Ufafanuzi wa kisheria watolewa kufuatia kujiondoa kwa Jaji Elinaza Luvanda kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi wa Freeman Mbowe na wenzake..

Cha kufanya ni Mbowe akimaliza kifungo chake cha miaka 30 jela atakayohukumiwa, aache kabisa ugaidi pamoja na wafuasi wake. Akifanya hivyo hakuna atakayemfungulia kesi tena ya ugaidi.
Wewe ni muumini wa dini gani?
 
Cha kufanya ni Mbowe akimaliza kifungo chake cha miaka 30 jela atakayohukumiwa, aache kabisa ugaidi pamoja na wafuasi wake. Akifanya hivyo hakuna atakayemfungulia kesi tena ya ugaidi.
Mkuu hongera naona mimba yako umekaribia kuzaa, ikifika muda huo ni kawaida yenu kupata ndoto za ajabu ajabu.
 
The only solution is to have a new constitution for our country.

Partly, it can be a solution...

Moreover, solution ya kupata taifa lenye jamii ya watu bora, waliostaarabika ya kila mtu kujali utu wa mwenzake, ni kuimarisha msingi ya UADILIFU ambao ni KUKUBALI KUONGOZWA NA MUNGU MUUMBA na kumtii yeye peke yake na kutii sheria na maongozi yake...

Ni kwa sababu Mungu ni PENDO na MUNGU NI WA HAKI. Na msingi Wa jamii iliyostaarabika ni UPENDO na HAKI na hapo huleta kutamalaki kwa AMANI katikati ya jamii hiyo...
Na hilo ndilo kaa la moto, ambalo watawala wetu wa CCM hawataki kulimeza!
Haliwezi kuwa kaa la MOTO kama tutaacha na kuukataa UADILIFU. Kumbuka katiba ni utaratibu wa kujisimamia aliojiwekea mwanadamu mwenyewe na yeye huyohuyo anaweza kuupuza utaratibu huo...

Kaa la moto la kweli linaloweza kumwadabisha kila mtu ni UTII WA SHERIA YA UPENDO + HAKI = UADILIFU ambaye msingi wake ni aliyetuumba yaani Mungu Yehova...!
 
alichokifanya jaji ni busara zaidi kuliko angemuachia huru na akakamatwa tena mda huohuo.
Wamkamate wampeleke wapi wakati umeambiwa mahakamani mtu huingizwa huku anayeshtaki akiwa na hati ya mashtaka [Charge sheet] mkononi mwake ili kuipa uhalali mahakama kumshikilia mtuhumiwa wakati ikitafuta ukweli mashtaka/tuhuma hizo...?

By the way, kama serikali/polisi walikaa naye kwa zaidi ya wiki tatu kabla ya kumfikisha mahakamani na bado wakashindwa kutunga mashtaka ipasavyo, watawezaje kwa muda huu ambao kila kitu kiko wazi ktk mwanga angavu...?

Ndugu, hakuna kitu hapo, hakuna kesi hapo, hakuna mashtaka hapo. Ni uhuni na upumbavu tu wa watawala unao swing kupotezea watu muda na kuingizia nchi hasara kwa jambo ambalo halipo kiuhalisia...!
 
Tupe kirefu cha hiyo IJP yako hiyo tafadhali.
 
Hapo hao mawakili wa utetezi inavyoonekana tayari wana details za namna serikali ilivyopanga kuitumia mahakama kukandamiza haki ya mteja wao.

Hilo likitimia kama serikali inavyotaka serikali isifikiri itakuwa mshindi bali wajue kwamba watakuwa wamekalia the timing bomb na matokeo yake yatakuwa ni yale wazungu wanaita "Situational Irony" kwani hii kesi inafuatiliwa sana ndani na nje ya nchi.
 
mnapewa kamba ndefu lakini ndo yuko ndani hivyo huyo gaidi

Kwani inaondoa ukweli kuwa hana makosa yoyote...?

Wanamuumiza Freeman Mbowe kimwili na kumnyima Uhuru wake kwa muda tu huku roho na nafsi yake ikiwa na amani tele....

Lakini maumivu na hukumu ya mtu au nafsi na roho itendayo ubaya kwa nafsi/mtu asiye na hatia ni mabaya na ya milele...!!

Ukitaka kujua hili soma historia ya waliowahi kudhulumu uhai Wa nafsi za watu uone wanavyoteseka...

Mfano mkuu kuliko yote ulimwenguni ni wa Yesu Kristo...

Huyu alishtakiwa, kuteswa na kuhukumiwa kwa makosa ya kutunga, ya uongo ambayo hakuwahi kuyatenda na wajinga waliofurahia na kushabikia kama wewe walikuwepo.. Waulize waliotenda uovu huo leo wana hali gani...
 
mkuu si vyema kutoa conclusion kabla kesi haijaanza, kinachopambaniwa sasa hivi ni hati tu

kesi yenyewe ya msingi bado haijaanza kutolewa ushahidi

so kwa namna yeyote ile hata kama jaji angemuachia huru, ni lazima angekamatwa hapo hapo

kwasababu serikali bado ina interest nae kwenye ile kesi ya msingi

kukosewa kwa hati ya mashitaka hakumuondolei makosa ndugu yetu

kinachofanywa na mawakili wa utetezi ni tactics za kawaida kabisa kisheria, ambazo kiuhalisia zinachelewesha kesi tu na si kuondoa kosa la msingi mtuhumiwa(niko tayari kurekebishwa)
 
Marais wanatumia fursa iliyopo kwenye hii katiba mbovu kuteua majaji ambao hawana sifa ili mradi tu wakalinde maslahi yao ndio maana wengine kama hawa wanatolewa Tiss na kutunukiwa ujaji bila kuwa na sifa ya kuwa jaji.

Ninachoona kumkataa huyo jaji, japo sio ufumbuzi, kwa maana hata huyo atakayeletwa atakuwa ni wale wale lakini inafanya dunia iamke na kufahamu kwamba Tanzania tuna majaji wa aina gani.
 
Imeeleweka. Mbowe kashikiriwa bila "proper charges". Huu ni mwendelezo wa uvunjifu wa katiba na haki za binadamu. "It is a pity to be a citizen of this country".
 
Sioni kama marehemu atafufuka hapa mnachelewesha mazishi , kurefusha matanga na kuwachosa walala matanga
Mna uzoefu sana na marehemu kutofufuka, maana yule wenu hata bishop Rashidi, hakuweza kumfufua!
 
Hilo ndilo swali kubwa hivi sasa.

Na hiyo ndiyo uthibitisho usio na shaka yoyote kuwa hiyo kesi ya Mbowe ni ya kubambika!
Kama hawana ushahidi lazima hati ya mashtaka kuwa na mapungufu
 
Kuna usahihi fulani kwenye maelezo yako, lakini nikupe tu taarifa kwamba, kama unaiamini Bible, Torati yote ndo katiba ya Israel na taifa la Israel ni kielelezo cha jinsi ya kujenga taifa!
Ili watu wawe na uadilifu na ustaarabu lazima watii sheria za Mungu, Sawa! Sheria za Mungu zipi? Ten Testament? Amri kumi zenyewe zinahusu mahusiano kati ya Mungu na watu, na pia watu wao kwa wao!

Hivyo basi, katiba mpya ni muhimu, lakini izingatie kwamba kuna Mungu, kwa hiyo serikali ilimiti mamlaka yake kwa kujua kwamba kuna mamlaka kubwa zaidi! Pili wathamini utu kwa kutambua binadamu wote ni Sawa, kwamba wao hawapo juu ya sheria, bali wote Tupo chini ya sheria moja!

Hizo hapo juu ni sheria za Mungu, ni mapenzi yake na tukizifuata tutakuwa simply, taifa takatifu lenye uadilifu na ustaarabu!
 
Yaani ukisikiliza hii space ya maria kuna wanashria wa ajabu wanatafsiri sheria kinyumenyume...kuna wakati mpaka karume anaingilia kuwasahihisha ....kuna mwingine anaongea mambo ya double jeopardize ya marekani bila kujua sisi tunatumia common law system na principle kama hizo zipo za RESJUDICATA , RES SUBJUDICE , AUTREFOIS CONVICTO, AUTREFOIS CONVICTO zipo na zina standands zake sasa pale.wanasheria wanapobadilika kuwa wanaharakati matokeo yake ni kuwalisha jamii matangopori
 

Katiba huundwa kwa maana kamili iliyokusudiwa inayokuwa kwenye kifungu kwa kifungu. Panapotokea sintofahamu kuhusu chochote mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kutoa tafsiri sahihi.

Katika kufikia tafsiri sahihi si nadra kwa mahakama kupata mawazo ya yaliyo kusudiwa katika kifungu husika, kutoka kwa waliokuwa waandishi wa katiba husika.

Hapa chini ni baadhi ya vichochoro vingi vilivyoko kwenye katiba yetu kama yalivyoelezwa na mzee Kingunge mmoja katika waadishi wa katiba hii 1977:



Huenda hata DRC aliyetangazwa kuwa mshindi wa urais, hakuwa mshindi halali.

Vipo vichochoro vingi kwenye katiba yetu vinavyowawezesha wakanyaga katiba kutowajibika na hata kutowajibishwa tu.

Kwenye hali kama za kwetu ambako kuna mhimili uliojichimbia zaidi, si ajabu hata kwa tafsiri zilizo wazi kuvutiwa kokote ili ku justify the end kama unavyojaribu kufanya wewe.

Humo ndimo ulipo sasa msingi wa mahitaji ya katiba mpya. Katiba itakayo fft thehakikisha uhuru wa kamili wa m ihimili kama msingi mkuu wa haki, usawa na haki ambapo utawala wa kidemokrasia utajengeka.

Tuko kwenye zama nyingine hizi ambazo ujanja ujanja hauna nafasi tena.
 

Kwani jaji ni sehemu ya mashitaka?

Kwani jaji alipo ana ushahidi wowote dhidi ya Mbowe?

Tofautisha jaji na Jamhuri mahakamani. Zingatia haki za kila upande pasipo na sheria yoyote kukiukwa.

Utaratibu kisheria kwenye hali kama hizi ambapo charge sheet haipo, mtuhumiwa huachiwa akakamatwa tena baada ya kutoka mahakamani.

Kumbuka wenye ushahidi ni kurugenzi ya upelelezi polisi (DCI) na kurugenzi ya mashtaka (DPP) pekee.

Tulipo sasa Mbowe yuko ndani pasipokuwa na charge sheet kinyume cha sheria. Kwa misingi hii haki ya mshitakiwa umekiukwa kinyume cha sheria. Katiba imekanyagwa na huo ndiyo ulio ukweli wenyewe.

Karibu kwenye uwanja wa sheria na misingi ya utoaji haki.

Achana na hadithi za vijiweni.
 
Sasa wote hamjui sheria na wewe ndo mshauri huoni kama ni bomu tu linasubiri kulipuka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…