Ufaransa imetangaza marufuku ya kutotoka nje usiku wakati ambao inakabiliwa na machafuko

Ufaransa imetangaza marufuku ya kutotoka nje usiku wakati ambao inakabiliwa na machafuko

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Ufaransa imetangaza marufuku ya kutoka nje usiku katika baadhi ya maeneo siku ya Jumatatu huku waandamanaji wakizuia lango la Jumba la Makumbusho la Louvre mjini Paris.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati serikali ikijaribu kudhibiti hasira za wananchi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, baada ya maandamano ya mwishoni mwa wiki kugeuka vurugu kubwa za mitaani.

Waziri Mkuu, Sebastien Lecornu, amesema serikali inaweza hata kutangaza hali ya hatari ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya. Kauli hiyo ilikuja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani kusema kuwa polisi walishindwa kudhibiti machafuko yaliyozuka.

Hali hiyo inatokea miezi sita tu kabla ya uchaguzi wa kumchagua mrithi wa Rais Emmanuel Macron. Serikali imesema marufuku ya kutoka nje itaanza saa mbili usiku hadi saa 12 asubuhi katika miji minne ya kaskazini mwa nchi, ikiwemo Lille, kwa lengo la kulinda biashara na mali za wananchi.

Lecornu amesema amedhamiria kurejesha utulivu na usalama wa umma. Takribani watu laki tano walishiriki maandamano kote Ufaransa Jumamosi kupinga gharama kubwa za maisha.
Chanzo : Dw Swahili
 
Back
Top Bottom