Ufanyike msako maalumu nchi nzima kuwanasa mafamasia wasio na sifa

Ufanyike msako maalumu nchi nzima kuwanasa mafamasia wasio na sifa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
tfda.jpg

KWA UFUPI
Inashangaza kuona kuwa, pamoja na kuwachuja wauguzi hao waliokuwa wameomba kupewa mafunzo ya uuzaji wa maduka ya dawa muhimu, bado walikuwapo wengine waliobainika kutokuwa na ujuzi wowote katika fani hiyo.

Habari kwamba watu 462 kati ya 1,205 waliokuwa wakisailiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Baraza la Wafamasia katika Mkoa wa Mwanza wamebainika kuwa na vyeti feki ni za kushtua na kutia hofu kubwa. Kubainika kwa watu hao kulijitokeza wakati walipokuwa wakifanyiwa mafunzo kuhusu uuzaji wa dawa katika maduka yanayouza dawa muhimu ambayo hutolewa tu kwa maelekezo ya madaktari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza juzi, Mratibu wa Mpango wa Maduka Muhimu unaoratibiwa na Baraza la Wafamasia, Richard Silumbe alisema Mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliobainika kuwa na vyeti bandia. Kwa mujibu wa mratibu huyo, asilimia 46 ya watu waliofika katika usaili huo walikuwa na vyeti bandia vinavyodaiwa kutolewa na baadhi ya hospitali mkoani humo. Alisema hali hiyo haikubaliki, hasa kutokana na ukweli kwamba watu hao wapo dukani na wanaendelea kuwahudumia wananchi.

Kama tulivyodokeza hapo juu, hali hiyo ni ya kushtua na kutia hofu kubwa. Inapofikia wakati sekta muhimu kama ya afya ikavamiwa na watumishi ambao hawana sifa ya kutoa huduma nyeti kama hizo, ni ushahidi kwamba hakuna mwananchi hata mmoja aliye salama.

Inashangaza kuona kuwa, pamoja na kuwachuja wauguzi hao waliokuwa wameomba kupewa mafunzo ya uuzaji wa maduka ya dawa muhimu, bado walikuwapo wengine waliobainika kutokuwa na ujuzi wowote katika fani hiyo.

Jambo lililozidi kuleta utata ni kuwa, kati ya watu hao 1,205 waliofika katika usaili huo, 743 vyeti vyao havikuonyesha kasoro yoyote. Lakini ulipokuja mtihani, wengi wao walishindwa kujibu maswali hata yale ambayo hayahitaji mtu kuwa amesomea mambo ya afya. Hapo ndipo ilipogundulika kwamba wengi wao walikuwa wauguzi feki na vyeti walivyokuwa navyo vilikuwa vya kuazima au kukodi.

Hatuoni haja ya kusisitiza umuhimu wa kuwapo maduka hayo ya dawa muhimu, kwani mpango huo umeanzishwa kwa ajili ya kutoa huduma sahihi kwa wananchi tofauti na hali ilivyokuwa huko nyuma. Wizara ya Afya inasema umuhimu huo ndiyo hasa ulioifanya kuamua kujiridhisha kuhusu watoa huduma hao kwa kuwapatia mafunzo ili waweze kutoa huduma za uhakika.

Kwa kiasi fulani, wizara husika lazima ikubali kubeba lawama kwa kuacha tatizo la vyeti bandia kukua hadi kufikia kiwango hicho. Ni jambo lisiloeleweka kwa watumishi wa sekta hiyo nyeti kupewa ajira kwa kutumia vyeti bandia pasipo kugundulika. Swali ambalo ni vigumu kupata jibu ni kuwa, ni watu wangapi nchi nzima hadi sasa wameathirika kiafya kutokana na kupewa huduma na watu hao ambao hawana sifa isipokuwa wanatumia vyeti feki?

Nani asiyejua kwamba wamiliki wengi wa maduka hayo ya dawa muhimu wanakodi vyeti vya mafamasia ili maduka hayo yaweze kusajiliwa na kufanya biashara, kama wafanyavyo askari wanaokodisha silaha kwa wahalifu na kulipwa fedha kila wanapofanya hivyo?

Tunadhani sasa ni wakati mwafaka kwa Serikali kufanya msako nchi nzima ili kuwanasa mafamasia feki na maduka ya dawa muhimu yenye wahudumu wasio na vyeti wala sifa.

Msako huo ufanyike kuanzia makao makuu ya mikoa na wilaya hadi tarafa, kata, vijiji na vitongoji. Ni kwa njia hiyo tu tutaweza kuepuka maangamizi ya maisha ya wananchi.http://www.mwananchi.co.tz/uchambuzi/-/1597604/1725312/-/m3pcl7z/-/index.html

Aiseee safi sanaaaa maana unaenda sehemu zingine unasema unaumwa malaria unapewa viagra mahusiano wapi na wapi?thus only happen in bongo land
 
Kaka Mzizi Mkavu. Haitasaidia.

SHeria zipo, mechanism za ukaguzi zipo. Tatizo ni weledi.

Wakaguzi wanalipana pocho za ukaguzi wakifika kwenye famasi wanachukua rushwa.

Ukifanya operation nchi nzima leo, the following year ukirudi unakuta hali imerudi palepale. Swala la ukaguzi linapaswa kuwa endelevu. Na ili liwe na manufaa rushwa lazima idhibitiwe.

Kwa sababu maduka ya dawa hayauzi dawa "gizani" hata kukagua ni rahisi tu. Tatizo weledi...
 
Mkuu ZeMarcopolo Kwa maneno yako yaani hii nchi inaongozwa na wachache wenye pesa za kutoa rushwa? Watoaji na wapokeaji wa rushwa ndio wanaofaidi hii cnhi kuliko sisi walala hoi masikini tunaoteseka na nchi yetu wenyewe? Tupo nchini kama tupo ugeneni mkuu ZeMarcopolo? Kwa Hiyo Tanzania bila Rushwa haiwezi kuendelea?
 
Last edited by a moderator:

Ndugu yangu Mzizi Mkavu.

Kwa bahati mbaya sijawahi kukutana na mtanzania mwenye umri zaidi ya miaka 30 ambaye ni rushwa-free. Kila niliyemuhoji alikiri kutoa au kupokea rushwa wakati fulani.

TAKUKURU ndio wanaongoza kwa rushwa, wakati wanategemewa kupiga vita rushwa! In summary, we are too tolerant to rushwa na "kila mtu" anafikiri rushwa ni mbaya pale tu ambapo mchukuaji au mtoaji rushwa sio yeye.

Ndio maana utaona vijana wa chadema wanakemea ufisadi wa vyama vingine, lakini ukiwaonyesha ufisadi wa chadema wanautetea kwa nguvu zao zote. Kwao wao ufisadi ni mbaya kufanywa na vyama vingine, lakini ukifanywa na chadema hawaoni tatizo!!!
 
Mkuu ZeMarcopolo Kwa maana hivyo hakuna hata chama kimoja kilichokuwa kipo safi na Ufisadi,Rushwa, na kusema uongo? Yaani chama Tawala na vyama vya Upinzani vyote ni swa Ufisadi na Rushwa wapi pa kukimbilia hapo nchini petu? Tutamkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alivyokuwa anakemea mambo ya Rushwa asante mkuu nimekupata.
 
Back
Top Bottom