Ufanye nini ukitukanwa na mkuu wa shule?

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
895
Reaction score
571
Ndugu wana JF. Kuna mwalimu mmoja wa kiume ambaye amejitolea kufundisha kwenye shule moja ya sekondari inayomilikiwa na serikali. Siku moja aliitwa na mkuu wa shule na kuambiwa kwamba yeye ni mwanamme suruali kwa sababu ni mpole sana pale shuleni. Anaomba kufahamu maana ya kauli hiyo. Kama kauli hiyo ni mbaya anastahili kuchukua hatua gani dhidi ya mkuu wake wa shule. Naomba tumsaidie mtu huyu ili ajue hatua za kuchukua.
 
Kila mtu anayo haki kuheshimiwa,bila kujali kada ya ya mtoa heshima na mpokeaji...Ikiwa huyu mwalimu X katukanwa na mwalimu Y na ana ushahidi wa kutosha,pamoja na vielelezo basi sheria zipo wazi! Anaweza kufungua mashitaka na ikibainika bila shaka, kwamba ndugu Y alitenda hiyana dhidi ya ndugu X ndipo sheria ichukue mkondo wake!
 
Ndugu wana JF. Kuna mwalimu mmoja wa kiume ambaye amejitolea kufundisha kwenye shule moja ya sekondari inayomilikiwa na serikali. Siku moja aliitwa na mkuu wa shule na kuambiwa kwamba yeye ni mwanamme suruali kwa sababu ni mpole sana pale shuleni. Anaomba kufahamu maana ya kauli hiyo. Kama kauli hiyo ni mbaya anastahili kuchukua hatua gani dhidi ya mkuu wake wa shule. Naomba tumsaidie mtu huyu ili ajue hatua za kuchukua.
  • Je mkuu wa shule ni jinsia ipi? Je ni ME au KE.
 
Nasikia sheria za utumishi wa walimu haziruhusu kukimbilia mahakamani.
 
Jinsi ya mkuu wa shule ni KE. Amemtukana mwalimu wa kiume. Kamwambia yeye ni "mwalimu suruali."
 
Ndugu wana JF. Kuna mwalimu mmoja wa kiume ambaye amejitolea kufundisha kwenye shule moja ya sekondari inayomilikiwa na serikali. Siku moja aliitwa na mkuu wa shule na kuambiwa kwamba yeye ni mwanamme suruali kwa sababu ni mpole sana pale shuleni. Anaomba kufahamu maana ya kauli hiyo. Kama kauli hiyo ni mbaya anastahili kuchukua hatua gani dhidi ya mkuu wake wa shule. Naomba tumsaidie mtu huyu ili ajue hatua za kuchukua.

Acha kazi. Walimu wengi Tanzania ni wakorofi japo wanadai haki zao. Ukifuatilia kwa usawa bila hiyana, walimu tulionao si walimu bali ni waganga njaa. Na hasa walimu wakuu. Maadili ya utumishi wa Umma kwao ni hadithi ya sungura na fisi.
 
Mkuu wa shule hana kosa hapo alikuwa yupo kazini hakuna obstructive anaweza kwenda wizarani sio kwenye mahakama na huyo mwalimu awache mambo ya nonsense aendelee kusomesha watoto
 
Kama mkuu wa shule ni jinsia ke basi msamehe kwani anaonekana alikuwa na self interest bt kama angekuwa ni jinsia me basi ningekushauri umpige na kitu chenye ncha kali
 
Alitukanwa wakiwa wawilu tu, sasa mahakamani atathibitishaje kama kweli alitukanwal?
 
Back
Top Bottom