vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 895
- 571
Ndugu wana JF. Kuna mwalimu mmoja wa kiume ambaye amejitolea kufundisha kwenye shule moja ya sekondari inayomilikiwa na serikali. Siku moja aliitwa na mkuu wa shule na kuambiwa kwamba yeye ni mwanamme suruali kwa sababu ni mpole sana pale shuleni. Anaomba kufahamu maana ya kauli hiyo. Kama kauli hiyo ni mbaya anastahili kuchukua hatua gani dhidi ya mkuu wake wa shule. Naomba tumsaidie mtu huyu ili ajue hatua za kuchukua.