bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
Unajua kwamba watu wengi wenye upeo wa chini wa ufahamu, husikiliza ili kujibu na hutazama ili kusimulia. Tofauti na watu wenye upeo wa juu ambao wao husikiliza ili kutafakari na hutazama ili kuona. Wapumbavu hudhani kutazama inawasaidia kufahamu kwa kuwa maisha yao yanaendeshwa na hisia za miguu badala ya ufahamu wa akili. Na hii ndiyo maana hata kula kwao ni sababu ya kujaza utumbo mpana ili kushindana na tembo kunya mavi manene.
Huwezi kuweka mpango wa kula kabla hujaumwa njaa halafu uwe na akili timamu. Yaani unaamka ukiwa umepanga utakula saa tatu, saa saba na saa mbili usiku. Upo hapa duniani kula, akili inawaza kula ndiyo maana safari za chooni zinakuwa nyingi kuliko za maktaba. Haya tazana huyu mwingine anasema natumia lugha ngumu lakini haoni ugumu wa dona linalomkosesha usingizi mzuri usiku. Hilo ni tatizo la kusikiliza ili kujibu badala ya tafakari. Mdomo ukiwa mkubwa kuliko ubongo ni vigumu sana kujipa muda kabla ya kupayuka maana kila kitu unakipa tafsiri inayokupa ruhusa ya kushambulia.
Ukikua utagundua kwamba kichwa ni chumba cha ufahamu na siyo shamba la kufugia nywele. Utagundua kwamba ulifanya vita na watu waliokutakia amani huku ukitumia nguvu kupambana na wanaokupenda. Lakini kukua siyo kutuna mashavu au kuwa na miguu mirefu kama vibupuru vya shamba la mpunga, bali ni kuuona ufahamu wako ukibadilika na kuenda sambamba na midundo ya ulimwengu.
Nisikuchoshe maana huenda unachelewa kwenda kula pweza na kachori kwa mpemba. Ulichookota chukua, ulichokosa siyo chako. Dunia hii si ya watu laini na wavivu wa kufikiri.