Ufanye nini tairi likipasuka (basti)

Ufanye nini tairi likipasuka (basti)

Asante kwa kuShare!

Niliwahi kupata mkasa wa tairi ya nyuma ya Suzuki-Maruti kupasuka na nilikuwa moto bati nikiwa na mdingi Mandera Road maeneo ya Vingunguti, sikupaniki na sikukanyaga breki Mpaka ilipopungua mwendo!

Changamoto ni kuiweka kwenye mstari jasho lilinitoka!
 
Aiseee![emoji134] kiweka nyutro "N" ni kujiongezea hatari sababu gari litakuwa jepesi zaidi,

Kuongeza mwendo napo ni hatari maana gari itakuwa haina balance,

Kweli ni vizuri kuondoa mguu taratibu kutoka kwenye eksileleta na kuanza kukanyaga breki taaratibu taaratibu sana kama ukiweza.....ukikanyaga kwa ghafla breki aisee spidii ambayo unatembea nayo ndio spidi ambayo itakutupa nje kupitia kioo cha mbele kama hujafunga mkanda, na ndio spidi hiyo hiyo gari itabinuka na kubilingita.

NB: epuka kupaniki ukiwa dereva....kama ukipaniki basi ndani ya sekunde chache uwe umeshajimaster na kuwa calmed.
 
Inaonyesha ni jinsi gani usovyojua udereva. Gari iko 160kph ikilia mbata utaona vumbi kisha giza ukifumbua macho mamako mzazi kashika bakuli la uji na ina drip mkono wa kushoto

Kama mzaha nimejikuta nacheka sana japo ndio hali halisi kwa asilimia kubwa
 
Aiseee![emoji134] kiweka nyutro "N" ni kujiongezea hatari sababu gari litakuwa jepesi zaidi,

Kuongeza mwendo napo ni hatari maana gari itakuwa haina balance...
Tusidanganyane kagua gari kabla ya safari. Tumia yairi sahihi. Ona hiyo tairi ya afande imebanduka utafokiri omefanyiwa retreading. Kama una safaro ndefu upepo weka 35kpa.

Tairi kama kumho blacklion au kwa ujumla tairi ya uzi haifai kwa safari ndefu. Gari kama kuruza mkonga kilimo kwanza prado tumia BFG. Tizama tairi kama ina machacha ukiona machacha itoe haraka.

Viongozi wetu waepuke kuendeshwa kwa kasi. Unakimbilia wapi? Naupendaga msafara wa JPM na mama samia ni wa taratibu na wa kistaarabu. Pia prof.mihongo anapenda mwendo wa kistaarabu.
 
Ujue kuna mambo huwa yanatokea, nafikiri si kwa ujanja wangu/wako/wetu.

Yaani naweza kusema Mungu anatuongoza.

Ilishawahi kunitokea Tairi la mbele lilipiga Mzinga halafu mie nilikuwa KIBATI.

Yaani hata sasa hivi ukiniuliza niliwezaje wezaje mpaka kufikia CHOMBO kukisimamisha salama bila kupinduka, au hata Mimi mwenyewe kuumia.

Jibu sina.

Yaani haielezeki.

Ujue kimaongezi, ni rahisi sana kusema fanya hivi, fanya vile.

Lakini litakapotokea la kukutokea, kitu cha kwanza Akili lazima ikuruke, kwasababu ni kitu ambacho hukutegemea na kimekujia ghafla.

Kuna mambo huwa hayana KANUNI
 
Ukikutwa na hali hii tairi kupasuka usikanyage break wala kuongeza mwendo, toa mguu kwenye mafuta, fungua vioo ili gari iwe nzito.
 
Ukikutwa na hali hii tairi kupasuka usikanyage break wala kuongeza mwendo,toa mguu kwenye mafuta,fungua vioo ili gari iwe nzito
... mada nyingine za ajabu sana. In short, tairi likipasuka utakuja kugundua lilipasuka a week later ukiwa umezungukwa na doctors na ndugu zako ICU; otherwise, you will never get any information about what happened for ever and ever! La muhimu omba Mungu isitokee achana na vijifomula vyako vya kijinga.
 
Acha nicheke balaa la jf hili
 
Mercedes Benz tairi ikipasuka ikiwa kwenye mwendokasi wa 240km/h utasikia mlio tu, lakini gari haitavuta wala kupinduka wala kukudhuru.
Kilimo Kwanza Sasa......
Hii itakuwa imetengenezwa kiwanda cha Hayati ..
 
Gari nyingi siku hizi zina ABS hii husaidia gari kupunguza mwendo kwenye situation km hii

Watu wengi hudhani tair ya mbele ni hatari zaidi ikipasuka ila mimi nakwambia tairi ya nyuma ni hatari zaidi..kwa hizi gari ndogo zisizo na double tyres nyuma.

Tairi ikipasuka wee wala usipaniki kikubwa komaa usitoke nje ya mstari kisha rudisha gia kwenye 3 km ni auto km ni manual anza kupangua gia tu.

Hii itakusaidia sana
 
Tusidanganyane kagua gari kabla ya safari. Tumia yairi sahihi. Ona hiyo tairi ya afande imebanduka utafokiri omefanyiwa retreading. Kama una safaro ndefu upepo weka 35kpa.

Tairi kama kumho blacklion au kwa ujumla tairi ya uzi haifai kwa safari ndefu. Gari kama kuruza mkonga kilimo kwanza prado tumia BFG. Tizama tairi kama ina machacha ukiona machacha itoe haraka.

Viongozi wetu waepuke kuendeshwa kwa kasi. Unakimbilia wapi? Naupendaga msafara wa JPM na mama samia ni wa taratibu na wa kistaarabu. Pia prof.mihongo anapenda mwendo wa kistaarabu.
Darasa la nne la zamani au?
 
Back
Top Bottom