Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Nashukuru kwa ufafanuzi wako ila kuna kitu kimoja nazani umekikosea nyota kubwa kwenye milky way Galaxy inaitwa VY majoris
 
Mkuu Kifyatu Bahari jion.
Nini kinasababisha atmosphere,chombo kinachotoka hapa Dunian kwenda deep space inabidi kiwe na speed ya scape gravity,je kikiwa kinarudi kinapoingia kwenye atmosphere yetu nini kinafanyika mpk kisiungue!!?
 
Escape Velocity
Samahani mkuu, mambo mengine hayaelezeki kirahisi bila ya hesabu. Nitazirahisisaha.

Ili chombo kiepuke gravity ya dunia (escape velocity) ni lazima nishati iliokuwa nayo kwa kasi yake (Kinetic Energy) iwe sawa au zaidi ya nishati inayokivuta kutokana na gravity (Potential Energy) hapo chombo kilipo. Hizi nishati mbili ni hizi:
Kinetic energy = 0.5*m*v*v
Potential energy = G*M*m/r

  • m=uzito wa chombo
  • M=uzito wa sayari (dunia)
  • v=kasi ya chombo (escape velocity)
  • r=umbali wa chombo kutoka center ya sayari (dunia)
  • G=Gravitational constant (haibadiliki kutoka sayari hadi sayari).
Kwa hiyo ili chombo kichoropoke gravity ya dunia:
Kinetic energy >= Potential energy au

0.5*m*v*v >= G*M*m/r au

Escape velocity v >= sqrt (2*G*M/r)

Kwa hiyo, escape velocity ya chombo chochote na mahali popote pale inategemea mambo mawili tu.
  1. Ukubwa (uzito) wa sayari (M) na
  2. Kiko umbali gani kutoka center ya hiyo sayari (r).

Chombo kurudi duniani.
Chombo kikirudi duniani wakati kinaingia kwenye atmosphere (hewa) lazima kitapata joto kali sana kwa sababu ya friction. Wataalam wanatumia vigae maalumu ili kuzuia kisiungue. Wasipofanya hivyo basi kitaungua kama kimondo.

Swali kwako: Ni Space Shuttle gani ya Kimarekani iliyoungua hivi?

Lakini kitu kingine cha kuangalia ni kuwa lazima hiki chombo kiingie duniani katika angle nzuri. Kikiingia katika angle ndogo basi kita-bounce na kutupwa kwenye giza la space. Hii ni kama ukitupa jiwe bapa majini (ziwa, bahari) huwa linagonga maji na kuruka-ruka. Sijui kama ulikwishawahi kufanya hii kitu?
 
Kifyatu
Space shuttle ambazo zimewahi kuungua ni 2,

Ya kwanza iliungua mwaka 1986 ambayo ilikuwa inaitwa challenger.ilianguka kwenye Bahari ya Atlantic na mabaki yake yakipatikana katika pwani ya cape Canaver,Florida.
Iliua jumla ya watu 7,katika hao 5 ni wanaanga na 2 ni wanasayansi!.

Hilo tukio likifanya kuzuiwa kwa shughuli za safari za anga kwa jumla ya miez 32 na rais wa kipindi icho wa marekan ndugu Ronard Reagan alitoa maagizo uchunguz wa ajali ufanyike ambao ulibain kulikuwa na mapungufu kwenye kusimamia taratibu za anga kwa maana controller wa huku ulimwenguni walikuwa wanafaham kuwa kuna baridi Kali ivyo haikuwa busara kuruhusu iyo shuttle kufanya kaz kwa muda ule.

Ajali nyingine ya space shuttle ilitokea feb 1mwaka 2003 ambayo ilikuwa inaitwa Colombia.pia hii ajali iliua jumla ya wanaanga 7. Tofaut hii iliungua wakati inaingia kwenye anga la dunia(atmosphere )

Baada ya janga hili space shuttle operations ilisimamishwa kwa muda wa miaka 2 na zaid na pia ujenz wa kituo cha wanaanga ukasimamishwa kwa muda.i lichukua miez 41 kila kitu kurudi Kama kilivyokuwa mwanzo.
 
1465143238651.jpg

Wana anga wa Colombia ambayo ilipata wakati mwaka 2013,

1465143299506.jpg

Hapo ni space shuttle ukiwa ina takeoff

1465143356187.jpg

Hapo ni space shuttle ilivyo kiutaalam
 
Space shuttle ambazo zimewahi kuungua ni 2,

Ya kwanza iliungua mwaka 1986 ambayo ilikuwa inaitwa challenger.ilianguka kwenye Bahari ya Atlantic na mabaki yake yakipatikana katika pwani ya cape Canaver,Florida.
Iliua jumla ya watu 7,katika hao 5 ni wanaanga na 2 ni wanasayansi!.
Hilo tukio likifanya kuzuiwa kwa shughuli za safari za anga kwa jumla ya miez 32 na rais wa kipindi icho wa marekan ndugu Ronard Reagan alitoa maagizo uchunguz wa ajali ufanyike ambao ulibain kulikuwa na mapungufu kwenye kusimamia taratibu za anga kwa maana controller wa huku ulimwenguni walikuwa wanafaham kuwa kuna baridi Kali ivyo haikuwa busara kuruhusu iyo shuttle kufanya kaz kwa muda ule.

Ajali nyingine ya space shuttle ilitokea feb 1mwaka 2003 ambayo ilikuwa inaitwa Colombia.pia hii ajali iliua jumla ya wanaanga 7.
Tofaut hii iliungua wakati inaingia kwenye anga la dunia(atmosphere )
Baada ya janga hili space shuttle operations ilisimamishwa kwa muda wa miaka 2 na zaid na pia ujenz wa kituo cha wanaanga ukasimamishwa kwa muda.i lichukua miez 41 kila kitu kurudi Kama kilivyokuwa mwanzo.
Excellent! A+.
Nilimaanisha hiyo ya pili ambayo iliungua wakati inaingia kutokana na hitlafu ya hivyo vigae.
 
Mkuu Kifyatu..planet Mars as inavyochukuliwa Kama red planet Sababu ya Atmosphere yake kuruhusu kuwa inapigwa na vimondo...na ndo plan b ya dunia kuhamia huko!,pia Kama ambavyo maisha Kule wanasema yanawezekana sababu kuna dalili za kuwepo kwa Bahari iliyoganda.
Watafanya nini kufix issue ya atmosphere na gravity.

Pia Mars wana jumla ya miez 4..Kama ambavyo tumeona huku kwetu mwezi una affect maji ya bahari itakuwaje kwenye mfumo wa maji Kule wakati wana jumla ya miez 4.
Ikiwa mwezi una reflect mwanga wa jua ndo tunapata majira ya mwez.je Kule Mars hakuna giza sababu mchana jua na usiku mwezi 4 inakuwa ina angaza??.
Swali la mwisho ukiwa Mars wakati wa mwanga kinakuwa na kivuli??
 
Ahsante mkuu Kifyatu...kupewa A+ na mtaalam Kama wew kunafanya na mm nijione Kama najua kumbe ni msaada wa watu wa Marekan kwenye Wikipedia..
Sote sisi tukimwaga nondo hapa ni kuwa tumejifunza mahala fulani. Usijirudishe nyuma mkuu.
 
Mkuu Kifyatu..planet Mars as inavyochukuliwa Kama red planet Sababu ya Atmosphere yake kuruhusu kuwa inapigwa na vimondo...na ndo plan b ya dunia kuhamia huko!,pia Kama ambavyo maisha Kule wanasema yanawezekana sababu kuna dalili za kuwepo kwa Bahari iliyoganda.
Watafanya nini kufix issue ya atmosphere na gravity.

Rangi nyekundu ya Mars ni shauri ya rangi ya udongo wake kama hapa duniani (red coffee soil) kwenye sehemu fulani.

Kufix atmosphere ndio mpango kamili (kuongeza hewa ya Oxygen). Huu ni mpango wa muda mrefu kwa kupanda miti. Katika kipind cha muda mfupi watategemea kutengeneza Oxygen yao kutokana na maji yaliyopo. Maana kubeba mitungi ya hewa kila uendapo.

Kuhusu gravity hii itabidi miili ya wakazi wa huko izoee tu gravity ndogo.

Pia Mars wana jumla ya miez 4..Kama ambavyo tumeona huku kwetu mwezi una affect maji ya bahari itakuwaje kwenye mfumo wa maji Kule wakati wana jumla ya miez 4.
Ikiwa mwezi una reflect mwanga wa jua ndo tunapata majira ya mwez.je Kule Mars hakuna giza sababu mchana jua na usiku mwezi 4 inakuwa ina angaza??.
Miezi ya Mars haitaathiri maisha. Unafikiri kama kila usiku wetu tungekuwa na mbalamwezi tungechukia?

Swali la mwisho ukiwa Mars wakati wa mwanga kinakuwa na kivuli??

Ukiwa chini ya mwamba au pango kutakuwa na kivuli.
 
Samahani braza hivi Luna simple formula ya kuweza kupredict kupatwa kwa jua, nataka nijaribu kufanya kuangalia accuracy yake maana mwezi wa 9 mikoa ya kusini hasa mkoa wa mbeya kutakuwa na total solar eclipse hivyo nataka nijaribu.
 
Mkuu Kifyatu tueleze kuhusu kifaa kilichopo Jupiter.
Nini wanategemea kupata kwa muda huo ambapo kitakuwa huko!.
Jupiter yenyewe Kama wana vyoeleza ni kuwa ni gas planet
Ina helium na hydrogen same as jua .sa mbona yenyewe It doesn't burn Kama jua??
 
Lakini pia kifyatu au Neo1 kwa nini siku zote tumekuwa tukiliona hili wingu la blue na halina ukomo wala kubadilika? Nini chanzo cha hili wingu la blue tunaloliona kwa macho kama vile limeifunika dunia?
 
Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC2. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, nyekundu na bluu. Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawasilisha.

I am sorry if this is an overkill.
asante mkuu, kuna jamaa hapo juu alicomment kwa kifupi jamaa akamkosoa ila nashukuru umeeleza kitaalam zaidi, ubarikiwe!
 
Back
Top Bottom