Ufahamu kuhusu nyota za angani

Hakuna juu wala chini. Popote ulipo ule upande unaovutwa na gravity ya dunia ndio chini (kwa sababu vitu vinaanguka kuelekea chini) na ule upande mwengine ndio juu. Mfano, kama kuna watu wawili, mmoja yuko north pole na mwengine yuko south pole. Upande anaouita juu alieko north pole basi utakuwa ni chini kwa alie south pole.

Watu wanavutwa kuelekea katikati ya dunia. Kwa hiyo popote ulipo duniani upande unaoelekea katikati ya dunia ndio chini na ule mwengine ndio juu.
 
Swali ni kwanini jua linapoanza kuchomoza huwa halina mwanga mkali na jinsi linavyozidi ndio mwanga huwa mkali na pia likaanza kuishia huwa linaanza kupungua ule mwanga mkali????
Jua linapotoka au kuzama mionzi ya mwanga wake inagusa dunia katika angle ndogo (karibu na sifuri). Kadri siku inavyoendelea mpaka kufika mchana (saa sita, hasa kama uko karibu na equator) basi hii mionzi inatua ardhini katika angle ya 90 degrees. Sasa, nishati (energy) ya jua inayoangukia duniani inategemea hii angle (tuiite A).

Kwa mfano, kama jua linatoa nishati (tuiite) N kwa ujumla, basi nishati inayobakia ardhini ni N*Sin(A). (Sin(A) ni sine ya angle A.) [Kama hukufanya trigonometry utakuwa hujui sine ni nini. Cha muhimu ni kujua kuwa Sin(0) = 0 na Sin(90) = 1). ] Kwa hiyo asubuhi na jioni wakati hii angle ni karibu na sifuri, nishati ya jua inayotua duniani ni karibu na sifuri wakati mchana - saa sita, nishati yote toka kwenye jua tunaipata.
 
Napenda sana watu wenye fikra tofauti na mimi. Hii ndio njia ninayotumia kujifunza. Nakusubiri.
Asante mkuu, mimi pia napenda challenge na mawazo tofauti kutoka kwa mtu aliye open minded, kama wewe.
1. Uwepo wa Mungu: Sijajuwa tuzungumzie Mungu yupi hapa kwa sababu Miungu ni mingi. Lakini wacha tubase kwenye Mungu wa "wengi", Mungu anayezungumziwa kwenye maandiko ya dini kubwa mbili...yaani Biblia na Qur'an. Ukimsoma Mungu as potrayed in the Bible unapata kwamba sisi binadamu "ametuumba" kwa mfano wake, kwa maana alijiangalia akatuumba, isipokuwa alitunyima mambo ambayo ni makubwa akajibakizia yeye ili aendelee kuwa mkuu pekee. Kwa maana hiyo basi, he is NOT a particle, he is rather a guy, with supernatural powers. Kusema kwamba the "god" particle huenda ni dalili za Mungu ni irrelevant, utakuwa unajaribu kumtengeneza Mungu mwingine tofauti na yeye mwenyewe anavyojitanabahisha au anavyotanabahishwa na mitume yake kwenye vitabu "vyake". Ukisoma maandiko unaona kwamba mungu alikuwa anatokea dhahir mbele ya baadhi ya waja wake, au wakati mwingine kuongea nao kwa sauti tu....thats the God we need to confirm his existence, siyo particle. That God doesn't exist.

2. Spirituality: Umetafsiri neno hili kama hali ya kuwa na "imani" kwamba utafanikiwa. Sijajua kwa nini umetafsiri hivyo, maana kuna neno sahihi zaidi ambalo ni HOPE! Spirituality linatokana na neno "Spirit", ambalo kwa kiswahili linamaanisha Mzimu, as in Holy Spirit, Holy Ghost, yaani kwa kiswahili Mzimu Mtakatifu. Unaponunua ticket ya bahati nasibu una-HOPE kwamba utashinda, ukitaka kuingiza spirituality inamaana uombe mizimu (spirits of all sorts, holy and "unholy").

My take; Ukishakuwa Spiritual inamaana tayari una imani kwa some deity ndani yako, kwamba ukiomba hao/huyo deity anaweza kutenda miujiza. Kusema kwamba wewe ni Agnostic na Spiritual ni lugha laini tu inayotumika ili Atheists wasikushangae na Theists wasikushangae pia. Scientifically God doesn't exist, uzuri wa sayansi ni kwamba kukitokea mtu akaprove kwa credible evidence basi wanasayansi watampigia saluti na kukubali uwepo wa Mungu na goti watapiga ikibidi, na ubaya wa Spiritualism ni kwamba evidence ziko "moyoni" zaidi, yaani mtu hahitaji solid evidence za uwepo wa Mungu, badala yake anahitaji kitabu kimoja tu cha kale atachokisoma kwa msisimko mkubwa...na baada ya hapo hautaweza kumbadili mawazo hata kwa evidence.
Asante.
 
Subiri kwanza kwahio kama nna miaka ishirini ntarudi nyuma umri niwe mtoto mdogo kabisa?? Mifupa irudi ya kitoto??
 

Mkuu Kifyatu shukran sana, tuko pamoja .
 
Hapo nimekupata,lakini bado hujaniambia kama hata leo hii tukienda sayari ya Mars kwa mfano je, tukiwa kule nako tutaiangalia Dunia kwa juu kama leo hii tunavyoiangalia sayari ya Mars kwa juu ........???
 
Hapa hutapata upinzani toka kwangu. Kila dini inaamini kivyake. Dini tatu, yaani Ukristu, Uislamu na Judaism (Abrahamic religions) zinapaswa kuamini Mungu wa aina moja lakini ukiwasikiliza viongozi wa dini hizi wanavyovutia kwao unaweza kufikiri wanaabudu miungu tofauti.

Mimi ni agnostic kwa hiyo sitampinga mtu na imani yake. Nitawasikiliza waumini wa dini zote wakimtafsiri Mungu wao lakini sitatia neno. Imani ni kitu personal sana. Sio busara kumwambia mtu kuwa imani yake ni potofu.

Nadhani hatutofautiani hapa. Nimesema kuwa Spirituality ni yale matumaini....... Sasa matumaini ndio HOPE. Unapo-HOPE unamaanisha (intrinsically) kuwa kuna higher power itakayoingilia. Hii higher power inaweza kuwa Mungu, mizimu, maruhani, n.k. Cha muhimu hapa ni kuwa binaadam wote wanayo hii hali ya matumaini (HOPE), hasa wanapokuwa katika matatizo.


Ukiwa spiritual (hopeful) ina maana una imani kuwa kuna higher power (sio lazima awe mungu au deity). Hii ndiyo broader definition ya spirituality. Agnostics are searchers of knowledge. Please do not pigeon hole me into the other two categories.

Scientifically, creation happened (refer to Higgs boson story). Now if only God creates then Higgs boson must be a god-particle because it accomplishes what only God does.

You see, the question of whether or not GOD exists is not resolved by science. What science has done is to prove that some of the things that only God can do (like creation) can actually be explained scientifically. If you already believe in God (Theist) this will be an affirmation that "YOU SEE, WE TOLD YOU THERE IS GOD". If you don't believe in the existence of God (Atheist) then this scientific proof of creation further affirms to you that "YOU DO NOT NEED GOD TO CREATE".

Now probably you understand why I am Agnostic.
 
Subiri kwanza kwahio kama nna miaka ishirini ntarudi nyuma umri niwe mtoto mdogo kabisa?? Mifupa irudi ya kitoto??
Lakini kusafiri kwa kasi zaidi ya mwanga haitawezekana kamwe. Kwa hiyo hii nadharia haina maana kuijadili.
 
Hapo nimekupata,lakini bado hujaniambia kama hata leo hii tukienda sayari ya Mars kwa mfano je, tukiwa kule nako tutaiangalia Dunia kwa juu kama leo hii tunavyoiangalia sayari ya Mars kwa juu ........???
Ukiwa Mars basi muelekeo wa katikati ya Mars (center) ndio chini na upande mwengine ndio juu kama hapa duniani. Sasa wakati Mars ikitokea usiku (yaani tunaiona) basi itakuwa juu yetu wakati wa usiku na chini yetu wakati wa mchana. Hivyo hivyo ndivyo itakavyokuwa kama tuko Mars na tunaiangalia dunia yetu.
 

kuna swali huwa najiulizaga kuhusu hizi black holes kitako chake kipo wapi hasa (bottom yake inaishia wapi)
 
View attachment 425444kuna swali huwa najiulizaga kuhusu hizi black holes kitako chake kipo wapi hasa (bottom yake inaishia wapi)
Black hole ni center nyingine tu ya Gravity kama lilivyo jua letu au hata dunia yetu. Tofauti yake ni kuwa gravity ya blackholes ni kubwa sana hivyo humeza chochote kinachoikaribia, hata mwanga.
 
mkuu hizi neutrinos zina utofauti gani na photons?
 
Mkuu wa Egypt ya kale kwenye swala la astronomy na hesabu hawa jamaa walikuwa vizuri kuna baadhi hata ya formula za hesabu zina mizizi yake huko.
kwanini egypt ya sasa wasiweze kutengeneza mapyramid kama hayo? ninahisi hiyo kazi haikufanywa na watu wa kawaida
 
Photons ni light particles (chembe chembe za mwanga) na zina electric charge. Neutinos azina electric charge na hazihusiani na mwanga.
sasa mkuu ukiacha hizi kuna zile tatu tulizojifunza ndani ya atom(electon proton neutron) kuna uwezekano yeyote kati ya hizo kutoka au kuwa nje ya atom? ma ka zikiwa nje zinaweza kuleta madhara yeyote
 
sasa mkuu ukiacha hizi kuna zile tatu tulizojifunza ndani ya atom(electon proton neutron) kuna uwezekano yeyote kati ya hizo kutoka au kuwa nje ya atom? ma ka zikiwa nje zinaweza kuleta madhara yeyote
Protons na neutrons zinashikiliwa kwa nguvu kubwa sana (Strong Nuclear Force). Kuzitawanya unahitaji atom iliyo unstable kama za Uranium au plutonium. Hii ndio njia inayotumiwa kutengeneza mabomu ya nyuklia au mitambo ya umeme ya nyuklia.

Electrons, kwa upande mwengine, ni rahisi kuziyumbisha (au kuzipukusa) hasa zile zilizoko kwenye ulingo wa nje wa atom. Radi hufanya hivi kila inapopiga. Huondoa electrons chache kwenye atom (ya Nitrogen, Oxygen au hewa yeyote angani). Radi ikifanya hivi hii hewa inakuwa ionized na inaitwa plasma. Rejea mazungumzo yetu kuhusu plasma.
 
Photons ni light particles (chembe chembe za mwanga) na zina electric charge. Neutrinos azina electric charge na hazihusiani na mwanga.
Mkuu nilikuwa na google Leo lakini cha kushangaza naambiwa kutoka duniani mpk Venus ni mbali zaidi kuliko kutoka duniani mpk kwenye jua hii imekaaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…