A
Anonymous
Guest
Kuna malalamiko kuhusu mwenendo wa uuzaji wa dawa katika Kituo cha Afya Katunguru, kilichopo Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza. Tunaomba Wizara ya Afya na mamlaka nyingine husika zifuatilie suala hili ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki.
Baadhi ya wafamasia wanapoingia zamu huleta dawa zao binafsi na kuziuza katika duka la dawa la kituo hicho. Fedha zinazopatikana kutokana na mauzo hayo huchukuliwa na wahusika badala ya kufuata utaratibu rasmi wa mapato ya kituo.
Aidha, kuna malalamiko kuwa dawa hizo zinauzwa kwa bei kubwa na malipo hufanyika kwa fedha taslimu bila kutumia namba ya malipo ya Serikali (control number). Hali hii inazua maswali kuhusu uhalali wa mauzo hayo na namna mapato yanavyosimamiwa.
Pia, Mganga mfawidhi anafahamu kinachoendelea, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa. Hata hivyo, tunaomba suala hili lichunguzwe.
Vilevile, kuna malalamiko kuhusu daktari mmoja ambaye inadaiwa hubeba dawa kwenye begi lake, kisha humwandikia mgonjwa dawa na kumuuza. Tunaomba mamlaka husika lichunguze suala hili na kubaini kama utaratibu unaotumika ni halali.
Hali hiyo imekuwa ikichangia upungufu wa dawa katika kituo hicho, kiasi kwamba wagonjwa wanapofika kupata huduma hukosa dawa zinazohitajika. Inadaiwa pia kuwa pikipiki huleta dawa kituoni wakati baadhi ya wafamasia wanapoingia kazini, kisha dawa hizo huuzwa kwa wagonjwa.
Ombi kwa Wizara ya Afya na mamlaka husika
Tunaomba yafuatayo:

- Kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu uuzaji wa dawa katika Kituo cha Afya Katunguru.
- Kukaguliwa kwa utaratibu wa manunuzi, uingizaji na uuzaji wa dawa pamoja na usimamizi wa mapato ya kituo.
- Kuchunguzwa kwa madai yanayowahusu wafamasia, daktari anayetajwa na uongozi wa kituo.
- Kuchukuliwa kwa hatua stahiki endapo itabainika kuwa kuna ukiukwaji wa taratibu.
- Kuhakikisha wagonjwa wanapata dawa kwa utaratibu halali, kwa bei zinazostahili na bila kukosa huduma kutokana na vitendo visivyo vya kitaalamu.