Ufaransa inafaidika nini na Niger mpaka itake kusaidia Ecowas kuvunja mapinduzi?

😁 😁 😁 Ukoloni mambo leo
 
Mi naunga mkono mapinduzi hayo, na hata tz natamani pia
 
Asante sana mkuu, najiuliza Nigeria inataka kutima jeshi huko Niger sa mbona wameshindwa kumaliza boko haram nyumbani kwao? Au bokoharam ipo kimkakati? Kwanini hiyo nguvu ya Ecowas isitumike kuondoa makundi ya kigaidi West Afrika?
 
Kama hii ina ukweli basi ni hatari.
 
Lakini mkuu kwa ukwasi wa Gadaffi kwanini asingeomba msaada Russia? Kuwalipa hata Wagner kumlinda?
 
Kuna bomba la gesi limeanza kutandazwa kutoka Nigeria, kupitia Niger linaeekea Ulaya. Ni mbadala ya Nord Stream. Huyo mwamba tangu aingia amestopisha mpango wa hilo bomba. So ufaransa anakuwa furious thats why wanataka jamaa arudi. Pia ufaransa huwa anajibebea Urenium kwa bei ya kutupa, pamoja na kugawana na Niger 50% ya mapato ya exports. So ni pigo kubwa sana kwao ndo maana wanataka kutumia kila means jamaa arudi madarakani
 
France ana wizi wa kibabe sana
Yuko tayari kuwapa silaha waasi ili walete tafrani kwenye nchi na kupigana na jeshi halafu wao wanavuta kiulaini

Sasa Mali wamefuta mikataba yao yote na France tuone
Yaani wamepingulua au talaka moja kwa moja maana naona ulikuwa ni zaidi ya urafiki ni ndoa kabisa

Hapo kwa sisi waafrika wanatafuta ndoa nyingine sasa na Russia naona katongoza
 
......yezebeli anasaini takataka utamwita kiongozi....?
 
Lakini mkuu kwa ukwasi wa Gadaffi kwanini asingeomba msaada Russia? Kuwalipa hata Wagner kumlinda?
Kweni wewe kesho unaijua, hasa watoto wako wanapotaka kukubadilikia unaweza ukajua hilo? Kuna watu wachache walienda kutengenezwa mawazo yao na mzungu, kudai demokrasia kwenye nchi inayo ishi kiimla, wakapitisha kirusi kimya kimya kwa wananchi na baadhi ya viongozi, Gadaffi anakuja kustuka kua siyo NATO tu iliyo mvamia ni pamoja na waLibya wake, ameshachelewa
 
Asee wazungu wanaiba sana Afrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…