Ufahamu mchezo wa ngumi unaoitwa Musangwe

Ufahamu mchezo wa ngumi unaoitwa Musangwe

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Habari ya uzima wanaJF ni matumaini yangu kuwa mnaendelea Vyema sana pia niwape Pole wagonjwa. Kama ilivyo Kawaida yangu ya kupitia vyanzo mbalimbali vya kimtandao pamoja na makala kadhaa basi leo Naomba nilete uzi huu maalumu kuhusu Moja kati ya mchezo wa kipekee barani Afrika unaopatikana nchini Afrika ya Kusini.

IMG_1493.jpg

Kutana na Kabila la Wavenda linalopatikana huko Afrika ya Kusini; ambapo wanaume hukutana uwanjani na kutengeneza mfano wa duara la kiasi tu kisha wapambanaji wawili huingia ndani ya duara hilo mfano wa ulingo. Huku mashabiki waliotengeza duara hilo wakipiga makofi na kuongeza makeke kunongesha mpambano. Mchezo wa Musangwe.

IMG_1492.jpg

Ni mchezo wa kipekee sana Kwani hufanyika siku Za Jumamosi kwenye kijiji cha Tshifundi. Ni wakati ambao wahusika huwa kwenye mapumziko na hujumuika kuendeleza utamaduni ambao umedumu kwa zaidi ya Miaka 200; yaani mtu achezee vitasa mpaka aombe radhi.

IMG_1494.jpg

Mchezo wa Musangwe ni mchezo wa kikatili sana Kwani wapambanaji hupigana wakiwa hawana gloves wala kitu chochote hivyo ni mwendo wa makonde tu na vitasa vya kutosha. Ingawa Afrika ya Kusini pamoja na dunia imebadilika lakini Bado kuna sehemu kama Milima ya kaskazini mwa Afrika ya Kusini. Kila wiki watu hukusanyika kwa ajili ya musangwe; ili kuoneshana umwamba.

IMG_1495.jpg

Sheria za mchezo huu ni rahisi ila hatari; hakuna kuvaa gloves, wala kilinda meno na hakuna kikomo cha muda wa kupigana. Hata kama utazidiwa; unaweza kusimama na kuendelea kupambana. Kitu kikubwa ni mmoja wao kunyoosha mikono kusurrender. Hakuna mambo ya kamari. Ukiachilia mbali majeraha; wapambanaji hutoka wakiwa na heshima na sifa kwa watazamaji.

IMG_1496.jpg

Tshilidzi Ndevana almaarufu kama Sumu ndo bingwa mkali kwa sasa. Ana Miaka 56 Mwalimu wa shule na baba wa watoto watano. Na Bwana Tshilidzi aliingia kwenye mchezo huu akiwa na Miaka kumi tu.

IMG_1499.jpg

Kukitokea kutokuelewana baina ya watu basi suluhu ni kwenda kwenye mpambano huu; ambapo uchukuliwa kama kuondoa kinyongo baina ya watu.

IMG_1497.jpg

Naomba nimalizie Hapo kwa leo mpaka Wakati Mwingine tena wanaJF.

Shukrani sana kwa kuchukua muda wako kusoma uzi huu.
 
Mutsaambwe ni zimbabwe mkuu nilikuwa nàufuatilia sana enzi za kina diesel, cyborg, kota ilikuwa shida tupu
 
huu ndo mchezo nilioshuhudia mtu kazimishwa (kapoteza faham) akatibiwa kwa kupigishwa nyeto....

yaan daktar wao mtu akila ambakat akataka kuzima fasta anashushwa sarawili anapigwa blowjob[emoji3] dah ... hii dunia

nb: utafute youtube utauona...
 
Apana kwakweli,angalau basi kungekuwa na malipo kwamba mnashindana alafu mpambano ukiisha mnavuta chenu.
Lakini mnapigana tu ili kumaliza vinyongo?
 
Blow Job [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Apana kwakweli,angalau basi kungekuwa na malipo kwamba mnashindana alafu mpambano ukiisha mnavuta chenu.
Lakini mnapigana tu ili kumaliza vinyongo?

Unetisha [emoji16]
 
huu ndo mchezo nilioshuhudia mtu kazimishwa (kapoteza faham) akatibiwa kwa kupigishwa nyeto....

yaan daktar wao mtu akila ambakat akataka kuzima fasta anashushwa sarawili anapigwa blowjob[emoji3] dah ... hii dunia

nb: utafute youtube utauona...
Hii naikumbuka mpaka kesho
View attachment 1722654
 
Back
Top Bottom