Mwadilifu Mdhulumiwa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2021
- 419
- 640
Utangulizi:
Ndoa ni muunganiko wa hiari unaotokana na maridhiano baina ya mwanaume na mwanamke. Maridhiano haya hutoka moyoni kwa kila mmoja baada ya kuwa ameshawishika na kuridhika na mwenzake, kulingana na vigezo anavyovitaka na hivyo huamua kuushusha upendo wake kwa mwenzake, humuamini na kuridhia kuishi naye katika maisha ya uhai wake wote.
Hata hivyo katika maisha ya ndoa kuna changamoto nyingi ambazo kama zisipotafutiwa ufumbuzi mwafaka huweza kupelekea ndoa husika kuvunjika na kujikuta wahusika wakilazimika kutoa au kudai talaka kwa mwenzi wake bila kutarajia.
Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa la kuvunjika kwa ndoa nyingi na kupeana talaka mahakamani huku ndoa nyingine zikiwa hata mwaka mmoja haijamaliza tangu ifungwe kanisani. Pengine ni hulka ya vijana wa leo au ni jamii nzima kutokuwajibika ipasavyo kupambana na janga hili.
Katika makala haya, nitajadili baadhi ya sababu zinazochangia kuvunjika kwa ndoa nyingi na hatua za kuchukua kupunguza au kuepukana na janga hili.
Sababu Za Kuvunjika Kwa Ndoa.
Miongoni mwa sababu zinazopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi zinzofungwa miaka ya sasa ni pamoja na hizi zifuatazo:-
Kuingia Katika Ndoa Kwa Kujaribisha
Vijana wengi wamekuwa wakiingia katika ndoa kwa namna kupima joto au kimo cha maisha. Hivyo anapokumbana na hali ngumu ya maisha tofauti na alivyotegemea hukata tama mapema na kuamua kuikimbia ndoa akiamini kuwa huku nje huenda atapata fursa nyingine ya ndoa yenye neema zaidi.
Kuingia Katika Ndoa Bila Kufanya Maandalizi ya Kutosha
Vijana wengi wa siku hizi hupenda kufuata mkumbo wa kufunga ndoa bila kufanya upembuzi yakinifu wa gharama za maisha ya ndoa pamoja na kutunza familoia.
Matokeo yake huanza misuguano, kwani mwanamke huwa mkali kwa kitendo cha mwanaume kushindwa kuhudumia familia, huku mwanaume naye huwa mkali akitaka asibughudhiwe. Hali hii hufika mahala wanandoa hawa hushindana na hatimaye huamua kuvunja ndoa yao na kupeana talaka.
Kuingia Katika Ndoa na Mtu Usiyemfahamu Sawasawa
Katika miaka ya hivi karibuni vijana wengi wamekuwa wakianzisha mahusiano baada ya kukutana mitandaoni kufahamiana sura wala kabila au maeneo ya makazi yao kijiografia. Katika mazingira hayo wengi wao, hujigeuza na kujivika umbo na sura ya uongo tofauti na hali yake halisi. Ndoa nyingi zimevunjika kutoka na mwenzi kuja kugundua kuwa aliyokuwa akielezwa na mwenzi wake ni uwongo.
Mathalani mwanaume anaweza kuwa anakopa fedha na kukodisha gari kila anapokwenda kumtembelea mchumba wake na kudanganya kuwa ni mali yake, huku akifanya matumizi makubwa ya fedha kuonyesha kanakwamba ana uwezo mkubwa wa kifedha, lakini mara baada ya ndoa mwenzi wake huja kubaini kuwa mumewe ni fukara na maisha yake ni ya shida tupu.
Wapo pia wanawake ambao katika kipindi cha mahusiano ya uchumba hujifanya wenye wanyekevu na wenye heshima sana, lakini baada ya kuingia kwenye ndoa huyafunua makucha yao na kuanza kuonyesha kiburi na dharau kubwa kwa mwenzi wake. Hali kama hizi husababisha migoro na misuguano katika ndoa, hatimaye upendo uliokuwepo katika ndoa hutoweka na kupelekea ndoa kuvunjika.
Kupuuzia Shida Za Mwenzi Wako
Kuna hatari ambayo wenza wengi walioko katika ndoa huwa hawaifahamu, siri hii ni kupuuzia shida na matatizo anayokuletea mwenzi wako. Mathalani mkeo anaomba msaada wa fedha akachangie ndugu yake aliyepata tatizo flani ananyimwa, anakuomba fedha ya kutengenezea nyewele ananyimwa, anakwambia hajisikii vizuri, anaumwa anapewa jibu ambalo halimfariji n.k.
Katika mazingira hayo upendo wa mwanamke huanza kutoweka kwani anakuwa haioni thamani yake kwako kama mumewe. Hali hii ikiendelea hupelekea kuvunjika kwa ndoa na kupeana talaka.
Kukosa Uaminifu Katika Ndoa
Uaminifu katika ndoa ni jambo la msingi sana katika kudumisha ndoa husika. Uaminifu ukitoweka katika ndoa, hupelekea kila mmoja kupoteza imani na mwenzake. Baadhi ya matendo yanayochangia kutoweka kwa uaminifu katika ndoa ni pamoja na kuwa na tamaa kupita kiasi. Mathalani Mwanaume au mwanamke anaweza kuwa na tamaa ya kufanya ngono na watu wengine nje ya ndoa hasa kama mwenzi wake hamridhishi sawa au hamumuhudumii ipasavyo.
Wakati mwingine kutengana kimazingira kwa kuishi wilaya au mikoa tofauti ya makazi huchangia wanandoa husika kujikuta wanavunja uaminifu na kutoka nje ya ndoa. Matendo na tabia hizi husababisha migogoro mikubwa sana katika ndoa pale mwenzi mmoja anapobaini kuwa mwenzi wake anatoka nje ya ndoa. Migogoro hii hupelekea kuvunjika kwa ndoa na kupeana talaka bila kutarajia.
Kutajirika na Kufilisika Bila Mpangilio
Ndoa nyingi nchini zimekumbwa na janga la talaka na kupelekea wanandoa husika kutengana kutokana na kufilisika kiuchumi. Familia yoyote ikiwa na uchumi mzuri maisha huwa ni ya raha na amani sababu huwa hakuna changamoto za kiuchumi.
Hata hivyo inapotokea familia iliyozoea maisha ya raha ikaporomoka kiuchumi na kufilisika, maisha huanza kuwa magumu na kupelekea familia kuanza kuishi maisha ya dhiki ambayo haikuyazowea.
Katika mazingira ya aina hii wanawake wengi hukosa uvumilivu na kuamini mumewe ndiye anayetesa familia kwa kuinyima fedha za mahitaji na huduma mbalimbali walizoziwea. Hivyo huanzisha migogoro na misuguano katika ndoa na mwishowe ndoa hiyo huvunjika.
Imani Za Ushirikina
Uchunguzi katika ndoa nyingi zilizo hai na zilizovunjika, unaonyesha kuwa wanawake wengi hupendelea kwenda kwa waganga wa jadi kutafuta madawa ya mapenzi na kimazingira, ambayo huwaroga waume zao kwa njia tofauti ili kuwafanya waume zao kuwapenda kupita kiasi, kuwatimizia mahitaji yao yote hata kama ni ya hovyohovyo,kuwafunga wasitoke nje ya ndoa, kuwafunga mikono wasiwe wakali na kuwapiga hata kama atamkosea vipi.
Inapotokea mwanaume akagundua kuwa mwenzi wake ni mshirikina, huanzisha misuguano na hata kuhama nyumba na kulala nje ya nyumba akihofia kurogwa. Kuanzia hapo misuguano huendelea na kupelekea ndoa husika kuvunjika.
Kutokubali Kujishusha, Ubishi na Ujuaji Mwingi
Kama ilivyo katika muundo wa serikali, kuna mamlaka za juu na mamlaka za chini, Mfano Rais wa nchi yetu akiwa kama mamlaka kuu ya kiutawala ndiye mwenye sauti ya mwisho kuhusu maamuzi ya jambo lolote lile, hakuna mamlaka nyingine inayoweza kupinga au kupingana nae.
Vivyo hivyo katika ndoa mwanaume ni mamlaka ya juu na mwanamke ni msaidizi wake au ni mamlaka inayofuatia.
Hivyo basi kuna mambo ambayo mwanaume anaweza kuwa na sauti ya mwisho katika maamuzi yake. Sasa inapotokea katika ndoa mwanamke akawa mbishi na mwenye kuleta ujuaji kupita kiasi husababisha ndoa kukosa amani na hivyo kupelekea misuguano isiyokwisha kwani kila mmoja atataka awe juu ya mwenzake.
Hali hii hupelekea ndoa nyingi kuyumba na mwishowe kuvunjika na kupeana talaka.
Malezi Mabovu Kutoka Familia za Wanandoa
Malezi mabaya ambayo mwanamke au mwanaume amelelewa na kukulia toka kwa wazazi wake huathiri sana msingi wa tabia na uadilifu wake katika kuyaenzi maadili ya ndoa yake.
Mathalani mtoto wa kiume aliyekulia katika familia ya wazazi walevi wanaotukanana matusi na kugombana hovyo hata mbele za watoto, mwanandoa huyu ni lazima atabeba chembechembe za tabia hizi na kuziingiza katika ndoa yake.
Inapotokea matendo kama hayo yakaingizwa kwenye ndoa, huku mwanamke akiwa hakuwahi kuyazowea wala kutegemea kuyakuta katika ndoa yake, hapa mwanamke huchukuwa uamuzi wa haraka sana kuvunja ndoa na kuondoka.
Je Nini Kifanyike ?
Ili kuepuka au kupunguza wimbi la talaka katika jamii yetu, vijana wote mnaotarajia au kufikilia kuingia katika ndoa manapaswa kuchukua tahadhari zifuatazo:-
Serikali kwa kushirikiana na jamii nzima haina budi kutunga sera na sheria zitakazoweka msingi thabiti na njia endelevu za kuwezesha malezi na makuzi bora kwa vijana. Aidha katika kutoa mafundisho ya ndoa kwa wanandoa watarajiwa taasisi za dini ziwahusishe pia wadau kutoka raasisi malimali za serikali ikiwemo RITA a mahakama.
Wadau hawa wanaweza kusaidie kutoa mafundisho yatayowajenga vijana kutambua thamani ya uadilifu katika ndoa na athari za kuvunja ndoa.

- Epuka kujiingiza katika ndoa kwa kujaribisha, tambua kuwa ndo ni pingu za maisha. Ukikosea kuingia, ujuwe madhara yake yatakufuata maishani mwako mote.
- Hakikisha mtu unayetaka kuingia naye kwenye ndoa unamfahamu sawasawa. Jipe muda wa kutosha na ujiridhishe sawa kabla ya kufanya uamuzi.
- Fanya maandalizi ya kutosha kabla hujaingia kwenye ndoa, Mwanaume jiandae vema kiuchumi tambua heshima yako mbele ya mkeo na familia itategemea sana uwezo wako wa kubeba majukumu kama baba wa familia. Mwanamke pia jiandae vema na maisha ya ndoa tafuta mafundisho kwa wanandoa wazowefu.
- Epuka kupuuzia shida na haja za mwenzi wako hata kama ni mambo madogomadogo, tambua kuwa hayo mambo ndiyo huchangia kustawisha upendo na amani katika ndoa.
- Jiepushe na mazingira yote yanayoweza kukufanya ukapotea na kutumbukia katika vishawishi vya kuvunja uaminifu. Unapojisikia haja yoyote ya kimapenzi ikite akili yako ikutume kuwa daktari wako wa haja zako ni mwenzi wako tu.
- Iwapo uko mbali na mweza wako, andaeni utaratibu wa kukutana kila wiki au kila mwezi katika siku za mapumziko.
- Iwapo familia itapata mtikisiko wa kiuchumi au kufilisika, mwanaume unapaswa kuwa mpole na muwazi kwa mkeo. Pia mwanamke unapaswa kuwa mvumilivu na kutunza upendo nyakati zote za shida na raha.
- Epukana na imani za ushirikina katika ndoa, dawa ya kuimarisha ustawi wa ndoa ni kuyaenzi maadili yote ya ndoa kikamilifu, bila kumsahau Mungu kama mlinzi na kiongozi wa ndoa yako.
- Epuka kuanzisha mijadala itakayoleta mabishano yasiyo ya lazima. Mwanamke kubali kujishusha mbele ya mumeo hata kama umesoma au una cheo kikubwa kiasi gani, tambua mume ana nafasi yake katika maisha yako.
- Kunapotokea mgogoro wa ndoa au unapoona mwenzi wako ameanzisha tabia zisizo eleweka, Jitahidi kushirikisha bila kuchoka viongozi wa kiroho na wazazi wa pande zote mbili kutafuta ufumbuzi w a haraka.

Upvote
6