Mkuu, Kansa huharibu mpangilio wa DNA kama ilivyo HIV na yenyewe huharibu DNA na ule Mnyororo unaposomwa, yanaanza kusomwa makosa ambayo husababisha ile sehemu ianze kufanya ndivyo sivyo.
Ndiyo maana nikasema tusubiri wataalamu maana mie niko kwenye Engineering zaidi na Biology sijaisoma kabisa ila nimekuwa nikishiriki sana Story zinazohusu DNA na Virus kwa ujumla Mwilini na kwenye Computer.
Unajua hata HIV mwingine anaweza akasema ni HIV na siyo Virus. Inawezekana tunaongelea jambo hilohilo. Siwezi kukupinga kwa hilo ingawa ukiangalia sana ni kitu ileile kuwa "
chembe chembe za mwili huasi utaratibu na kuamua kuishi milele na kugawanyika/kuongezeka bila mpango" ambapo ni sawa na Virus wakiingia kwenye Computer na Computer huanza kufanya mambo bila mpango unaotakiwa.
Ninavyofahamu mie, si kuwa ZINAAMUA from no where kuishi bila utaratibu ila ni hao VIRUS wanaanza KUZIPOTOSHA na kuzipa Information FAKE. Kwa mfano mmepanga foleni na mnahesabiwa, 1, 2, 3, 4, na ghafla mmoja anasema Baba, badala ya 5, kuna uwezekano anayefuata akasema Mama, Dada, Shangazi, 6, 100 nk nk.
kwani KANSA nayo ni infection? Nayo pia inasababishwa na pathogens? Siyo kwamba ni chembe chembe za mwili huasi utaratibu na kuamua kuishi milele na kugawanyika/kuongezeka bila mpango?