Sawa tuambie tunawezaje kuupata huo ufalme wa mbinguni duniani ? tuachane na hii mifumo ya kidini
Niliishi kwenye mifumo ya kipentekoste zaidi ya miaka 20, Nanena kwa lugha ambazo hata mitume wala manabii hawajawahi Nena. Wachungaji waliniambia ni lugha za Malaika, Wakati siyo sahihi, maana Malaika wote walioshuka Duniani walinena lugha za wanadamu. Nimetoka kwa Sasa Nina Amani na nipo huru kuongea na Baba yangu aliye mbinguni Nikiwa huru.
Tukitaka kujua Ufalme wa Mbinguni, ni lazima Kwanzaa tuanze kusoma mwanzo 1:26
Genesis 1:26-27
[26]And God said, Let us make man in our image, after our likeness: and let them have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over the cattle, and over all the earth, and over every creeping thing that creepeth upon the earth.
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
[27]So God created man in his own image, in the image of God created he him; male and female created he them.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Hapo tunaona jinsi baba alivyotukabidhi ufalme baadaye tulipoteza ufalme ,Mfalme Yesu akaja kuturejeshea, kwa hiyo Yesu hakuja kuanzisha Ukristo Bali alileta Ufalme , ukristo ulianzishwa na Rumi kwa ajili ya manufaa binafsi Chini ya udanganyifu wa shetani, Yesu ameleta Ufalme, Rumi imeleta Ukristo.