenu?

Short cited ni wewe. Kutokuheshimu katiba ndiyo u short cited wenyewe.

Anajuta sasa hivi Alpha Conde kwa kutaka kusigina katiba.

Ukiukwaji Katiba, Tanzania tunafeli Wapi?

Haki, usawa, uhuru na utawala wa kidemokrasia si kwa hisani ya mtu yeyote bali kwa mujibu wa katiba.

Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom