Ufahamu kuhusu kulangua mpunga.

Du mkuu wapi huko unaponunulia, maana mi nilikuwa shinyanga juzi gharama kama ifuatavyo
1.Bei 60,000
2.Usafiri 2000
3.Upakiaji pandisha +shusha 1000
Hamna ushuru, pia gharama za kutunza bure maana unakobolea hapo hapo. nasikia igunga bei iko 36,000/gunia japo sina uhakika
 
sio kwamba nipo nanua ila kwa hizo ni bei za mpanda,sio kweli kwa igunda kuwa bei hiyo wakati nasikia watu wengi wa kahama wamekimbila mpanda na ndio wameufanya hata upande bei!!wakati kipindi cha nyuma kwa sasa bei huwa ni 30,000-35,000!!ila nasikia kuna katazo la kutoa mpunga mkoa wakatavi ,linakuja muda c mrefu bali ni mchele tu
 
ok kwa mpanda sawa, bei inakuwaga chini
 
ha ha ha,kila biashara sasa ni pasua kichwa,bora kulima mwenyewe tu
 
ivi gunia mojaa la mpunga ukikoboa unapata wastani wa kilo ngp za mchele
 
Kuna aina za mipunga lazima ujue na upi una soko sanaa... Na ujue kukoboa kwa kutumia mikono kuona huu unafaa ama haufai..

Lasivyo utabambikiziwa mpunga na kuhisi umerogwa kumbe huna ujuzi...
 
ha ha ha,kila biashara sasa ni pasua kichwa,bora kulima mwenyewe tu
HII Point ila uwe na mtaji mzuri unaeza rudi kulekule kwenye hasara. kama
1.utakodi shamba
2.utakodi tractor
3.vibarua kupanda/kupalilia
4.vibarua kuvuna
.5.usafiri na kulipia store.
wakulima wanapata faida kozi nguvu kazi ni wao wenyewe
 
Wewe tupo pamoja kabisa uzoefu wangu kwa hiyo biashara n km unavyosema hapa
 
Uwezi uka utunza mchele mpaka hzo siku zifike
 
Mtaji ni sh ngap?
 
Mwaka jana nilifanya biashara hii kidogo nipoteze mtaji ila changamoto kadhaa nilizoziona ni kuwa 1. nilikuwa naagiza mtu anunue mie natuma pesa tu na aliponunua aliweka kwenye store ya interior ambapo bei kipindi cha kuuza haikupanda sana kutokana na location ya store ilipo ila walioweka store za mjini waliuza kwa bei ya juu kidogo, 2. changamoto nyingine niliyokuja kuiona ni aina ya ndoo aliyokuwa anatumia kupima kipindi anakusanya mpunga toka kwa wakulima alitumia ndoo za kawaida tu ndio maana pengine faida ikawa almost haipo zaidi ya kurudisha mtaji tu.

Kwa hiyo mwaka huu nimeamua kununua ndoo ya kibiashara ambayo niliipata kwa laki mbili, lakini pia nitafanya usimamizi wa karibu nimebadilisha msimamizi wa zoezi la ukusanyaji nami ntakuwa nafika site mara kwa mara kuona mwenendo wa makusanyo na pia store lazima niweke mjini ambako kuna wafanyabiashara wengi wanaohitaji mchele mda wa kukoboa ukifika.
 
Mkuu Morogoro mavuno yanaanza mwezi wangapi kama una taarifa .??
Na hiyo ndoo ya laki mbili ikoje.??
Na kingine bei za kuhifadhi zinakuwaje kwa gunia moja.?
 
Mkuu unafanyia wapi hyo biashara?
 
Mkuu Morogoro mavuno yanaanza mwezi wangapi kama una taarifa .??
Na hiyo ndoo ya laki mbili ikoje.??
Na kingine bei za kuhifadhi zinakuwaje kwa gunia moja.?
ndoo za laki mbili zipo na sio kwamba ni mpya hapana ni hizi za rangi za lita 20!ila huwa zinafanyiwa utundu wa kuzipanua,kuhusu bei za kuhifadhia mpunga store ni kati ya 300-4000 kwa msimu mmoja!na hukatwa wakati wa kukoboa kama utakoboa
 
Mdanganye,, siku hizi Wasukuma wanatumia ndoo zao kama hutaki tembea! Pia chunga sana siku hizi wanadaiwa kuonesha mashamba, ama sivyo unanyang'anywa mpunga wote! Hawa Usukumani wanaitwa "Bagalagaja"
 
Mdanganye,, siku hizi Wasukuma wanatumia ndoo zao kama hutaki tembea! Pia chunga sana siku hizi wanadaiwa kuonesha mashamba, ama sivyo unanyang'anywa mpunga wote! Hawa Usukumani wanaitwa "Bagalagaja"
Mambo ni moto, msimu huu lazima nikisanue kwenye mpunga, nalima mwenyewe, tena kando kando ya ziwa mvua ikizingua napiga irrigation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…