Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bibie, elimu ina misingi yake ambayo ni muhimu sana kuipitia hatua baada ya hatua, sio kama barabara za Dk. Magufuli ambazo unashusha greda, linaanza kukwangua barabara na magari yanaanza kupita.
Tuliona madudu ya Ndalichako, ndio njia zake hizo? kufelisha watoto wa Kiislaam waliofaulu.
Duh hamtoacha kulalama vizazi hadi vizazi kutokana na kutawaliwa na mawazo mgando,shule zenu ovyooo,vyuo vyenu havina dira ila hamkosi lawama,Mungu wape nusra hawa watu tumechoka na kelele zao.
Mwaka 2014 kule Brazil, imesemwa wingi wa mgoli WC ulitokana na mipira iliyotengenezwa na NASA kwa kwa vipimo wanavyojua wao. Tumepata magoli ya kutosha.FIFA haikuongeza upana au urefu wa magoli, ilichofanya ni kutafuta chanzo cha tatizo.
Kinachofanyika nchini mwetu kinasikitisha sana. Tunajua mfumo wetu wa elimu una matatizo.
Ni kuanzia Walimu wanavyopatikana, mafunzo wanayopewa, masilahi yao yanavyozingatiwa na vitendea kazi wanavyopewa.
Kwa mwaka mmoja tangu matokeo mabaya hatujaonyeshwa kwanini kulikuwa na matokeo mabovu, na mkakati gani uliopo kuondoa tatizo husika. Haiwezekani katika kipindi cha miezi 10 serikali iweze kutafuta suluhu ya tatizo pana na kubwa kama la elimu.
Tunakumbuka mwaka jana walichukuliwa vijana wa div 4 ili kujaza highschool.
Inawezekanaje kwa muda mfupi kiaisi hicho, bila kuambiwa tatizo na mikakati tumepata jawabu rahisi sana kama tunalosoma.
Enedapo tumeweza kufanya hivi katika sekta ya elimu, sidhani kama tungeshindwa ku-balance bajeti yetu kwa mwaka mmoja.
Ni miezi 10 ile ile ya 'kuinua kiwango'' cha ufaulu ingeweza kutumika ku-balance bajeti, na ndani ya miaka 5 kuondoa umasikini.
Inakuwaje tatizo la elimu lipate ufumbuzi wa haraka kiasi hicho huku tatizo la umeme likiendelea kwa miaka 8 ya serikali ile ile. Inawezakanaje tatizo la elimu lipate ufumbuzi haraka wakati tatizo la mishahara ya walimu likiwa ni sugu na lisilo na jawabu.
Hatukatai kuongezeka kwa ufaulu, lakini hili la kutoka 40% kwenda 95 lazima lina sababu.
Je, sababu za kuanzisha Div 5 zimeondoka, au nini matokeo ya kuanzisha Div 5? Mbona hatuambiwi kitaalamu.
Tunachokifanya ni kubumba wataalamu na wasomi wa siku zijazo. Kama alivyosema Naz, huko nyuma tulikuwa na mfumo wa kidato cha sita ambao ulihitaji mtu apate principle 2 na subsidiary moja kuingia chuo kikuu.
Hii ina maana kwa wakati ule mtu aliweza kupata E 2 na S akajiunga na kozi za chuo.
Wataalamu wengi na maprofesa waliopo walitumia mfumo huo. Hii haina maana kuwa na A nyingi za ulaini ni kuongeza ufahamu. Watu wanakumbuka Div 1 au 2 za wakati huo zilikuwa haswa, kila mtu anazikubali. Je, utitiri wa sasa una maana tunafanikiwa?
Hoja hapa ni kuwa kiwango cha ufaulu si tatizo, tatizo ni kama watahiniwa watafikia kiwango kile kwa weledi.
Hapa ni mambo ya kisiasa tu hakuna lolote la maana.
Kinachofanywa ni kukuza div na kupanua wigo wake ili div 3 ionejane bora kuliko 4 na 5.
Lakini, je, hiyo 3 ina maana yoyote?
Je, hiyo 3 ya 2014 inalingana na ipi ya 1980,1990? Je, kama 3 ya kupanua magoli itakuwa sawa na 0 ya 1990 tutakuwa tunajenga taifa la aina gani? Tunamdanganya nani na kwa faida ya nani?
Kama tunavyoona shule za kata zikipigiwa upatu na kuwa ngazi za kisiasa, kinachoendelea ni kuzipa div 1 na 2 ili mbele ya safari ijengwe hoja. Wakati wanafanya hivyo kwetu, wao wako bize kutafutia watoto wao shule South Africa, India na kwingineko.
Sisi tunaendelea kushangilia maafa!
ifike wakati serikal isikimbie ukwel na kuanza kutafuta njia mbadala katika suala la elimu. Tatizo la elimu nchini litaisha endapo WALIMU wataboreshewa maslai yao tu. haiwezekan mtu ambaye hakuangaika kutafuta elimu just form four lakin mshahara wake ni mkubwa tena ana leshen kila katikati ya mwezi maduka yao ni duty free mwalimu Wa TGTS C analipwa 382 000/= hiyo ni take home tena huyo ana dioloma. sasa sijui yule Wa ngazi ya cheti ambao ni primary teachers hali ikoje.
Shirikisheni hata ubongo kidogo jamani mwanafunzi aliemaliza darasa la saba hajui kusoma wala kuandika leo anapata division one form 6 unataka watu washangilie utakua sio mzima
nyie mnasema ufaulu watia shaka wakati askofu akunwa na matokeo
You're very right... ni kwamba muda si mrefu tutakuwa hatuaminiki tena .....and in fact, si tu kwenye ajira bali hata kwenye suala zima la admission kwenye serious higher learning institutions duniani. Haitachukua muda mrefu huko duniani kufahamu kwamba our grading system has changed to the worst grading system. Hilo likishakuwa clear, manake ni kwamba, ukitoka na cheti chako hapa cha NECTA unataka Admission kwenye (say) serious UK universities, lazima pass marks zako wazi-standardize! Ndo hapo tena, unakuta una Div. I, kikiwa standardized, Div I ina-dissolve to Div III na matokeo yake ama kukosa admission moja kwa moja au kupata kozi ambayo hukuhitaji!!Mkuu NasDaz ahsante sana kwa kuziweka nondo za hali ya juu katika post yako # 12. Watanzania tumekuwa wajinga sana kiasi ambacho hii Serikali inafanya uhuni bila hata woga tena kwa kiburi cha hali ya juu huku wakijua fika kwamba uhuni wao unazidi kuchangia kwa kiwango cha kutisha kuanguka kwa elimu nchini.
Sitashangaa miaka ijayo ni Watanzania wachache sana ambao wataweza kupata ajira kwenye makampuni mbali mbali nchini au hata Serikalini kutokana na uwezo wao mdogo utakaosababishwa na kuanguka kwa elimu. Serikali na makampuni hayo itabidi yaajiri wafanyakazi toka nchi za nje ili kukidhi mahitaji yao ya Wafanyakazi. Taifa letu litakuwa ni Taifa la Wajinga kutokana na kiwango cha elimu yetu kuwa duni mno ukilinganisha na nchi majirani au dunia nzima.
You're very right... ni kwamba muda si mrefu tutakuwa hatuaminiki tena .....and in fact, si tu kwenye ajira bali hata kwenye suala zima la admission kwenye serious higher learning institutions duniani. Haitachukua muda mrefu huko duniani kufahamu kwamba our grading system has changed to the worst grading system. Hilo likishakuwa clear, manake ni kwamba, ukitoka na cheti chako hapa cha NECTA unataka Admission kwenye (say) serious UK universities, lazima pass marks zako wazi-standardize! Ndo hapo tena, unakuta una Div. I, kikiwa standardized, Div I ina-dissolve to Div III na matokeo yake ama kukosa admission moja kwa moja au kupata kozi ambayo hukuhitaji!!
subiri wafike huko chuo....Nafikiri wizara ya elimu ilikaa chini na TCU wakabuni mkakati madhubuti wa kuziba pengo kubwa vyuoni lililoachwa kutokana na wanafunzi wengi wa kidato cha nne mwaka juzi kufeli vibaya.