Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ndio imegunduliwa tu kwa hiyo bado hatujajua kama kweli itaelezea dark matter na dark energy au la. Lakini sisi sasa tuko kiti cha mbele kabisa katika sayansi kuona ni nini kinakuja. Very exciting.
Mkuu Kifyatu hii nguvu mpya ina faida gan kwenye maisha ya kawaida km inavyo Fahamika Kwa electromagnetic,nyukria fission na matumizi yao Ila hii nguvu mpya ukiachana na kuchunguza kuhusu ulimwengu inaweza kuwa na matumizi gan kwenye day to day life!!!?
 
Kifyatu unaamini ama uliwahi sikia kuna wanasayansi wa mambo yaanga walifanya uchunguzi wao na kuishia kusema KWELI MUNGU YUPO??
 
NYOTA ni kama jua lakini ziko mbali sana na dunia kushinda jua.NYOta ni kubwa kushinda jua.
Mkuu una uhakika na unachokiongea lkn?? Jua ni nyota ilio karibu na sayari yetu kulinganisha na nyota zingine zote
 
Swali gumu hili mkuu.

Hii nguvu kama ipo tayari inatuathiri kwa njia moja ua nyingine. Matumizi yake yatakuja baadae. Ni kama Magnetism ilivyogunduliwa hakuna aliejua kuwa itatumika kutengenezea motors, kuzalisha umeme, telecommunications (simu, TV, internet), x-rays, na taaluma zote zinategemea matumizi ya hii magnetism. Tusubiri tu mkuu. Ndio tumefungua tu mlango unaoingia katika nguvu hii mpya. Matumizi yake yatakuja tu. Pengine matumizi yake yasije katika uhai wetu lakini yatakuja.
 
Hili lina utata kdg lbd ni kutokana na upeo wng mdogo pengine ningeomba udadavuzi zaidi ktk hii hoja...sayari inawezaje kuwa na mwanga kiasi cha sisi huku tuliopo billions km away kuweza kuziona km nyota vile??
 
Kifyatu unaamini ama uliwahi sikia kuna wanasayansi wa mambo yaanga walifanya uchunguzi wao na kuishia kusema KWELI MUNGU YUPO??
Hapana!

Lakini najua kuwa wanasayansi, kama Higg, wamegundua (na kuthibitisha kuwepo kwa) Higgs Boson ambayo kazi yake ni kuumba (create) matter. Sasa tujuavyo katika dini ni kuwa muumba vitu vyote ni Mungu. Kama hii Higgs boson inaumba basi itakuwa na uhusiano na Mungu. Hii ndio sababu ya Higgs boson kuitwa God-particle.

Kwangu mimi ni uthibitisho wa kisayansi kuwa kuumba (creation) kunawezekana. Huu uumbaji unaweza usiwe kama unavyoelezwa kwenye vitabu vitakatifu (kama Bibilia au Qur'an) lakini ulitokea. Kama unataka kuuita huu uumbaji kuwa ni uthibitisho wa kisayansi wa kuwepo kwa Mungu, unaweza. Mimi sitaki kufika mbali kiasi hicho.
 
 
Hili lina utata kdg lbd ni kutokana na upeo wng mdogo pengine ningeomba udadavuzi zaidi ktk hii hoja...sayari inawezaje kuwa na mwanga kiasi cha sisi huku tuliopo billions km away kuweza kuziona km nyota vile??
Sasa hivi ikifika jioni wakati jua linazama ukiangalia magharibi utaona nyota inayowaka sana kabla ya nyota nyingine kutoka. Hii sio nyota bali ni sayari ya Venus. Na asubuhi kukipambazuka kuna nyota (ya mwisho kufifia) inayowaka sana mashariki, hii siyo nyota bali ni sayari ya Mercury.
 
Weak nuclear force ndiyo inayosababisha radioactive decay inayofanya nuclear material ku-deteriorate.
Strong nuclear force ndiyo inayozishikilia protons na neutrons pamoja katika kiini (nucleus) cha atoms.
 
Weak nuclear force ndiyo inayosababisha radioactive decay inayofanya nuclear material ku-deteriorate.
Strong nuclear force ndiyo inayozishikilia protons na neutrons pamoja katika kiini (nucleus) cha atoms.
mkuu nina swali kuhusu atoms kama kila kitu kimeundwa na atoms why kuna vyenye uhai na visivyokua na uhai mfano wanyama na mawe wakati vimeundwa na mkusanyiko wa atoms zilezile? au kuna atom zenye uhai na zisizo na uhai... swali la pili chembechembe za mwanga nazo ni atoms? kwanini zinatembea speed kubwa sana? samahani kama nitakua nimetoka nje ya mada
 
Mkuu Kifyatu naomba kutofautiana na wewe katika masuala mawili.
1. Uwepo wa Mungu
2. Spirituality.
Currently niko mobile, nipe masaa machache nikikaa nitaandika.
 
Mkuu Kifyatu mi naomba unifafanulie kidogo kuhusu ulimwengu ulivyo,maana tunaambiwa ulimwenguni kuwa hakuna juu wala chini,japo sisi tunaliangalia jua kwa juu,mwezi kwa juu na sayari zote na vikorokoro vyote tunaviangalia kwa juu hapo ndipo ninapotatizwa ufafanuzi tafadhari.
 
Swali ni kwanini jua linapoanza kuchomoza huwa halina mwanga mkali na jinsi linavyozidi ndio mwanga huwa mkali na pia likaanza kuishia huwa linaanza kupungua ule mwanga mkali????
 
Mkuu hata siku moja usiombe samahani kwa kuuliza swali. Hakuna swali la kijinga bali majibu ya kijinga.

Atom ndio sehemu ndongo inayotengeneza vitu (matter). Sasa hizi atoms zinaweza kujiweka katika mpangilio fulani na ukapata kitu tofauti kabisa. Kwa mfano, atom za carbon zikijipanga katika mfumo wa mabapa (flat structures) unapata graphite (yani penseli) ambayo ni laini sana lakini carbon atoms hizo hizo zikijipanga kama pyramids basi unapata almasi ambayo ni ngumu kuliko vitu vingine.

Sasa atom za aina moja zinaweza kuungana na za aina nyingine kutengeneza molecules zenye sifa tofauti. Kwa mfano, Nitrogen, Hydrogen na Oxygen zinaweza kuchanganyika na kutengeneza molecules zijulikanazo kama Amino Acids. Hizi amino acids ndizo molecule za kwanza kuwepo kabla uhai haujatokea. Hizi ndizo zinazojenga viumbe hai.

Kwa hiyo, katika kujibu swali lako, atoms hazina uhai bali atoms za elements tofauti vinaweza kujipanga na kutengeneza molecule zinazoweza kuanzisha uhai.

Mwanga (au photons) ni baadhi ya chembe chembe (sub-atomic particles) kama zilivyo bosons, neutrinos, electrons, n.k. Photons zina uzito karibu na sifuri na sub-atomic particles za aina hii (kama neutrinos) huwa zinasafiri kwa kasi kubwa. Sijui kwa nini zinafanya hivi bali hiyo ndiyo sifa yake.
 
Mkuu Kifyatu naomba kutofautiana na wewe katika masuala mawili.
1. Uwepo wa Mungu
2. Spirituality.
Currently niko mobile, nipe masaa machache nikikaa nitaandika.
Napenda sana watu wenye fikra tofauti na mimi. Hii ndio njia ninayotumia kujifunza. Nakusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…