ABTWAHILAKILIMALI
Member
- Jan 10, 2015
- 78
- 27
TATIZO NI TAFSIR TULIZOZIBEBA TOKA KWA WAZAZI.
Nikizungumza tafsiri nadhani unanielewa maisha yetu yako hapa yalipo kwa sababu ya tafsir tulizozibeba, hebu kumbuka mama yako alipokwambia tema mate tumchape mtoto mwenzako baada ya kukukosea ulibeba tafsiri kuwa lazima kila atakaekukosea umlipizie, ona leo huna roho ya kusamehe, hebu kumbuka ulipokuwa unaenda kucheza mpira ukirudi nyumbani mama yako anakuchapa fimbo kwa sababu eti watoto wenzio watakufanya usijisomee ukabeba tafsiri kuwa kitu bora pekee ni kusoma shule na kuwa na kazi nzuri na kipaji chako kikafa, ndio maana leo umemaliza chuo huna kazi na hutambui kipaji chako au unafanya kazi ambayo huipendi,na huna kingine cha kufanya.
Hebu kumbuka ulipokuwa ukitoka shuleni umekosa hesabu unakaa nyuma ya nyumba ukiwaza utachapwa kwa sababu umekosa hesabu, na ukaibeba hiyo tafsiri kuwa kushindwa ni kosa kubwa sana na hadi leo unashindwa kuanzisha hata biashara kwa sababu unaogopa itakufa unaogopa kukosea (kushindwa)na unabaki kuwa masikini. Hebu beba tafsiri mpya kuwa kukosea ni sehemu ya kujifunza na matajiri walikosea mara nyingi sana hadi wamefanikiwa.
Hebu kumbuka ulivyokuwa unakatazwa kwenda kwa majirani kisa wao wana pesa na ukaweka tafsiri kwamba ukiwa masikini hutakiwi kukaa karibu na matajiri ni kujipendekeza, matokeo yake unashinda vijiweni na kupiga story za siasa na kusema watu eti hao ndio watu wa type yako, unafikiri watakushauri nini kama sio kukukatisha tama hata kama ulikuwa na ndoto kubwa, unafikiri watakwambia nini wakikuona unanunua kitabu usome kama sio kukwambia unapoteza muda na pesa zako, watakushauri nini wanapoona unatoa pesa kuhudhuria mafunzo,ulisoma shule na huku mtaani unasoma tena, nani ka kwambia ukitaka kuruka uambatane na kinyonga ambatana na mwewe utaruka, siku zote kukaa karibu na waliofanikiwa wanakupa njia na mbinu za kufanikiwa na wanakutia moyo hata kama unapokuwa unaona umeshindwa.
Tatizo ni tafsiri tulizobeba kutoka kwenye familia zetu, siwezi kukulaumu maana huenda ulikuwa mdogo hujui, lakini sasa ulishakuwa, hebu futa hizo tafsiri hasi ulizozirithi huko nyuma ndizo zinafanya kuwa hapo ulipo, hebu chukuwa tafsiri mpya kuhusu wewe, kuhusu maisha yako, na familia yako.
Hebu tafsiri kusoma vitabu ni sehem ya kupata mbinu za mafanikio, hebu chukuwa tafsiri kukaa karibu na waliofanikiwa ni kupata njia na mbinu zakufanikiwa, Hebu tafsiri kutoa sadaka ni kufanyabiashara na Mungu, hebu tafsiri kuhudhuria semina ni kupata mawazo mapya ya mafanikio.
Hakuna mafanikio ya mtu mmoja lazima mtu mmoja aungane na wengine ndipo mafanikio hutokea usijidanganye hakuna mafanikio ya mtu mmoja.
Futa tafsiri za kushindwa wewe unaweza, futa tafsiri za umasikini ndani yako kuna mtu tajiri sana mruhusu atokee.
Futa tafsiri mbaya zisizokuletea faida kwenye maisha yako na anza sasa kutafsiri kimafanikio mafanikio yatatokea
Action=SUCCES