Ufafanuzi wa tozo sijaelewa zaidi ya kumung'unya maneno

Ufafanuzi wa tozo sijaelewa zaidi ya kumung'unya maneno

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Salama wandugu
Nimemsikiliza Mwigulu akijieleza kuhusu tozo hakuna cha maana anachoeleza zaidi ya kumung'unya maneno
tulishasema ondoeni tozo siyo kuilemba lemba na kuipaka wanja ionekane kama asali wakati ni pilipili,kodi zilizopo zinatosha kuendesha nchi ila nyie mnacheka na wafanyabiashara.
Mmeruhusu matumizi mabovu hamkujifunza kwa JPM alizuia hata safari za nje ambazo hazina Tija kwa taifa.
Mmejazwa ujinga na mabeberu kwamba serikali ijitoe kwenye kuwekeza halafu mtegemee kukusanya kodi,
wenzenu mabeberu wana makampuni ambayo yapo chini ya serikali na faida inaingia serikalini.

NB Leo hii Russia asingekuwa na jeuri ya kukata gesi ulaya kama angeachia sekta binafsi .

Russian state-backed energy firm Gazprom is poised to hand a bumper £8.6bn payout to the Kremlin after notching up record profits.
 
Ni kweli hata Mimi sijaelewa. Ila hapo ulipo taja MAGUFULI ndio umeharibu Kila KITU. Seriously MAGUFULI hata kama angekuwa anatulipa mshahara Kila mtanzania bila kufanya kazi. Bado hakutakiwa kuwa rais yeye NDIO chanzo cha upuuzi wote huu unaoendelea
 
Nimefuatilia maelezo ya Serikali kupitia mawaziri kama yalivyotolewa leo kuhusu malalamiko na uashauri mbalimbali kutoka kwa wananchi kuhusu tozo mbalimbali.
Nadhani ni mapema mno kusema kama maelezo ya Serikali yamejitosheleza au la kwa kuwa kuna mambo ambayo Serikali imeahidi kuyatolea ufumbuzi siku chache zijazo.
Ila kuna jambo moja tu mhimu ingawa limetolewa mwishoni kabisa mwa mjadala huu.
Kwa kusema kwamba mijadala kama hii iwe inafanyika mara kwa mara, kwangu ni kambo muhimu sana kuliko mambo karibu yote yaliyotollewa na Serikali katika mjadala huo.
Hii itapunguza sintofahamu nyingi zinazowakabili wananchi hasa maisha yao yanapokuwa magumu kitokana na sera au hatua za kouchumi ambazo zonachukuliwa na Sreikali katika uendeshaji wa nchi.
Kunapokuwa na ukimya wa Serikali kunaleta mkanganyiko na kuzua mtafaruku mkubwa sana miongoni mwa wananchi.
Pia katika mijadala hii, serikali isiwe msemaji mkuu bali iruhusu wananchi kupitia waandishi wa habari kuuliza maswali mengi iwezekanavyo na Serikali iyatolee majibu na ufafanuzi wa kina
Hii itasaidia si kwa Wananchi tu kupata ufahamu na utanduzi wa matatizo yao, bali hata Serikali itapata manufaa mengi yatakayoipa mwongozo hata wa kutunga sera na sheria mbalimbali kulingana na mahitaji halisi ya wananchi wake.
 
Back
Top Bottom