Ufaulu mbovu Kidato cha Nne ni mpango wa Serikali!

Ufaulu mbovu Kidato cha Nne ni mpango wa Serikali!

NGOWILE

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
454
Reaction score
258
Habari wana JF,

Wataalam wa siasa walipata kusema kuwa ili utawale kundi ama jamii kwa namna unavyotaka wewe ni lazima ufanye mambo makubwa mawili, mosi ikiwa ni kuwafanya watu masikini ili wakunyenyekee na pili ni kuwafanya watu wajinga kwa kuwanyima elimu ili wasikuhoji.

Mbinu hutumika na watawala wenye chembechembe za kidictator na hutumia mwavuli wa democrasia kuwahadaa mataifa na wanaowatawala. Nami kuwa umasikini wa watanzania sio mpango wa Mungu bali ni mpango wa watawala kwani kama ni rasilimali nchi yetu ina rasilimali kila kona na sitazitaja kwani sote tunazifahamu. Licha ya rasilimali zote bado nchi ni masikini kiasi cha kuwa ombaomba.

Ni mwendawazimu pekee ndie atakaekuelewa pale utakapomwambia kuwa Tanzania ni kati ya nchi tatu duniani kwa kutegemea misaada ikiwa pamoja na Somalia ambayo haikuwa na serikali kwa zaidi ya miaka ishirini. Aibu hii yote watawala hawawezi kuikwepa kwani kwa mifano hai tumeshughudia wakiiuza nchi kwa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji huwa wazawa wakibaki wanyonge na masikini katika nchi yao.

Tumeshughudia haya katika migodi,ardhi na sasa kwenye gesi. Ni mara nyingi sana wizi wa fedha za umma umefanyika na serikali kukaa kimaa na kuwadaa watanzania kwa maigizo.Nitatoa mfano wa sakata la EPA ambalo lilimuhusu mojamoja gavana wa benki kuu wakati huo Daudi Balali,wakati sakata likiendelea tukasikia kafariki dunia nchini marekani.

Ni nani anayeweza kutupa ushahidi pasipo na shaka juu ya kifo cha balali? kama viongozi wakubwa wa wanaweza kuhudhuria mazishi ya wasanii ni kiongozi gani aliyehudhuria? Kwa kukosa majibu ya maswali haya nakosa woga wa kusema kuna agenda ya siri ili kupoteza ushahidi dhidi ya sakata la EPA. Hii no mifano tu ya namna watanzania tunavyofanywa masikini kwa makusudi. Hapo sikuzingumzia kuuwa viwanda, kuuwa mashirika ya umma, kuuwa kilimo ikiwemo cha mkonge na kahawa na mengine mengi.

Tukija kwenye swala la elimu ndipo ambapo serikali imevurunda kwa makusudi kabisa ili kuendelea kuwahadaa watanzania waendelee kuwatawala.Elimu ya Taifa lolote hubebwa na Falsafa ya taifa hilo pamoja na malengo na matarajio ya taifa hilo.Kwa kuangalia msingi wa elimu ya nchi yetu iliwekwa kwa kuzingatia misingi ya azimio la arusha ambapo lengo la elimu lilikuwa no kuwafanya watu wanahitimu waweze kujitegemea.Hii iliwezekana kwani elimu iliwafanya watu wawe wadadisi, wabunifu, majasiri kwa maana ya watu wanaothubutu, pia iliwafanya watu kuwa wazalendo kwa taifa lao.

Misingi hii ya elimu imekiukwa na watawala kwa makusudi kabisa ndio maana ha mwanafunzi anaesoma shule sasa hajui falsafa wala itikadi ya nchi yake. Ni mwendawazimu pekee ndie atakaeweza kukubaliana na mfumo wa elimu wa nchi hii. Elimu ya nchi yetu imekuwa ikiangalia zaidi idadi ya wanafunzi na madarasa na sio ubora wa elimu inayotolewa. Tumefika mahali mpaka elimu yetu tumeiweka kwenye soko huria kila mtu atoe elimu atakavyo yeye. Utasikia shule hii inatumia mtaala wa kongo, mara malawi tusishangae siku tukasikia shule inatumia mtaa kisukuma ama kichaga.

Ni aibu nchi kuwa haina mitaala ya elimu. Ni aibu sana kusikia wanafunzi wanakaa chini wakati nchi imejaa misitu kila kona.Ni aibu sana mwalimu kuwa ni yule aliyefeli. Shule hazina walimu na wale waliopo wamekata tamaa kutokana na maslahi duni.Shule hazina masbara,vitabu, maktaba nk. Badala ya kutatua matatizo haya inaundwa Tume ya kuchunguza kwanini ufaulu mbovu wa kidato cha nne. Ni mwendawazimu pekee ndiye atakaekuelewa.

Pengine ni makusudi kuuwa elimu ya taifa letu ili wakitangaza ukabila, udini, ukanda na propaganda nyingine za kishenzi dhidi ya vyama vinaelekea kushika dola tuwaelewe. Si muda wote watatudanganya na kutukandamiza.

By Nicholaus Ngowi (mtoto wa seremala)
 
Well said brother and good analysis vp unaendeleaje lakini? Sie tunakimbizana na Prof. Kopoka,don't give up the fight nakuaminia kamanda.
 
Kuna Ukweli hapa, Ukija kwenye ishu ya Umasikini ukijaribu kuangalia yale maeneo ambayo ndo kuna Umasikini wa Kutisha ndo huko CCM ina mizizi cheki maeneo kama SINGIDA, DODOMA,MTWARA,LINDI, TABAORA,PWANI NA TANGA, hii mikoa sehemu kubwa ya wanainchi wake ni Masikini wa kutupwa kabisa ila ndo huku ambako CCM inakubalika sana, na CCM hawezi peleka maendeleo huku make wale wanachi watakuwa bise na shughuli za maendeleo kama biashara na wataisahau CCM , so ili waendelee kuinyeyekea CCM ni lazima CCM ihakikishe hawa watu wanaendeleo kuwa masikini,

Hapa sasa inakuw ni wakati wa Kampeni wakina baba kupewa Kofia na Tshirt, wakina maa wanapa Kanga na vitambaa vya kichwani, hapo kwisha kazi,

Mikioa ambayo isha amka siku nyingi kimaendeleo kama Kiliamnjaro na Arusha CCM hawawezi peleka huu ujinga wa kugawa Kofia na kanga, Haya hufanyika huko Mtwara, Lindi, Tabora, Tanga na kwingineko
 
Ni rahisi sana kumtawala mtu masikini ni asiyekuwa na elimu Chasha
 
Last edited by a moderator:
Watanzania tuna mtindo wa Kudharau Watanzania wenzetu bila sababu za msingi na hii hasa kwa serikali inasababisha kurudisha maendeleo nyuma ya elimu ya nchi kwa ujumla. Mifano

1. Bungeni: Juzi tu wapinzani wamelalamika kwenye mfumo wa elimu nchini kwenye bunge lakini serikali ime dharau na hata hoja haikuruhusiwa kisikilizwa kwasababu tu ni ya upinzani. Watanzania na wana CCM wameweka siasa zaidi kuliko nchi.

2. Mfumo: Kuna mawazo mengi ya kubadilisha mfumo wa shule ambayo yametolwa na watu mbalimbali ikiwa pamoja na Haki Elimu lakini matokeo yake Serikali imekuwa ikiweka siasa na kutengeneza shule za kata kwa kupitia sera za siasa badala ya wataalamu wa elimu. Sasa tuna shule mbovu ambazo hazina na hazitakuwa na walimu. Swala la elimu ni la kisayansi na sio la kisiasa.

3. Watanzania wa Diaspora: Watanzania wenzetu ambao wameenda kutafuta elimu na maisha nje kwasababu tofauti wamekuwa waki dharauliwa bila sababu za msingi. Hawa ni Watanzania ambao wamesoma kwenye system yetu na wamekuwa wanatoa mawazo mengi sana ya jinsi ya kufanya mabadiliko na kuongeza viwango vya elimu. Watanzania wako dunia nzima na mawazo yao yangechukuliwa na kuiga vitu ambavyo wao wameona huko wanapoishi ni vizuri tungeweza kusaidia sana nchi yetu. dharau ambazo hazina misingi zimetolewa kwa Watanzania ambao wengi wao hawana agenda ya ufisadi wala ya kujinufaisha bali ya mapenzi ya nchi lakini wamekuwa wakisemwa kila siku bila sababu za msingi kabisa. Hao Viongozi ambao wanafanya vitu bila kuwa na uzoefu au kujifunza mbinu mpya za kufanya vitu na uongozi wamekuwa wakiweka sera za kijamaa ambazo zimeshidwa dunia nzima hadi Russia, China wamekuwa wakipeleka wanafunzi Marekani kwa masomo baada ya kugundua mfumo wao sio mzuri.

Watanzania cha kwanza cha kubadilika ni kujifunza kusikiliza na kutafakari mawazo badala ya kukimbilia kutafuta madongo ambayo hayatusaidii. Tanzania imekuwa ikisaidiwa kwenye kila kitu kuanzia barabara, afya, budget, maji, umeme n.k lakini wameweka ubishi wa kubadilika au hata kusikia mbinu mpya za maendeleo lakini wanafikiri tutabadilika.
 
Kuna Ukweli hapa, Ukija kwenye ishu ya Umasikini ukijaribu kuangalia yale maeneo ambayo ndo kuna Umasikini wa Kutisha ndo huko CCM ina mizizi cheki maeneo kama SINGIDA, DODOMA,MTWARA,LINDI, TABAORA,PWANI NA TANGA, hii mikoa sehemu kubwa ya wanainchi wake ni Masikini wa kutupwa kabisa ila ndo huku ambako CCM inakubalika sana, na CCM hawezi peleka maendeleo huku make wale wanachi watakuwa bise na shughuli za maendeleo kama biashara na wataisahau CCM , so ili waendelee kuinyeyekea CCM ni lazima CCM ihakikishe hawa watu wanaendeleo kuwa masikini,

Hapa sasa inakuw ni wakati wa Kampeni wakina baba kupewa Kofia na Tshirt, wakina maa wanapa Kanga na vitambaa vya kichwani, hapo kwisha kazi,

Mikioa ambayo isha amka siku nyingi kimaendeleo kama Kiliamnjaro na Arusha CCM hawawezi peleka huu ujinga wa kugawa Kofia na kanga, Haya hufanyika huko Mtwara, Lindi, Tabora, Tanga na kwingineko

Mkuu kuna muda ccm watahama singda,am coming!
 
Ni kweli kabisa, angalia walivoichinjia baharini ile hoja ya "Mitaala rasmi", na Mungu asivo si asumani akafanya itu vyake na mayai yakatotolewa ya kutosha. Hili ni pigo kubwa kutoka kwa Mungu kwa kumkandamiza mnyonge.
 
Kunakipindi huwa nafikiri watawala tuliona sio raia wa Watanzania kutokana na matendo yao.
 
Tokea Uhuru CCM inatumia ujinga wa watu kujihakikishia ushindi ndio maana mara zote Inachukia wasomi
 
quote_icon.png
By Chasha

Kuna Ukweli hapa, Ukija kwenye ishu ya Umasikini ukijaribu kuangalia yale maeneo ambayo ndo kuna Umasikini wa Kutisha ndo huko CCM ina mizizi cheki maeneo kama SINGIDA, DODOMA,MTWARA,LINDI, TABAORA,PWANI NA TANGA, hii mikoa sehemu kubwa ya wanainchi wake ni Masikini wa kutupwa kabisa ila ndo huku ambako CCM inakubalika sana, na CCM hawezi peleka maendeleo huku make wale wanachi watakuwa bise na shughuli za maendeleo kama biashara na wataisahau CCM , so ili waendelee kuinyeyekea CCM ni lazima CCM ihakikishe hawa watu wanaendeleo kuwa masikini,

Hapa sasa inakuw ni wakati wa Kampeni wakina baba kupewa Kofia na Tshirt, wakina maa wanapa Kanga na vitambaa vya kichwani, hapo kwisha kazi,

Soma signature yangu!
 
Back
Top Bottom