screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Baada ya pambano la Israel Adesanya na Costa kufanya vizuri sana kwenye ulimwengu wa 'combat sports' kwenye UFC253, kesho tena tunatarajia kushuhudia pambano ambalo pengine ndio kubwa zaidi kwa mwakahuu linalowakutanisha mabingwa wawili wa UFC 'lightweight', kati ya mrusi Khabib aliyejitengenezea umaarufu mkubwa kwa kumchakaza Conor McGregor na mmarekani Gaethje aliyetoka kumchakaza Tony Ferguson miezi kadhaa iliyopita. Khabib hajawahi kupoteza mechi yoyote kati ya mechi 28 alizocheza wala kupoteza Round, je Gaethje ambaye ni 'underdog' ataweza kutupa upset? Leo usiku tutapata majibu