Ufahamu wako ungependa kujua/kushuhudia nini kabla haujatoeka...?

Ufahamu wako ungependa kujua/kushuhudia nini kabla haujatoeka...?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Matamanio yetu hutofautiana kulingana na vile tulivyo,Muda nao hautupi nafasi kubwa ya kukata kiu ya yale matukio ambayo tungependa kuyaona.
Haijalishi liwe kubwa au dogo kiasi gani,ilimradi ungependa kulijua ama kulishuhudia basi kiu chako kitakata!.

Ni jambo gani hilo..?

Binafsi moja ya kiu yangu kubwa katika ulimwengu huu ningependa kushuhudia binadamu akikua kisayansi zaidi Hadi kufikia hatua ya kugundua maisha nje ya sayari yetu!.
Nijue nini kipo nyuma zaidi ya huu uhai tulionao!,Kama Kuna ancestors wetu wajitokeze tuwaone!.. hata hao Alien wanaosemwa kuwepo basi niwaone dhahiri, nijue uwezo wao Kama wanatamaduni, kiujumla maisha yao!.

Kiu changu chengine kikubwa ni kujua chanzo cha ulimwengu ambacho nitakuwa sina mashaka nacho!,Siri za ulimwengu na kanuni zake nikiyajua hayo hakika furaha yangu itakuwa kubwa zaidi ya jana!..
Japo najua ni ngumu ila hicho ndio kiu changu cha miaka yote!.

Mzunguko wa maisha yetu ukiufikiria ni kama vile hatuna dira ya kidunia!..😅
Wengine najua itakuwa ngumu kunielewa lakini angalia mzunguko huu wa binadamu ndo utaelewa kwanini kiu changu ni hicho hapo juu!.
Tunazaliwa
Tunasoma
Yanatokea ya kutokea lakini kila mmoja lengo lake linakiwa ni kuwa na maisha mazuri tu!,then utazaa nao utakaowazaa watapigania kuwa na maisha mazuri!..

Binafsi naona hichi hakitoshi bado tunahitaji kufanya kazi kubwa Sana ya kufichua vilivyojificha!,kuwa na maisha ya kumudu mahitaji yako tu haitoshi.. sidhani Kama hicho tu ndo kitufe cha nini tunachotakiwa kufanya!!.

Hiyo ni kiu yangu yako je..?
 
Kuna sehemu nimesoma sina uhakika wapi lakini kuna mtu aliyesema kuwa "Tunapenda kusema' 'I will go to heaven" lakini "...tunaogopa kufa...'
Na ndio njia..😂
 
Ni Mungu ndiye aliyeumba, akatuwekea uhai...

Akili za MUNGU hazichunguziki
 
Back
Top Bottom