Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mkuu Kifyatu unamaanisha nin unaposema tumeumbwa kwa carbon???
Binadamu na wanyama hupata lishe yao kubwa kutokana na mimea. Mimea hutumia Carbon dioxide kwa wingi sana kutengeneza chakula chao. Sisi binaadamu, zaidi ya Oxygen, Carbon ndio madini nyingine iliyoko kwa wingi mwilini mwetu. Angalia chati hapo chini.

Siku hizi kuna watu mataajiri wakifa huchoma miili yao na ile carbon inayobakia (majivu) inatiwa kwenye mashine zenye presha na joto kubwa kama ilivyo ndani ya ardhi yetu na kutengeneza almasi (synthetic diamond) badala ya kuwa na kaburi au majivu.

(Hiyo Oxygen - 65% na Hydrogen - 10%, ni sehemu ya maji yaliyomo mwilini mwetu)

500px-201_Elements_of_the_Human_Body-01.jpg

Source: Composition of the human body - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Napoangaliaga angani wakati wa usiku huwa naona nyota zingine ambazo hazina mwanga wa rangi moja,yan inabadilika badilika mara nyekundu,kijan,bluu.
Je hizi nyota ni za aina gani? mana kuna mtu katika stori za utoto alinambia eti zile ni satelaiti
Pia nyota chanzo chake cha mwanga ni kipi?
Karibuni wadau wa Sayansi ya anga
unaniua wewe....umeeleza vzr sn[emoji122] [emoji122]
 
Binadamu na wanyama hupata lishe yao kubwa kutokana na mimea. Mimea hutumia Carbon dioxide kwa wingi sana kutengeneza chakula chao. Sisi binaadamu, zaidi ya Oxygen, Carbon ndio madini nyingine iliyoko kwa wingi mwilini mwetu. Angalia chati hapo chini.

Siku hizi kuna watu mataajiri wakifa huchoma miili yao na ile carbon inayobakia (majivu) inatiwa kwenye mashine zenye presha na joto kubwa kama ilivyo ndani ya ardhi yetu na kutengeneza almasi (synthetic diamond) badala ya kuwa na kaburi au majivu.

(Hiyo Oxygen - 65% na Hydrogen - 10%, ni sehemu ya maji yaliyomo mwilini mwetu)

500px-201_Elements_of_the_Human_Body-01.jpg

Source: Composition of the human body - Wikipedia, the free encyclopedia
hivi mkuu nyota kama VY ambayo ipo ndani ya milkway ikilipuka na kuwa blackhole itatengeneza galaxy yake? au kuna blackholes ambazo hazipo katikati ya galaxy
 
Yes, kuna blackhole nyingi tu ambazo hazina galaxies zake zenyewe.

Nyota iliyopo tayari kwenye galaxy, hata kama ni kubwa kiasi gani, ikilipuka (super nova) na kuwa blackhole au neutron star, bado itabaki katika mzunguuko wa ile super-massive blackhole ya galaxy yake. Inaweza kumeza vijinyota vingine vya karibu yake lakini sio kutengeneza galazi yake yenyewe.
 
JE DARK MATTER IMEGUNDULIWA?

Mkuu neo1 niliahidi kuwa badala ya kujibu maswali tu, from time to time nitaleta taarifa muhimu zinazohusu huu uzi.

Unakumbuka tulizungumzia kuhusu DARK MATTER na DARK ENERGY hapa? Well, kwa muda mrefu tu wanasayasi wa CERN (Uswiss) walikiua wanachunguza uwepo wa hii dark matter lakini ilikuwa inawapa shida kuipata. Sasa mwaka jana (July 2015) hawa wanasayansi wanahisi wamegundua kitu kilichokuwa kinaificha hii dark matter. Wamegundua kuwa kuna nguvu nyingine ya tano (5th force of nature) ambayo inaweza kutufanya tuione au kuielewa hii dark matter.

Mpaka sasa wanasayansi walikuwa wanajua nguvu 4 tu za nature nazo ni:
  1. Gravitation
  2. Electromagnetism
  3. Strong Nuclear Force
  4. Weak Nuclear Force
Sasa wamegundua chembe chembe au sub-atomic particle (boson, wanaiita X-Boson) mpya kabisa yenye nguvu tofauti na hizo 4 hapo juu. Hii nguvu mpya wanaiita 5th Force of Nature ambayo inawaza kuelezea vizuri zaidi dark matter.

Ni mapema kujua kama imethibitishwa lakini kama ni kweli, this is a big deal wandugu. Itabidi vitabu vya physics viandikwe upya. Kama uko sekondari usijali, vitabu vyako bado vinafaa.

Naambatanisha links mbili hapa chini zinazoelezea huu ugunduzi kwa kina zaidi.

Samahani kama kuna mtu ambae hii mada haina maana kwake.

5th force of nature possibly discovered, US physicists say
CERN’s LHCb experiment reports observation of exotic pentaquark particles | Media and Press Relations
 
duh kwahiyo hiyo nguvu mpya x boson itakua ndiyo dark matter yenyewe
 
Hapana, lakini itafanya tuelewe vizuri matter ni nini na kwa nini matter nyingine haionekani, yaani dark matter.
1477159782150.jpg
mkuu naomba unieleweshe kidogo hapa kwenye kukua kwa universe dark energy inahusika vipi? na ile nguvu ya big bang bado ipo?
 
View attachment 422537mkuu naomba unieleweshe kidogo hapa kwenye kukua kwa universe dark energy inahusika vipi? na ile nguvu ya big bang bado ipo?
Ngoja nikuchukue taratibu katika haya maelezo ili unielewe vizuri. Niwie radhi kwa urefu wa jibu:

Big Bang:
Baada ya big bang, mikusanyiko mikubwa ya hydrogen ilizagaa sehemu mbalimbali. Katika kila mkusanyiko wa hydrogen gravity ilikuwa kubwa sana na kulipuka kutengeneza supper-massive blackholes ambazo zikawa centers za galaxies tunazoziona. (Wanasayansi sasa wanaamini kuwa galaxies ziliundwa pamoja na blackholes zake wakati wa big bang.) Nafasi kati ya galaxy mbili zilizopo karibu karibu kukawa na utupu au space.

Mtanuko wa Space na Hubble's Constant:
Wanasayansi wameona kuwa hizi galaxies zinakimbiana, na zile zilizoko mbali zinakimbia kwa kasi kubwa zaidi kuliko zilizopo karibu karibu. Ukweli ni kuwa hizi galaxies hazitembei isipokuwa space kati ya galaxies ndiyo inayotanuka at a constant rate (kasi). Hii kasi ya mtanuko ndio inayojulikana kama Hubble's Constant.

Mfano - Kama space kati ya galaxy mbili ni km 5 na Hubble constant (ya matanuzi) ni 2 kwa siku, basi ina maana kesho hiyo space itakuwa km 10 (yaani mara mbili ya km 5), lakini kesho kutwa hiyo space itakuwa km 20 (yaani mara mbili ya km 10), siku inayofuata itakuwa km 40, km 80, n.k.

Hiki ndicho kinachotufanya tuone kana kwamba galaxies za mbali zinapwaga kwa kasi kubwa sana kuliko za karibu. Narudia tena, galaxies hazitembei bali space kati yao ndiyo inayotanuka.

Dark Energy:
Sasa hapa ndio swala la dark energy linapokuja. Ni kitu gani kinacho fanya hii space itanuke kwa kasi kubwa namna hiyo? Wanasayansi wameona kuwa haiwezikani iwe ile nguvu ya mlipuko wa big bang. Ni lazima kuwe na nishati nyingine tusiyoiona inayosababisha huu mtanuko. Hii nishati tusiyoiona ndio inayoitwa Dark Energy.

Huu uvumbuzi wa juzi juzi wa CERN (rejea mada niliyoleta hivi karibuni) wa hii X-Boson na 5th force of nature, kama ni kweli, inaweza kuelezea vizuri sana hii dark energy na huu mtanuko wa universe yetu.

Natumaini sikukuchosha sana.
 
Kwa sasa sipo Tanzania lakini unaweza kuzipata kwenye internet. Telescope nzuri zinaanzia kama Tsh laki moja hivi. Lakini ukishop around kutoka China au India unaweza kupata bei nzuri.
Mkuu Kifyatu kwanza nikupe pongezi kwa elimu unayotupatia kwani imetusaidia wengi tumepata uelewa mkubwa kwa mambo ya anga na ulimwengu kwa ujumla.

Swali langu mkuu (niwie radhi kama nitakukera) ni kuwa pamoja na wewe kukiri si muumini wa dini yoyote ni kwa nini wanasayansi wengi hawaamini wala kukubali uwepo wa MUNGU.?
 
Swali zuri sana mkuu na wala usiombe radhi. Niko tayari kukuingiza ndani ya ulimwengu wa Kifyatu. Nami nakuomba radhi kwa jibu refu.

Kuna makundi ya aina tatu ya watu:
  1. Wanaoamini uwepo wa Mungu - Theists
  2. Wasioamini uwepo wa Mungu - Atheists
  3. Wasiojua na wanatafuta ukweli uko wapi - Agnostics
Wana sayansi wengi wapo kwenye hili kundi la tatu - Agnostics. Mimi ni agnostic mmojawapo.

Universe:
Unajua, ukiangalia ukubwa wa, na complexity ya, huu uimwengu wetu bado huwezi kuuelezea, hata kwa kutumia sayansi, kuwa ulianzaje. Kulikuwa na nini kabla ya big bang? Je hii Higgs boson (wanaiita God particle) ni ishara ya kisayansi ya uwepo wa Mungu? Unaona. Kuna maswali mengi sana ambayo sayansi bado haiwezi kuyajibu. Kwa hiyo mwanasayansi yeyote yule anaesema yeye ana uhakika Mungu hayupo basi huyo ninamtilia mashaka na hiyo elimu yake.

Dini:
Mimi naziona dini kama vyama vile. Kila moja inavutia upande wake na kujigamba kuwa wao wanamuelewa Mungu kiundani kuliko wengine na kutoa masharti chungu tele ya kuwa muumini. Mimi nimeamua kutoyumbishwa na hizi dini mbalimbali na maelezo yao. Sasa ukiangalia composition ya dini unakuta ina sehemu mbili.

Dini = Spirituality (matumaini au hope au "ucha mungu") + Culture (mila na desturi)

Spirituality ni ile hali ya kuwa na matumaini kuwa utafanikiwa. Hata watu wasio na dini lakini wakiwa katika matatizo watategemea kuwa miujiza (mizimu, lady luck, n.k.) itatokea wasalimike. Watu hawa pia watanunua tiketi za bahati-nasibu wakitegemea watakuwa na bahati siku hiyo ya kushinda. Hii hali ya matumaini kuwa kuna kitu kitaiingilia kutatua matatizo yako ndio SPIRITUALITY.

Kwa wale wenye dini basi hii spirituality wanailinganisha na uwepo wa Mungu mwenye uwezo wote. Binadamu wote wanayo hii spirituality (awe na dini au sio). Ndio njia kuu ya sisi binaadamu tunayotumia kupambana na matatizo ya maisha kisaikolojia (coping mechanism).

Culture au mila/desturi ndiyo inayotengeneza dini.
  • Uislam = Spirituality + mila za kiarabu
  • Ukristo = Spirituality + mila za kizungu/kiyahudi
  • Judaism = Spirituality + mila za kiyahudi
  • Na kadhalika.
Kwa hiyo ukiondoa mila/desturi katika hizi dini basi dini zote zitafanana. Jaribu kufikiria.

Kwa mfano, kama wewe ni mwarabu basi mila/desturi za kabila lako ndio hizo hizo mila/desturi za dini yako. Ikiwa hivyo basi dini kwako ndio mwenendo wa maisha (a way of life) na hujilazimishi. Kwa wengine wote inabidi tujilazimishe tu (kuvaa hijab, kuswali ukielekea Makkah kwa kiarabu, kutokula nguruwe, n.k.) ili tuwe waislam.

Mara nyingi ufuasi wa dini unategemea ulivyokuzwa. Hata wanasayansi, kama wamekuwa katika familia zenye misimamo mikali wa kidini wataamini uwepo wa Mungu kufuatilia imani walizokuzwa nazo.

Mimi:
Hivyo basi mimi katika maisha yangu ni Spiritual lakini sio Religious. Hiki ndicho nilichomaanisha niliposema "sina dini".

Natumaini umenielewa.
 
Ngoja nikuchukue taratibu katika haya maelezo ili unielewe vizuri. Niwie radhi kwa urefu wa jibu:

Big Bang:
Baada ya big bang, mikusanyiko mikubwa ya hydrogen ilizagaa sehemu mbalimbali. Katika kila mkusanyiko wa hydrogen gravity ilikuwa kubwa sana na kulipuka kutengeneza supper-massive blackholes ambazo zikawa centers za galaxies tunazoziona. (Wanasayansi sasa wanaamini kuwa galaxies ziliundwa pamoja na blackholes zake wakati wa big bang.) Nafasi kati ya galaxy mbili zilizopo karibu karibu kukawa na utupu au space.

Mtanuko wa Space na Hubble's Constant:
Wanasayansi wameona kuwa hizi galaxies zinakimbiana, na zile zilizoko mbali zinakimbia kwa kasi kubwa zaidi kuliko zilizopo karibu karibu. Ukweli ni kuwa hizi galaxies hazitembei isipokuwa space kati ya galaxies ndiyo inayotanuka at a constant rate (kasi). Hii kasi ya mtanuko ndio inayojulikana kama Hubble's Constant.

Mfano - Kama space kati ya galaxy mbili ni km 5 na Hubble constant (ya matanuzi) ni 2 kwa siku, basi ina maana kesho hiyo space itakuwa km 10 (yaani mara mbili ya km 5), lakini kesho kutwa hiyo space itakuwa km 20 (yaani mara mbili ya km 10), siku inayofuata itakuwa km 40, km 80, n.k.

Hiki ndicho kinachotufanya tuone kana kwamba galaxies za mbali zinapwaga kwa kasi kubwa sana kuliko za karibu. Narudia tena, galaxies hazitembei bali space kati yao ndiyo inayotanuka.

Dark Energy:
Sasa hapa ndio swala la dark energy linapokuja. Ni kitu gani kinacho fanya hii space itanuke kwa kasi kubwa namna hiyo? Wanasayansi wameona kuwa haiwezikani iwe ile nguvu ya mlipuko wa big bang. Ni lazima kuwe na nishati nyingine tusiyoiona inayosababisha huu mtanuko. Hii nishati tusiyoiona ndio inayoitwa Dark Energy.

Huu uvumbuzi wa juzi juzi wa CERN (rejea mada niliyoleta hivi karibuni) wa hii X-Boson na 5th force of nature, kama ni kweli, inaweza kuelezea vizuri sana hii dark energy na huu mtanuko wa universe yetu.

Natumaini sikukuchosha sana.
Kwanza congrats nyingo kwa kuliendeleza hili somo mkuu, swali langu ni dogo tu kwamba kama galaxies hazitanuki bali space ndio inayotanuka, wataka kusema kwamba hiyo space inakuwa tupu bila kitu chochote katikati yake? Na kama hiyo dark energy ndiyo inayosababisha huo mtanuko hiyo dark energy source yake ni nini?
Sorry kama nitakuwa nimekurudisha nyuma kidogo
 
Swali zuri sana mkuu na wala usiombe radhi. Niko tayari kukuingiza ndani ya ulimwengu wa Kifyatu. Nami nakuomba radhi kwa jibu refu.

Kuna makundi ya aina tatu ya watu:
  1. Wanaoamini uwepo wa Mungu - Theists
  2. Wasioamini uwepo wa Mungu - Atheists
  3. Wasiojua na wanatafuta ukweli uko wapi - Agnostics
Wana sayansi wengi wapo kwenye hili kundi la tatu - Agnostics. Mimi ni agnostic mmojawapo.

Universe:
Unajua, ukiangalia ukubwa wa, na complexity ya, huu uimwengu wetu bado huwezi kuuelezea, hata kwa kutumia sayansi, kuwa ulianzaje. Kulikuwa na nini kabla ya big bang? Je hii Higgs boson (wanaiita God particle) ni ishara ya kisayansi ya uwepo wa Mungu? Unaona. Kuna maswali mengi sana ambayo sayansi bado haiwezi kuyajibu. Kwa hiyo mwanasayansi yeyote yule anaesema yeye ana uhakika Mungu hayupo basi huyo ninamtilia mashaka na hiyo elimu yake.

Dini:
Mimi naziona dini kama vyama vile. Kila moja inavutia upande wake na kujigamba kuwa wao wanamuelewa Mungu kiundani kuliko wengine na kutoa masharti chungu tele ya kuwa muumini. Mimi nimeamua kutoyumbishwa na hizi dini mbalimbali na maelezo yao. Sasa ukiangalia composition ya dini unakuta ina sehemu mbili.

Dini = Spirituality (matumaini au hope au "ucha mungu") + Culture (mila na desturi)

Spirituality ni ile hali ya kuwa na matumaini kuwa utafanikiwa. Hata watu wasio na dini lakini wakiwa katika matatizo watategemea kuwa miujiza (mizimu, lady luck, n.k.) itatokea wasalimike. Watu hawa pia watanunua tiketi za bahati-nasibu wakitegemea watakuwa na bahati siku hiyo ya kushinda. Hii hali ya matumaini kuwa kuna kitu kitaiingilia kutatua matatizo yako ndio SPIRITUALITY.

Kwa wale wenye dini basi hii spirituality wanailinganisha na uwepo wa Mungu mwenye uwezo wote. Binadamu wote wanayo hii spirituality (awe na dini au sio). Ndio njia kuu ya sisi binaadamu tunayotumia kupambana na matatizo ya maisha kisaikolojia (coping mechanism).

Culture au mila/desturi ndiyo zinayotengeneza dini.
  • Uislam = Spirituality + mila za kiarabu
  • Ukristo = Spirituality + mila za kizungu/kiyahudi
  • Judaism = Spirituality + mila za kiyahudi
  • Na kadhalika.
Kwa hiyo ukiondoa mila/desturi katika hizi dini basi dini zote zitafanana. Jaribu kufikiria.

Kwa mfano, kama wewe ni mwarabu basi mila/desturi za kabila lako ndio hizo hizo mila/desturi za dini yako. Ikiwa hivyo basi dini kwako ndio mwenendo wa maisha (a way of life) na hujilazimishi. Kwa wengine wote inabidi tujilazimishe tu (kuvaa hijab, kuswali ukielekea Makkah kwa kiarabu, kutokula nguruwe, n.k.) ili tuwe waislam.

Mara nyingi ufuasi wa dini unategemea ulivyokuzwa. Hata wanasayansi, kama wamekuwa katika familia zenye misimamo mikali wa kidini wataamini uwepo wa Mungu kufuatilia imani walizokuzwa nazo.

Mimi:
Hivyo basi mimi katika maisha yangu ni Spiritual lakini sio Religious. Hiki ndicho nilichomaanisha niliposema "sina dini".

Natumaini umenielewa.
Mkuu Kifyatu we ni zaidi ya mwalimu, nimekuelewa vyema kiongozi...
 
Kwanza congrats nyingo kwa kuliendeleza hili somo mkuu, swali langu ni dogo tu kwamba kama galaxies hazitanuki bali space ndio inayotanuka, wataka kusema kwamba hiyo space inakuwa tupu bila kitu chochote katikati yake? Na kama hiyo dark energy ndiyo inayosababisha huo mtanuko hiyo dark energy source yake ni nini?
Sorry kama nitakuwa nimekurudisha nyuma kidogo
Mkuu fyddell nakumbuka tulianza pamoja katika hii mada zaidi ya miaka miwili iliyopita. Habari za siku?

Nikijibu swali lako:
Space kati ya galaxies ni tupu au ni ombwe (vacuum).

Dark energy inahisiwa kuwepo hapa ulimwenguni kwa kutokana na vitu inavyofanya, kama kutanua space, lakini mpaka sasa ilikuwa haijulikani inatoka wapi. Huu ugunduzi wa juzi juzi wa X-boson na hii nguvu ya tano ya nature (zaidi ya Gravity, Magnetism, Strong-nuclear, na Weak-nuclear) huko Uswiss (CERN) umeni-excite sana. Kwa mara ya kwanza tutaweza kuijua dark matter (compliments to X-boson) na dark energy (compliments to hii nguvu mpya ya tano ya nature). Soma kuhusu 5th Force of Nature au Discovery of X-boson.

Kwa hiyo mkuu sisi tukae mkao wa kula (tahyatu) tu kusubiri wanasayansi watupakulie uhondo. Hiki ni kipindi cha furaha sana katika sayansi. Bahati mbaya sio kila mtu anajua kwamba pengine neema kubwa sana inakuja katika sayansi.

Tusubiri tu mkuu lakini nadhani katika uhai wetu wewe na mimi tutashuhudia makubwa sana kuliko vizazi vilivyopita.
 
Ni kweli mkuu tulianza pamoja hii mada kitambo kweli ila majukumu na kutafuta knowledge mpya katika nchi ya watu huko kulinifanya niwe adimu kiasi. Nitapitia huu ugunduzi mpya wa hiyo nguvu ya tano ya nature na hii issue ya X- Boson muda si mrefu then nitarudi. Nikushukuru sana mkuu kwa kuendelea kutoa somo hili adhimu ili wengi wafaidike
 
Swali zuri sana mkuu na wala usiombe radhi. Niko tayari kukuingiza ndani ya ulimwengu wa Kifyatu. Nami nakuomba radhi kwa jibu refu.

Kuna makundi ya aina tatu ya watu:
  1. Wanaoamini uwepo wa Mungu - Theists
  2. Wasioamini uwepo wa Mungu - Atheists
  3. Wasiojua na wanatafuta ukweli uko wapi - Agnostics
Wana sayansi wengi wapo kwenye hili kundi la tatu - Agnostics. Mimi ni agnostic mmojawapo.

Universe:
Unajua, ukiangalia ukubwa wa, na complexity ya, huu uimwengu wetu bado huwezi kuuelezea, hata kwa kutumia sayansi, kuwa ulianzaje. Kulikuwa na nini kabla ya big bang? Je hii Higgs boson (wanaiita God particle) ni ishara ya kisayansi ya uwepo wa Mungu? Unaona. Kuna maswali mengi sana ambayo sayansi bado haiwezi kuyajibu. Kwa hiyo mwanasayansi yeyote yule anaesema yeye ana uhakika Mungu hayupo basi huyo ninamtilia mashaka na hiyo elimu yake.

Dini:
Mimi naziona dini kama vyama vile. Kila moja inavutia upande wake na kujigamba kuwa wao wanamuelewa Mungu kiundani kuliko wengine na kutoa masharti chungu tele ya kuwa muumini. Mimi nimeamua kutoyumbishwa na hizi dini mbalimbali na maelezo yao. Sasa ukiangalia composition ya dini unakuta ina sehemu mbili.

Dini = Spirituality (matumaini au hope au "ucha mungu") + Culture (mila na desturi)

Spirituality ni ile hali ya kuwa na matumaini kuwa utafanikiwa. Hata watu wasio na dini lakini wakiwa katika matatizo watategemea kuwa miujiza (mizimu, lady luck, n.k.) itatokea wasalimike. Watu hawa pia watanunua tiketi za bahati-nasibu wakitegemea watakuwa na bahati siku hiyo ya kushinda. Hii hali ya matumaini kuwa kuna kitu kitaiingilia kutatua matatizo yako ndio SPIRITUALITY.

Kwa wale wenye dini basi hii spirituality wanailinganisha na uwepo wa Mungu mwenye uwezo wote. Binadamu wote wanayo hii spirituality (awe na dini au sio). Ndio njia kuu ya sisi binaadamu tunayotumia kupambana na matatizo ya maisha kisaikolojia (coping mechanism).

Culture au mila/desturi ndiyo inayotengeneza dini.
  • Uislam = Spirituality + mila za kiarabu
  • Ukristo = Spirituality + mila za kizungu/kiyahudi
  • Judaism = Spirituality + mila za kiyahudi
  • Na kadhalika.
Kwa hiyo ukiondoa mila/desturi katika hizi dini basi dini zote zitafanana. Jaribu kufikiria.

Kwa mfano, kama wewe ni mwarabu basi mila/desturi za kabila lako ndio hizo hizo mila/desturi za dini yako. Ikiwa hivyo basi dini kwako ndio mwenendo wa maisha (a way of life) na hujilazimishi. Kwa wengine wote inabidi tujilazimishe tu (kuvaa hijab, kuswali ukielekea Makkah kwa kiarabu, kutokula nguruwe, n.k.) ili tuwe waislam.

Mara nyingi ufuasi wa dini unategemea ulivyokuzwa. Hata wanasayansi, kama wamekuwa katika familia zenye misimamo mikali wa kidini wataamini uwepo wa Mungu kufuatilia imani walizokuzwa nazo.

Mimi:
Hivyo basi mimi katika maisha yangu ni Spiritual lakini sio Religious. Hiki ndicho nilichomaanisha niliposema "sina dini".

Natumaini umenielewa.
Aisee haya mambo yanachanganya japokuwa ni matamu. ngoja tuwasikilizie hao scientist
Mkuu fyddell nakumbuka tulianza pamoja katika hii mada zaidi ya miaka miwili iliyopita. Habari za siku?

Nikijibu swali lako:
Space kati ya galaxies ni tupu au ni ombwe (vacuum).

Dark energy inahisiwa kuwepo hapa ulimwenguni kwa kutokana na vitu inavyofanya, kama kutanua space, lakini mpaka sasa ilikuwa haijulikani inatoka wapi. Huu ugunduzi wa juzi juzi wa X-boson na hii nguvu ya tano ya nature (zaidi ya Gravity, Magnetism, Strong-nuclear, na Weak-nuclear) huko Uswiss (CERN) umeni-excite sana. Kwa mara ya kwanza tutaweza kuijua dark matter (compliments to X-boson) na dark energy (compliments to hii nguvu mpya ya tano ya nature). Soma kuhusu 5th Force of Nature au Discovery of X-boson.

Kwa hiyo mkuu sisi tukae mkao wa kula (tahyatu) tu kusubiri wanasayansi watupakulie uhondo. Hiki ni kipindi cha furaha sana katika sayansi. Bahati mbaya sio kila mtu anajua kwamba pengine neema kubwa sana inakuja katika sayansi.

Tusubiri tu mkuu lakini nadhani katika uhai wetu wewe na mimi tutashuhudia makubwa sana kuliko vizazi vilivyopita.
 
Kwasasa ni ngumu kiasi kuconclude kuhusiana na hii nguvu ya tano ya nature coz wanasayansi wengi bado hawajaifahamu vizuri kutokana na level ya technology tunayotumia ila miaka si mingi (punde) itajulikana.
Ningependa sana kujua faida ya hii nguvu ya tano kwa sayari yetu na maisha ya viumbe kiujumla.
 
Ndio imegunduliwa tu kwa hiyo bado hatujajua kama kweli itaelezea dark matter na dark energy au la. Lakini sisi sasa tuko kiti cha mbele kabisa katika sayansi kuona ni nini kinakuja. Very exciting.
 
Back
Top Bottom