UFC254: Khabib Nurmagomedov vs Justin Gaethje

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Baada ya pambano la Israel Adesanya na Costa kufanya vizuri sana kwenye ulimwengu wa 'combat sports' kwenye UFC253, kesho tena tunatarajia kushuhudia pambano ambalo pengine ndio kubwa zaidi kwa mwakahuu linalowakutanisha mabingwa wawili wa UFC 'lightweight', kati ya mrusi Khabib aliyejitengenezea umaarufu mkubwa kwa kumchakaza Conor McGregor na mmarekani Gaethje aliyetoka kumchakaza Tony Ferguson miezi kadhaa iliyopita. Khabib hajawahi kupoteza mechi yoyote kati ya mechi 28 alizocheza wala kupoteza Round, je Gaethje ambaye ni 'underdog' ataweza kutupa upset? Leo usiku tutapata majibu
 
Attachments

  • ufc_20201024_085229_0.jpg
    165 KB · Views: 8
Mmh hapa siongei lolote, nisubiri matokeo tu
Binafsi sioni wa kumsimamisha Khabib kwenye ground game, Gaethje anaweza kushinda tu kama ataweza kumzuia Khabib kucheza game yake kitu ambacho ni kigumu sana. Gaethje ni bingwa kwenye stand up game na amewahi kukiri kwamba ana udhaifu kwenye ground game
 
Safi kabisa. Can't wait kumuona khabib akiendeleza ubabe.
Mkuu hapo kwenye mida umekosea. UFC254 timings zake ziko tofauti kidogo.
Main card inaanza Saa tatu usiku kwa saa za bongo.
 
japokuwa mimi ni shabiki mkubwa wa 'the notorious one' conor mcgregor, lakini nikiri tu kwa kusema kuwa sheikh khabib hafai,, alinichapia mcgregor mwaka juzi hakuna aliyeamini maana conor alichakazwa kama mtoto mdogo ..
 
Tena leo khabib atapigana kwa hasira
na hisia maana ni pambano lake la kwanza baada ya kumpoteza kocha wake ambae pia ni baba take miezi minne mitano ilopita alikufa kwa Corona
 
Game ni saa ngapi wakuu, yaani tatizo la huu mwaka , underdog wote wanashindashinda, ndio maana nina wasiwasi na khabib leo kwa huyo jamaa!!
Alivomduwaza ferguson hata sikuamini , leo mimi natoa 50/50
 
Safi kabisa. Can't wait kumuona khabib akiendeleza ubabe.
Mkuu hapo kwenye mida umekosea. UFC254 timings zake ziko tofauti kidogo.
Main card inaanza Saa tatu usiku kwa saa za bongo.
Sawasawa, ngoja niwe karibu
 
Game ni saa ngapi wakuu, yaani tatizo la huu mwaka , underdog wote wanashindashinda, ndio maana nina wasiwasi na khabib leo kwa huyo jamaa!!
Alivomduwaza ferguson hata sikuamini , leo mimi natoa 50/50
Hata kwenye Boxing Lomachenko,Dillian Whyte wamechezea vichapo vya underdogs
 
Alimfanya kitu kibaya sana Ferguson, sikutegemea kabisa hasa ukizingatia Fergson ni mtaalamu wa viwiko vya kuwachafua sura mahasimu wake, kuna kitasa gaethje alimpa fergy kizito kwenye dakika za lala salama mpaka Ferguson alitingisha kichwa (Kuashiria tayari kimejaa na network haisomi tena).

Alivyompa cha pili ilibidi refa amuokoe Fergy.
Game ni saa ngapi wakuu, yaani tatizo la huu mwaka , underdog wote wanashindashinda, ndio maana nina wasiwasi na khabib leo kwa huyo jamaa!!
Alivomduwaza ferguson hata sikuamini , leo mimi natoa 50/50
 
Hahahaha
 
Ile mechi ilikuwa kali sana, ila Ferguson ni sugu
 
Game ni saa ngapi wakuu, yaani tatizo la huu mwaka , underdog wote wanashindashinda, ndio maana nina wasiwasi na khabib leo kwa huyo jamaa!!
Alivomduwaza ferguson hata sikuamini , leo mimi natoa 50/50

Muda sio mrefu inaanza.
 
He did it. Khabib wins by submission in second round.
Dah analia kabisa akimkumbuka baba ake. Na anasema basi ana retire. 29 fights winning all. Age 32 ni mapema mno ku retire. Maybe atarudi kwa cage tena.
 
Huyu jamaa sijui kama kuna wa kumpiga,kamaliza game kiulainiii[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…