Ufafanuzi wa kufutwa kwa VRF kwa wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, waajiriwa tegemeeni kuongezeka kwa take home

Nimekusoma wewe ndio umetoa maelezo mazuri kuliko hayo ya bodi hapo juu
 
Vyovyote itakavyokuwa, namshukuru Mwenyezi Mungu kutuletea Mama Samia kuwa Rais.

Ndani ya mwezi mmoja wa uongozi wake tayari keshanishushia mzigo wa zaidi ya milioni 6 ambao ni hizo faini na riba haramu za mkopo ambazo Mwendazake na Ndungai walipitisha!
 
Kama 6% kila mwezi inaenda kulipa VRF sasa haya madeni mapya yanatokea wapi baada ya kumaliza deni awali.
Sidhani hata kama bodi wana rekodi sahihi ya data zake. Nafikiri mwezi wa saba kutakuwa na malalamiko mengi baada ya kuweka data mpya
 
Mm deni langu lilikua 7.3m baada ya kuweka VRF admistration fee na Panalti likafika 13.6m..swali je
Deni langu litarudi kwenye 7.3m au ndo litabaki kwenye 13.6 na halitaongezeka?
13.6m ukitoa 7.3m unapata 6.3m yaani ni zaidi ya kukopa benki. Nikiwaza hivi napata hasira sana.

Mungu asante, umeyajibu maombi yetu.
 
Wabunge wa CCM walisema NDIOOOO kupitisha mswada
Yaani mkuu acha tu.

Walikuwa wameshikwa masikio. Leo wanageuka na kushangaa eti walipitisha vipi? Kuna jamaa zangu wawili hii ishu imewaumiza sana kila tukikutana wananiambia hawawezi kumsahau kayafa...
 
Hapo kwenye maelezo yako mkuu nikuulize.
Mfano ulikua na deni la 12mil, baada ya gharama hizo zingine kuongezeka deni likafikia 16mil. Je, hio 1%, 6% na 10% ndiyo zimefikisha deni la 16mil? Au hio 6% haionekani kwenye 16mil?
 
Hapo kwenye maelezo yako mkuu nikuulize.
Mfano ulikua na deni la 12mil, baada ya gharama hizo zingine kuongezeka deni likafikia 16mil. Je, hio 1%, 6% na 10% ndiyo zimefikisha deni la 16mil? Au hio 6% haionekani kwenye 16mil?
Hii 6% mara nyingi hawaiweki kwenye slip sababu kila mwaka inabadilika kwahiyo haiwezekani kila mwaka wakaupdate hazina.
 
Nipo tayari kupokea deni jipya baada ya marekebisho yatokanayo na agizo la Mama Mh.Rais SSH.
Mungu amjalie maisha mema na marefu.
 
Retention fees bado watu wanakatwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…