Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Mei 24 kila mwaka, dunia inaadhimisha Siku ya Ugonjwa wa Skizofrenia (World Schizophrenia Day). Huu ni ugonjwa unaoathiri fikra, hisia na kumfanya mtu kushindwa kujitambua vizuri.
Hakuna chanzo kimoja hasa cha ugonjwa wa Skizofrenia, lakini mkusanyiko wa kigenetiki, mazingira na mabadiliko ya mfumo wa kemikali katika ubongo huweza kusababisha mtu kutafsiri uhalisia wa mazingira kwa namna tofauti. Wagonjwa hushuhudia ‘maruweruwe’ katika kuwaza na kuona vitu, hivyo kuathiri utendaji wao wa kila siku.
Sababu zinazoweza kupelekea ugonjwa wa Skizofrenia ni pamoja na:
Mtu mmoja kati ya kila watu 100 duniani yupo katika hatari ya kuugua ugonjwa huu katika kipindi chake cha maisha. Wanaotajwa kuathirika zaidi na ugonjwa huu ni wale wenye umri kati ya miaka 15 na 30, huku ugonjwa huo ukitajwa kuwa kati ya magonjwa 10 yanayosababisha ulemavu duniani katika nchi zilizoendelea.
Kufikia mwaka 2017, takriban watu milioni 20 walikuwa wameathirika na ugonjwa huu duniani, nchi za Australia na Uholanzi zikitajwa kathirika kwa kiwango kikubwa zaidi zikiwa na 0.36% ya wagonjwa wote duniani.
Takriban 50% ya watu wenye wanaougua ugonjwa huu wanatajwa kujaribu kujiua, huku ugonjwa huu ukitajwa pia kupunguza umri wa kuishi kufikia wastani wa miaka 18 tu.
Jinsi ya kujikinga:
Hakuna njia moja inayopendekezwa ya kujikinga na ugonjwa huo. Hata hivyo, Wataalamu wa Afya wanashauri mambo yafuatayo:
Matibabu ya ugonjwa huu huchukua muda mrefu, pengine katika kipindi kizima cha maisha ya mtu baada ya kuathirika.

- Msongo wa mawazo kwa mjamzito huweza kusababisha kuzaa mtoto mwenye hatari ya kupata ugonjwa huo, ingawa hiyo si sababu ya lazima.
- Kwa watoto, kuumia ubongo, ukatili wa kingono au athari nyingine za kiakili huweza kupelekea kupata ugonjwa huo baadaye.
- Matumizi ya dawa za kulevya na uvutaji wa bangi huongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.
Mtu mmoja kati ya kila watu 100 duniani yupo katika hatari ya kuugua ugonjwa huu katika kipindi chake cha maisha. Wanaotajwa kuathirika zaidi na ugonjwa huu ni wale wenye umri kati ya miaka 15 na 30, huku ugonjwa huo ukitajwa kuwa kati ya magonjwa 10 yanayosababisha ulemavu duniani katika nchi zilizoendelea.
Kufikia mwaka 2017, takriban watu milioni 20 walikuwa wameathirika na ugonjwa huu duniani, nchi za Australia na Uholanzi zikitajwa kathirika kwa kiwango kikubwa zaidi zikiwa na 0.36% ya wagonjwa wote duniani.
Takriban 50% ya watu wenye wanaougua ugonjwa huu wanatajwa kujaribu kujiua, huku ugonjwa huu ukitajwa pia kupunguza umri wa kuishi kufikia wastani wa miaka 18 tu.
Jinsi ya kujikinga:
Hakuna njia moja inayopendekezwa ya kujikinga na ugonjwa huo. Hata hivyo, Wataalamu wa Afya wanashauri mambo yafuatayo:
- Usitumie madawa, hasa kwa vijana kwa sababu wakati huo ubongo upo katika mchakato wa ukuaji, hivyo huweza kuathirika kwa urahisi.
- Epuka mambo yanayoweza kukusababishia msongo wa mawazo, kama kuwa kwenye mahusiano yanayokuumiza.
- Jiweke katika mazingira mazuri ya kijamii. Kuwa katika maelewano mazuri na jamii huongeza kujiamini, hupunguza msongo wa mawazo na kujisikia upweke na hukuweka katika hali ya kufanya kazi na kuwa na sababu ya kufanya kazi muda wote.
- Jitunze: kula chakula bora na fanya mazoezi ya mwili.