Ufafanuzi wa kisheria watolewa kufuatia kujiondoa kwa Jaji Elinaza Luvanda kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi wa Freeman Mbowe na wenzake..

Kwani jaji ni sehemu ya mashitaka?

Kwani jaji alipo ana ushahidi wowote dhidi ya Mbowe?

Tofautisha jaji na Jamhuri mahakamani. Zingatia haki za kila upande pasipo na sheria yoyote kukiukwa.

Utaratibu kisheria kwenye hali kama hizi ambapo charge sheet haipo, mtuhumiwa huachiwa akakamatwa tena baada ya kutoka mahakamani.

Kumbuka wenye ushahidi ni kurugenzi ya upelelezi polisi (DCI) na kurugenzi ya mashtaka (DPP) pekee.

Tulipo sasa Mbowe yuko ndani pasipokuwa na charge sheet kinyume cha sheria. Kwa misingi hii haki ya mshitakiwa umekiukwa kinyume cha sheria. Katiba imekanyagwa na huo ndiyo ulio ukweli wenyewe.

Karibu kwenye uwanja wa sheria na misingi ya utoaji haki.

Achana na hadithi za vijiweni.
Mkuu unajua kuwa kuendelea na charge yenye makosa inapelekea 'unfair trial'?
unaua ni wakati gani mtuhumiwa anaweza kufutiwa mashtaka yanayomkabili?, hayo mazingira kwa Mh. Mbowe yanajitosheleza?
kama hayajitoshelezi unajua nini kifanyike ili kusiwe na 'unfair trial' na kipo kwenye mkono wa nani?

unless uniambie kuwa ku amend charge ni practice iliyoanza jana kwa Luvanda J., tofauti na hapo uwe ni shabiki/umeokoteza stori za kijiweni Mkuu.
 
mkuu si vyema kutoa conclusion kabla kesi haijaanza, kinachopambaniwa sasa hivi ni hati tu

kesi yenyewe ya msingi bado haijaanza kutolewa ushahidi

so kwa namna yeyote ile hata kama jaji angemuachia huru, ni lazima angekamatwa hapo hapo

kwasababu serikali bado ina interest nae kwenye ile kesi ya msingi

kukosewa kwa hati ya mashitaka hakumuondolei makosa ndugu yetu

kinachofanywa na mawakili wa utetezi ni tactics za kawaida kabisa kisheria, ambazo kiuhalisia zinachelewesha kesi tu na si kuondoa kosa la msingi mtuhumiwa(niko tayari kurekebishwa)
Kwa hiyo hao mawakili wa Jamuhuri hawajui kuwa hawajui kwa sababu mpaka sasa hawajaomba kubadilisha hati ya mashtaka! Kama kosa lipo na ushahidi wanao mawakili wa Jamuhuri wanashindwaje kuandika kosa na maelezo sahihi ili kesi iendelee kusikilizwa?
 
Hii kesi serikali haina ujanja. Kwa tukio hili, sasa imethibitika bila shaka kuwa hii kesi ni ya kubumba...

Lolote litakalotokea, WATU WOTE DUNIANI KOTE NA WAJUE HIVYO...!

By the way, kila mtu alishangaa sana kwa Jaji huyu kujitoa kirahisi kwa namna ile kwa hoja za mshtakiwa jambo ambalo huwa ni gumu sana kwa mahakimu/majaji wengi unless kuwe na debate ili kuthibitisha sababu ya kumtaka Jaji/hakimu kukaa pembeni....

Ni wazi serikali inawapa wakati mgumu sana majaji/mahakimu pale inapowatengenezea mazingira ya kuwalazimisha kupindisha sheria na haki ktk mahakama zetu kwa maslahi ya watawala...

Hii Mungu haipendi na haitaki asilani. Lazima wapigwe upofu na wapoteane kabisa...

Kuendelea kumshikilia mtuhumiwa bila charge sheet haina tofauti na kesi ya Yesu mbele ya Pilato.

"Sioni hatia mbele ya mtu huyu" -- akasisitiza Pilato.

Jaji Luvanda anapata kigugumizi cha utendaji kwa sababu anatakiwa kuhalalisha ku justify the end.

Unayafanyaje hayo ukiwa umeshastukiwa
 
Kwa vijana wa Chadema, Jaji kujitoa kwenye kesi wanafikiri is a big deal, lakini kumbe ni jambo la kawaida kabisa. Nina rafiki yangu hapa Mwanza ana kesi na mimi ndie mshauri wake kwenye hiyo kesi na wote hatujasomea sheria na hatujui sana sharia, lakini juzi tumepeleka hoja ya kutokuwa na imani na Hakimu na Hakimu amejitoa temepangiwa Hakimu mwingine.
Tatizo sio hakimu kujiotoa, ni hati ya mashtaka.
Hatukulaumu kwa vile umesema haujasoma sheria, tunakulaumu kujitia kimbelembele na kumpa ushauri rafiki yako na hali ya kuwa unajijua kama wewe ni mbumbu.
Huyo rafiki kwa kutegemea ushauri wako hata kama hana kosa ataishia jela tu.
 
Kwa hiyo hao mawakili wa Jamuhuri hawajui kuwa hawajui kwa sababu mpaka sasa hawajaomba kubadilisha hati ya mashtaka! Kama kosa lipo na ushahidi wanao mawakili wa Jamuhuri wanashindwaje kuandika kosa na maelezo sahihi ili kesi iendelee kusikilizwa?
hii ni issue mhimu, lakini haikusaidii kukwepa kosa la msingi kama lipo,

maana hati itarekebishwa na utakamatwa tena.
 
Kuendelea kumshikilia mtuhumiwa bila charge sheet haina tofauti na kesi ya Yesu mbele ya Pilato.

"Sioni hatia mbele ya mtu huyu" -- akasisitiza Pilato.

Jaji Luvanda anapata kigugumizi cha utendaji kwa sababu anatakiwa kuhalalisha ku justify the end.

Unayafanyaje hayo ukiwa umeshastukiwa
Mahabusu siyo ya Mahakama; anayetaka Gaidi awe huru aende kuomba kibali Polisi
 
Mkuu unajua kuwa kuendelea na charge yenye makosa inapelekea 'unfair trial'?
unaua ni wakati gani mtuhumiwa anaweza kufutiwa mashtaka yanayomkabili?, hayo mazingira kwa Mh. Mbowe yanajitosheleza?
kama hayajitoshelezi unajua nini kifanyike ili kusiwe na 'unfair trial' na kipo kwenye mkono wa nani?

unless uniambie kuwa ku amend charge ni practice iliyoanza jana kwa Luvanda J., tofauti na hapo uwe ni shabiki/umeokoteza stori za kijiweni Mkuu.

Hujawahi kusikia washitakiwa wameachiwa huru na mahakama au wamefutiwa mashtaka lakini wakakamatwa mara tu baada ya kuweka mguu nje ya mahakama?

Hudhani "for the sake of impartiality" hii ndiyo iliyo kuwa njia sahihi zaidi kwa jaji huyu ambaye amegubikwa na tuhuma za kuwa mjumbe kindaki ndaki wa tiss mahakamani ku justify the end, kujiwekea imani kuwa ni wa kuaminika huku akiwapa nafasi prosecution kufanya yao?

Anayeomba charge sheet kubatilishwa ni jaji baada ya kuwa prosecution wamekomaa kuwa charge sheet yao ni timamu?

Mwenye wajibu wa kuhakikisha charge sheet iko sahihi ni jaji kwa ajili ya kesi kuendelea?

Kwani mshitakiwa anashitakiwa na jaji au prosecutor?

"Tender? Tender gani? Si mseme tu CRDB wamechukua lori lao?"
 
mkuu si vyema kutoa conclusion kabla kesi haijaanza, kinachopambaniwa sasa hivi ni hati tu
Ingekuwa bora ungejielekeza kujibu msingi wa malalamiko ya mawakili upande wa utetezi...

Hakuna mtu ametoa conclusion ndugu...

Kama unasikiliza na kufuatilia mjadala huu kwa makini, unaweza kujua mara moja kuwa, kinacholeta shida ktk kesi hii hatua kwa hatua ni Jaji kuonesha dalili zote za kuwa biased akiweka giza kwa haki kuonekana ikitendeka na ndiyo maana washtakiwa wamesema wazi mbele yake kuwa hawana imani naye, dhamiri yake ikamshtaki na akakubali kukaa pembeni...
kesi yenyewe ya msingi bado haijaanza kutolewa ushahidi

Wote tunajua hili...
so kwa namna yeyote ile hata kama jaji angemuachia huru, ni lazima angekamatwa hapo hapo
Unarudi kulekule.

Hii siyo kazi ya hakimu/Jaji, ni kazi ya polisi na mwendesha mashtaka wao. Hata kama watamkamata mtuhumiwa mara 20....!

Kati hatua yoyote, kazi ya hakimu/Jaji ni kuitolea maamuzi hoja yoyote iliyo mbele yake kwa mujibu wa sheria...

Katika hatua hiyo, ishu ilikuwa ni Charge sheet kama inakidhi vigezo vya kisheria au la....

Jaji mwenyewe akafanya ruling kuwa, haina hadhi kisheria na kwa hatua hiyo maana yake, hakuna offence, hakuna mshtakiwa...!

Ni kipi tusichoelewana mpaka hapo...?
kwasababu serikali bado ina interest nae kwenye ile kesi ya msingi

Yes, hakuna abishae. Ifuate sheria na imlete mtuhumiwa tena na tena lakini KWA KUZINGATIA TARATIBU NA SHERIA. Huu ndiyo msisitizo...!!
kukosewa kwa hati ya mashitaka hakumuondolei makosa ndugu yetu

Yes, hakuna anayebisha. Fuata utaratibu na sheria sasa kumpeleka mahakamani na kumshtaki. Ni hilo tu boss. Mbona huelewi...?
kinachofanywa na mawakili wa utetezi ni tactics za kawaida kabisa kisheria, ambazo kiuhalisia zinachelewesha kesi tu na si kuondoa kosa la msingi mtuhumiwa(niko tayari kurekebishwa)
Wewe ndiyo unaelewa hivyo kuwa ni "tactics" za kuchelewesha lakini walio jikoni wanajua nini wafanyacho na maana yake...

Nyakubonga, sikiliza kidogo. From the first place, mawakili wa utetezi na ule wa mashtaka wote wanajua kuwa hii kesi ni ya kutengenezwa na haina uhalisia wowote...

Makosa haya kijinga unayoyaona na kuleta sintofahamu hii ni kwa sababu msingi wake ni UONGO WA KESI...!

Sasa upande wa defense, wanaujua mchezo vizuri zaidi. Wakataka kuumaliza mapema na kujenga hoja hiyo. Na infact hata mawakili wa upande wa mashtaka wanajua kuwa ni ngumu kujenga hoja ktk mashtaka ya uongo na indirectly wanakiri kushindwa...

Tatizo liko kwa mahakama/hakimu anayeshinikizwa kufanya maamuzi nje ya haki na sheria. Hapa ndipo kilipo chanzo cha shida yote hii...!
 
ishu ilikuwa ni Charge sheet kama inakidhi vigezo vya kisheria au la....

Jaji mwenyewe akafanya ruling kuwa, haina hadhi kisheria na kwa hatua hiyo maana yake, hakuna offence, hakuna mshtakiwa...!
kwingine nimekuelewa ila hapa...

endelea kutoa ufafanuzi wa kisheria...

je hati ikikosewa inatoa mwanya wa kuondolewa kwa kosa?
 
Ingekuwa bora ungejielekeza kujibu msingi wa malalamiko ya mawakili upande wa utetezi...

Hakuna mtu ametoa conclusion ndugu...

Kama unasikiliza na kufuatilia mjadala huu kwa makini, unaweza kujua mara moja kuwa, kinacholeta shida ktk kesi hii hatua kwa hatua ni Jaji kuonesha dalili zote za kuwa biased akiweka giza kwa haki kuonekana ikitendeka na ndiyo maana washtakiwa wamesema wazi mbele yake kuwa hawana imani naye, dhamiri yake ikamshtaki na akakubali kukaa pembeni...

Wote tunajua hili...

Unarudi kulekule.

Hii siyo kazi ya hakimu/Jaji, ni kazi ya polisi na mwendesha mashtaka wao. Hata kama watamkamata mtuhumiwa mara 20....!

Kati hatua yoyote, kazi ya hakimu/Jaji ni kuitolea maamuzi hoja yoyote iliyo mbele yake kwa mujibu wa sheria...

Katika hatua hiyo, ishu ilikuwa ni Charge sheet kama inakidhi vigezo vya kisheria au la....

Jaji mwenyewe akafanya ruling kuwa, haina hadhi kisheria na kwa hatua hiyo maana yake, hakuna offence, hakuna mshtakiwa...!

Ni kipi tusichoelewana mpaka hapo...?

Yes, hakuna abishae. Ifuate sheria na imlete mtuhumiwa tena na tena lakini KWA KUZINGATIA TARATIBU NA SHERIA. Huu ndiyo msisitizo...!!

Yes, hakuna anayebisha. Fuata utaratibu na sheria sasa kumpeleka mahakamani na kumshtaki. Ni hilo tu boss. Mbona huelewi...?

Wewe ndiyo unaelewa hivyo kuwa ni "tactics" za kuchelewesha lakini walio jikoni wanajua nini wafanyacho na maana yake...

Nyakubonga, sikiliza kidogo. From the first place, mawakili wa utetezi na ule wa mashtaka wote wanajua kuwa hii kesi ni ya kutengenezwa na haina uhalisia wowote...

Makosa haya kijinga unayoyaona na kuleta sintofahamu hii ni kwa sababu msingi wake ni UONGO WA KESI...!

Sasa upande wa defense, wanaujua mchezo vizuri zaidi. Wakataka kuumaliza mapema na kujenga hoja hiyo. Na infact hata mawakili wa upande wa mashtaka wanajua kuwa ni ngumu kujenga hoja ktk mashtaka ya uongo na indirectly wanakiri kushindwa...

Tatizo liko kwa mahakama/hakimu anayeshinikizwa kufanya maamuzi nje ya haki na sheria. Hapa ndipo kilipo chanzo cha shida yote hii...!
Huna jipya mkuu wewe ni jiwe tu linalotoa mwangwi- fikiri utuambiwe mawazo yako wewe kama wewe siyo ya mwiigizaji Kibatala ambaye amesahihishwa vizuri na shangazi Fatuma
 
Walifungwa kina Mandela, Hakainde, Kenyatta, Odinga, nk.

Waliuawa kina Biko, Mahlangu, Luwum, Aquino, nk.

Walishitakiwa kina Nyerere, Navalny, Kyagulanyi, nk

Lakini bado mapambano yaliendelea.

Vipi "tour de Tanzania" inaendelea je huko?
Mama akimaliza huko anaanza kuandaa tamasha la mwaka kogwa ambalo kama kawaida atalisimamia mwenyewe.
 
Kwa vijana wa Chadema, Jaji kujitoa kwenye kesi wanafikiri is a big deal, lakini kumbe ni jambo la kawaida kabisa. Nina rafiki yangu hapa Mwanza ana kesi na mimi ndie mshauri wake kwenye hiyo kesi na wote hatujasomea sheria na hatujui sana sharia, lakini juzi tumepeleka hoja ya kutokuwa na imani na Hakimu na Hakimu amejitoa temepangiwa Hakimu mwingine.
MWANGALUKA.......
 
Huna jipya mkuu wewe ni jiwe tu linalotoa mwangwi- fikiri utuambiwe mawazo yako wewe kama wewe siyo ya mwiigizaji Kibatala ambaye amesahihishwa vizuri na shangazi Fatuma
Kwani, ni sababu gani ilimfanya mwendesha mashtaka wa serikali asiandae hati ya mashtaka [charge sheet] inayokidhi vigezo vya kisheria kabla ya kuipeleka mahakamani...?

Najua utajiuma uma tu kutoa jibu sahihi. Sasa mimi nakusaidia jibu lake;

Ni kwa sababu mashtaka ni ya uoñgo, ni ya kubumba na kesi yote kuwa ni ya kukomoa na hila tu dhidi ya CHADEMA na Freeman Mbowe...!

Kama unaweza kukanusha, karibu...
 
Kaka tatizo tunakuwa wanaharakati zaidi bila kujua namna ya kutafsiri haki za kikatiba, naomba usome ibara ya 30 ya katiba utaelewa vizuri andiko langu.kikubwa ni kuwa haki,uhuru haviko absolute, kwamba kwakuwa una haki ya mikutano ama maandamano sasa ukaonyesha na viashiria vya kuvunja amani/utulivu kwa mwamvuli wa katiba, uzuri sasa katiba yenyewe imetoa exceptions to the general rule and that is article 30... na ndio maana kuna vyombo na taasisi za serikali ambazo zimepewa jukumu la kuweka law and order in case ya viashiria vyovyote. be so informed
Kama kuna viashiria vya uvunjifu wa amani tatizo liko wapi kama kuna vyombo vya ulinzi na usalama? mbona mnaandika vitu msivyovielewa, hapa hakuna sababu ya kuleta vifungu vya sheria, jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama ni kulinda raia na mali zao, mengine ya general rule mnaandika tu kuwachanganya wasiojua sheria.
 
Back
Top Bottom