Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la Ufaransa (AFD), imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 361.7 kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa jua.
Mkataba wa makubaliano ya msaada huo umesainiwa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Bw. Frederic Clavier Pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stepanie Mouen Essombe, kwa niaba ya Serikali ya Ufaransa.
Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa Mkataba huo, Bw. Tutuba alisema kuwa mkopo huo utatumika kujenga mitambo ya kuzalisha umeme-jua kiasi cha Megawatt 50 katika Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga.
“Ni matumiani yangu kwamba AFD wataridhia kutupatia fedha kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ya mradi huo iliyopangwa kuzalisha Megawatt nyingine 100 ili kuweza kufikia kiwango cha uzalishaji kilichokusudiwa cha Megawatt 150”, alisisitiza Bw. Tutuba.
Alisema kuwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa lilitoa pia msaada wa Euro milioni 7 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa mradi ambao utatekelezwaji wake utaanza Mwezi Machi 2022 hadi Machi mwaka 2023.
Bw. Tutuba alisema kuwa faida za mradi huo utaongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme na kuiwezesha TANESCO kutimiza malengo yake ya kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali kupitia nishati jadidifu, utapunguza utegemezi wa umeme wa nguvu za maji na kuzalisha umeme wa ziada utakao tumika majira ya ukame.
“Sehemu ya mkopo uliosainiwa utatumika kufanya maboresha na kuimarisha Grid ya Taifa ili kuifanya ya kisasa ili kupunguza upotevu wa umeme” aliongeza Bw. Tutuba
Bw. Tutuba aliishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo huo kwani utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika ambapo utachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine nchini.
Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Bw. Frederic Clavier, alisema kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha Mpango wa Taifa wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26 unafikia malengo yake.
Mhe. Clavier alifafanua kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaifanya Tanzania kushika nafasi ya 2 kwa ukubwa Afrika Mashariki katika uzalishaji wa umeme wa nguvu ya jua na kuifanya TANESCO kuwa na umeme wa uhakika kutoka katika chanzo rafiki wa mazingira.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stephanie Mouen Essombe, alisema kuwa kati ya mwaka 2016 na 2020, Ufaransa imetoa zaidi ya Euro bilioni 6 kwa ajili ya Miradi ya Nishati sawa na shilingi za Tanzania trilioni 17 ambapo kati ya fedha hizo shilingi trilioni 2.8 zimetumika kwenye miradi ya umeme-jua.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa Umeme-Jua mkoani Shinyanga utaiwezesha TANESCO kuzuia zaidi ya tani 43,460 za hewa ya ukaa na kuchangia jitihada za Serikali ya Ufaransa za kuhifadhi mazingira duniani.
“Katika kipindi cha mwaka 2020, Ufaransa imetoa misaada na mikopo yenye thamani ya Euro milioni 330 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 932 na kwamba kusainiwa kwa kiasi kingine cha Euro milioni 130, kutaifanya jumla ya mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Ufaransa kupitia shirika lake kufikia Euro 580 sawa na sh. Tril. 1.6.
Alisema kuwa mwaka huu, Shirika lake linaandaa mkakati ama mpango mpya wa namna ya kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo hifadhi ya mazingira na kilimo endelevu kwa upande wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, miradi ambayo imewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) Mhandisi Dkt. Titto Mwinuka, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, alisema kukamilika kwa mradi huo utachangia kufikia lengo la Taifa la upatikanaji wa umeme kufikia Megawatt 5,000 kufikia mwaka 2025.
Aliongeza kuwa mradi huo utasaidia kuwa na mchanganyiko wa vyanzo mbalimbali vya nishati kwa sababu lengo la Serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya nishati ikiwemo maji, nyuklia na jua.
Dkt. Mwinuka aliahidi kusimamia kikamilifu mradi huo ili ikuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Pia, SOMA

- Mbunge Josephine Genzabuke, aishukuru Serikali ya CCM kwa kupata Mkopo wa Sh. Bilioni Laki Tatu
- Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!
- IMF yaidhinisha mkopo wa Tsh Trilioni 1.2 kwa ajili ya Corona Tanzania
- Tanzania imepokea bilioni 67.82 kutoka Serikali ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo ya KfW
- Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218
- Ziara ya Rais Samia Ufaransa: Tanzania yasaini Mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wa Euro Milioni 178
- Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Tsh Trilioni 1.5
- Tanzania yapokea mkopo wa trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia. Kuboresha tabia nchi, usalama na barabara
- Tanzania yapata Mkopo wa Dola Mil 278 kutoka Benki ya Dunia
- Ufaransa yaikopesha Tanzania shilingi bilioni 195 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Usambazaji wa Maji safi Shinyanga
- IMF yaidhinishia Tanzania mkopo wa Trilioni 2.4
- Tanzania yapewa mkopo nafuu wa trilion 1.24 kutekeleza mradi wa REA na daraja la Jangwani mto Msimbazi
- Benki ya Dunia yaidhinisha Mkopo wa Shilingi Trilioni oni 1.8 kwa Tanzania kwa ajili ya Sekta ya Afya na kuimarisha Uchumi
- Serikali yapata mkopo wa Tsh. Bilioni 650 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mradi wa BRT awamu ya 4 & 5 mwaka 2023
- Tanzania kupata mkopo mwingine wa Tsh. Bilioni 353.3 kutoka IMF ili kusaidia Uchumi
- StanChart Bank Yaipatia Tanzania Mkopo Nafuu wa Shilingi Bilioni 1.4 Kwa Ajili ya Sgr Lot 3 & 4
- Tanzania yapata mkopo wa nyongeza Dola Mil 153 kutoka shirika la fedha duniani (IMF)
- Benki ya Dunia imetoa Mkopo wa zaidi ya Shilingi Bilioni 700 Kwenye Kilimo
- Uingereza Yaipa Zanzibar Mkopo wa Sh.Tilioni 1 Kujenga Uwanja wa Ndege Pemba
- Zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kujenga upya Hospitali ya Muhimbili, Mkopo utalipwa baada ya miaka 25
- Benki ya AfDB yaidhinisha Mkopo wa Tsh. Bilioni 165.6 kwaajili ya kusaidia Benki ya Kilimo Tanzania (TADB)
- African Development Bank yaidhinisha mkopo wa zaidi ya trilioni 1.4 kujenga reli itakayounganisha Burundi na Tanzania
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
- Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar