Ufafanuzi wa notisi zilizotolewa kwa vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Enguserosambu, Arash na Losoito

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kutokana na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu notisi zilizotolewa tarehe 4 Juni, 2026 na Ofisi ya Msajili wa Hati Mkoa wa Arusha kwa Vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Enguserosambu, Arash na Losoito vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.

Notisi zilizotolewa zililenga kurekebisha Daftari la Msajili ili kuondoa kumbukumbu za usajili wa Hatimiliki zilizotolewa kwa Vijiji hivyo kabla ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Sura ya 114.

Utaratibu wa kurekebisha Daftari la Kumbukumbu za Usajili ulilenga kuondoa Hatimiliki na kubakisha Cheti cha Ardhi ya Kijiji kinachotoa mamlaka kwa Halmashauri za Vijiji hivyo kusimamia ardhi kwa ajili ya wanakijiji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Sura ya 114.

Utaratibu huu umekuwa ukitumika katika vijiji vingine nchini vilivyokuwa na Hatimiliki kabla ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Sura ya 114. Utaratibu wa kurekebisha daftari la usajili utakapokamilika, Vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Enguserosambu, Arash na Losoito vitabaki na vyeti vya ardhi ya Kijiji ambavyo ndio nyaraka rasmi inayoipa halmashauri ya vijiji vyao mamlaka ya kusimamia ardhi kwa manufaa ya wanakijiji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Sura ya 114.

Wizara inawataka wananchi kupuuza upotoshaji wowote unaotolewa kuhusiana na mchakato huo kwamba unania ya kuchukua ardhi za Vijiji tajwa na kuipeleka kwenye Mamlaka nyingine ya usimamizi, Mwekezaji au mwananchi yeyote.

TAARIFA KWA UMMA

IMG-20260713-WA0077.jpg

Pia soma Namba moja ajimilikisha kijiji cha Ololosokwan, Ngorongoro
 
Hivi kwa nini watu wa sekta ya ardhi hawajali wateja wao? Wanapenda sana kuwazungusha wanaofika kwenye ofisi zao kwa masuala yanayohusu ardhi.

Mfano nimenunua kiwanja toka halmashauri kwa kufanya malipo yote ikiwemo gharama/fedha za kumilikishwa (hati ya kiwanja) lakini mpaka sasa ni zaidi ya mwaka mmoja sijapatiwa hati. Kila ukienda kufuatilia wanatoa sababu zisizoeleweka.

Niliwahi kumsikia waziri wa ardhi akisema kwamba hati inapatikana ndani ya muda mfupi (nafikiri saa 48 kama sikosei), hata hivyo hali ni tofauti sana. Nimefuatilia hati kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa lakini mpaka leo sijapewa na wala sipewe sababu za msingi za kutopatiwa hati.

Inaumiza sana kila siku kwenda halmashauri kufuatilia hati bila mafanikio yoyote, leo ukienda unaambiwa mkurugenzi kasafiri, kesho unaambiwa bado haijawekwa kwenye mfumo, mara file halijarudi toka ofisi ya mkurugenzi, dah 😢 😢 😭

Kuna wakati najuta kununua kiwanja kupitia halmashauri (ofisi ya mkurugenzi), naona bora hata ningenunua kupitia madalali kwa sababu kuna watu wamenunua kupitia madalali na wakafanikiwa mapema zaidi.

Mimi ni mteja wao ambaye natakiwa kulipia kodi ya ardhi kila mwaka pamoja na kufanya maendeleo binafsi lakini wao hawajali, kila nikienda naambiwa njoo baada ya wiki, wiki mbili mara mwezi lakini kote huko hakuna hati wala sababu za kueleweka.
 
Kiukweli hawa CCM hawana nia yeyote ya kumkomboa mTanzania kwa hali yeyote, wamejaa ubinafsi, nio ovu na kujilimbikizia mali.

Notisi ya barua za kwanza haziendani na huu upumbavu unaoitwa ufafanuzi. Utapeli mwanzo mwisho.
WhatsApp Image 2026-07-14 at 1.33.08 PM.jpeg
 
Back
Top Bottom