Huyu binti anatwa Rina Palenkova na hii ni picha ya mwisho kuipandisha mtandaoni ikiambana na maneno Nyapoka. Nya inaaminisha Nyau ule mlio wa paka kwa Kijapani na Poka inamanisha kwaheri kwa Kirusi. Hii ilikuwa ni picha ya mwisho kabla ya kesho Rina kujirusha mbele ya train na kuuawa.
Kifo cha Rina hakikuwa kifo cha kawaida cha binti mwenye umri miaka 17 kuamua tu kujiua, bali ilikuja kugundulika kwamba ni mchezo wa mtandaoni unaujulikana kama Blue Whale. Rina alikuwa mhanga ambaye huko kwenye kikundi chao alipewa nambari moja.
Taarifa za kifo cha Rina zilisambaa kwa kasi na vijana wadogo pambe mbalimbali duniani walianza kujiua.
Inakadiriwa nchini Urusi walijiua watoto takribani 130 kupitia mchezo, nchini Marekani 2 na India 1 huku mwingine akipata majeraha na kuweeza kupona.
Huu mchezo ulihusisha mchezaji kupewa majukumu madogo madogo ambapo alipewa jukumu moja kila siku kwa siku 50. Kila siku ugumu wa jukumu uliongezeka. Majukumu hayo yalihusisha kujikata, kujidhuru, kuua wanyama na mwisho ilikuwa ni kujiua mwenyewe hasa kwa kujirusha kutoka ghorofani au kujirusha mbele ya train au gari lililo kwenye kazi ili kukamilisha mchezo.
Na kweli watoto wenye umri wa miaka 13-17 walikuwa wahanga wa mchezo huu.
Ajabu ni kwamba ni mchezo ambao uliwavutia watoto wengi huko Ulaya, Marekani na Asia. Wazazi walianza kuwa ana wasiwasi juu ya watoto wao kutumia mitandao maana mchezo huu ulikuwa ukichezwa katika makundi huko mtandaoni.
Binti wa pili kujiua kwa mchezo huu anajulikana kama Angelina DAvydova naye ni wa Russia. Yeye alikuwa na umri wa miaka 16 na alijiua mwezi mmoja baada ya Rina. Alijiua kwa kujirusha kutoka juu ya ghorofa. Na baada ya kujiua bofyfriend wake naye alijiua.