Ufanye nini kuondoa msongo wa mawazo kwa matendo uliyotendewa na mzazi wako?

Ufanye nini kuondoa msongo wa mawazo kwa matendo uliyotendewa na mzazi wako?

Rayz

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2016
Posts
339
Reaction score
261
Salaam wakuu!

Ilishawahi tokea hali ya kupelekwa polisi na mzazi wako na ukakaa lupango zaidi ya wiki ukiwa mtoto let say wa miaka kama 12 hivi, ulifanyaje ili kuondokana na mawazo mabaya kwa mzazi wako, na nini kifanyike kuondoa msongo kwa mtu aliyepitia hali kama hiyo?
 
Salaam wakuu! Ilisha wahi tokea hali ya kupelekwa polisi na mzaz wako na ukakaa lupango zaid ya wiki ukiwa mtoto let say wa miaka kama 12 hiv, ulifanyaje ili kuondokana na mawazo mabaya kwa mzazi wako, na nini kifanyike kuondoa msongo kwa mtu aliyepitia hali kama hiyo?
Sijawahi ingia lupangu. Japo lupango unaweza ingia hata kama huna kosa, ila namuomba Mungu aniepushe na hilo. Ee Mwenyezi Mungu ninusuru na hili jambo. [emoji120]
 
Kama mzazi wako asingekuhimiza kuhusu Shule basi hata hii post usinge weza kuiandika hapa,Mzazi wako alikuhimiza kuhusu elimu kwa manufaa yako.
Je kwa mtazamo wako unaweza mpeleka mtoto lupango kisa hataki kwenda shule?
 
Ukiona mpaka mzazi mwenyewe anakupeleka lupango , jua anakupenda sana na hayupo teyari kuona kwa macho yake ukifunzwa na walimwengu mpaka kukata roho..

Walimwengu wanafunza vibaya sana, bora kufunzwa na mzazi
 
Ukiacha kukataa shule, ni tabia gani zingine ulionyesha ambazo mzazi wako alikuwa anakulalamikia sana?

Miaka 12 ni mtoto mdogo sana ujue kwa mzazi kuona amekushindwa na kuamua kukupeleka mikononi mwa polisi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Yaani Kabla hata sijajua ulifanya Nini wewe utakuwa ulikuwa mtukutu balaaa,,,,, Kichwa Nazi[emoji848][emoji848][emoji848]
Je ni sahihi kumweka mtoto lupango na akafungwa na yale maminyororo mazito wiki nzima kisa utukutu?
 
Kuna jamaa mmoja humu JF alikuwa annasimulia, mtoto wa mjomba wake aligoma kwenda shule akaanza kushinda mtaani anavuta bangi na wenzie, wakaanza kupora watu Mali zao Kama panyaroad, siku ya siku wameenda kupora bodaboda wamekamatwa na wananchi wamechomwa Moto na matairi, mzazi akaletewa maiti nyumbani, mzazi Kama huyo alikosea kumhurumia mwanae kutokumpeleka lupango, hujakua wewe, umekuwa mtu mzima bado unaona mzazi alikuonea, unaanza kutaka kupata huruma za Wana JF, eti msongo wa mawazo, ulitaka huo msongo wa mawazo aupate baba yako kwa kukuangalia tu unavyoharibika au? Mada ya hovyo Sana umeleta.
 
Siyo mada ya hovyo, tuendelee kujifunza. Kwa hiyo hakuna njia nyingine sahih zaid ya kumfunza mtoto zaid ya kumpeleka selo?
 
Back
Top Bottom