Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 4,460
- 13,715
Mwanamke mmoja Mfaransa alitapeliwa zaidi ya $800K na mtu aliyejifanya kuwa Brad Pitt. Walikutana na tapeli huyo Instagram na kumshawishi kwa video na picha zilizohaririwa na kuzalishwa na AI
Tapeli huyo alimshawishi kuwa akaunti zake za benki zilifungwa kwa sababu ya talaka yake na Angelina Jolie na kwamba alihitaji pesa kwa ajili ya upasuaji wa figo.
Alikuja kugundua kuwa ilikuwa ni pitt wa bandia wakati alipuona Brad Pitt kwenye habari na mpenzi wake mpya.