Maskini, Tz yetu (si yao)!
Pamoja na kuyasikia hayo ya TICTS 'Tiscan' huko bandarini kama yalivyoelezwa na kamati ya bunge miundombinu pia kwenye gazeti la Thisday, KUNA NYINGINE NILIKUTANA NAYO MAJUZI HUKO MKOANI LINDI.
Kampuni ya kuwait ya KAFARI inayojenga barabara huko Lindi, ilisaini mkataba na Serikali wa 51bilions, lakini hadi sasa kumalizika kwa kazi imelamba mshiko wa 105bilions!
YAANI hizo 54bilions za ziada yasemekana zilitumika kukampeni SISIEMU.
Lakusikitisha sasa kampuni ikajenga barabara kwa tope lililokataliwa na wataalamu wa barabara. Na SISIEMU wakasema DOLE TUPU! ajabu nikaambiwa ati itadumu kwa miaka 20!
Zaidi majuzi serikali hiyohiyo ya CCM akatengua mkataba wa kujenga barabara eneo la daraja la mkapa kwa kuwa KARAFI haikuwa kwenye nafasi ya kushinda tenda, na sasa wametangaza tena ili mazingira mazuri yatengenezwe kuipatia tena kampuni hiyo tenda kusuport hela ya kampeni 2010, MPOOOOOOOOOOO! Wadanganyika? JE tutafika?
Mr Clean, info nzuri... Lakini kabla hatujaweza kuichambua mada hii naomba utusaidie kutuambia ni barabara gani hiyo unayoiongelea? Sababu hapo jamaa wanaweza wakawa na vielelezo kisha tukaonekana kwamba hatuna facts. Uzuri ukituambia ni barabara gani tutatafuta technical info na kutoa wazi hiyo "so called variation/cost overruns" ni ya kweli au girini tuu!! Pia hawa Kharafi kwa wale tulio katika construction industry tunwajua sana kwa mambo yao ya "kupiga mabao" lakini kwa hili hatuwezi kuwahukumu mpaka tujue kulikoni!!
Sisemi kwamba nakataa kwamba kuna mkono wa mtu kwenye hilo swala lakini siwezi kukubali sababu sina vielelezo.
Hili la pili la abortion ya hiyo tender at last minute naomba uangalie hii thread kwani tulishalijaribu kuliweka hapa ili tuambiwe ukweli lakini naona mambo yakawa patupu soma
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8699
Ukweli ni kwamba lazima wote tujue kwamba katika miradi yenye pesa nyingi na migumu kuona mazingaombwe ni ya barabara... Nakumbuka kuna wakati ilifanyika Technical Auditing ya Road Funds ambapo nasikia (through the bomba) ni matumbo matupu yalionekana kule ndani (TANROADS, TAMISEMI, RFB, MOW)...... lakini bahati mbaya report wengi tuliisikia tu na sikusikia tena kama hii ilifanyika tena (iklikuwa mwanzoni mwa 2000s)....
Bottom line is ngoja tumalize kwenye BoT, TICTS, CIS tukimaliza huko then tutarudi kwenye hizi barabara zetu kuanzia quality, tender process, financial aspects kisha tuwasulubu wale waliokula mapesa yetu!!!
UFISADI NCHINI TANZANIA
Ndugu wana jamboforums, napenda nitoe maoni yangu kuhusu tatizo la ufisadi hapa nchini. Ni ukweli usiofichika kwamba Tanzania inakabiliwa na tatizo la ufisadi katika sekta nyingi za umma kwa sababu tu baadhi ya viongozi wa juu serikalini walishindwa kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Aidha ni vyema pia tukatambua masuala mawili muhimu tunapojadili tatizo la ufisadi; kwanza, tatizo la ufisadi lilipo sasa ni matokeo ya utendaji mbovu wa muda mrefu wa baadhi ya viongozi serikalini, pili, mfumo wa utendaji serikalini kwa sasa bado haujakaa sawa kuweza kurekebisha kasoro zote za ufisadi zilizopo. Kutokana na hali hiyo vita dhidi ya ufisadi ni mchakato wa muda mrefu na kwa hali hiyo matatizo yote ya ufisadi hayawezi kutatuliwa kwa wakati mmoja, taasisi moja au mtu mmoja.
Kwa hivi sasa hakuna sababu ya kuanza kulaumiana na kukashifiana. Kinachotakiwa ni kujipanga upya ili kuweza kutafuta njia (namna) ya kuondoka hapo tulipo. Tumpe ushirikiano Rais KIKWETE kwani ameanza kuonyesha ushujaa na dhamira yake ya dhati katika kupambana na ufisadi serikalini kwa kufanya yafuatayo:
(i) Rais amefanya maamuzi mazito ndani ya BoT kwa kumfukuza kazi aliyekuwa Gavana wa taasisi hiyo DAUDI BALLALI na kumteua mpya Prof. BENNO NDULU. Halikadhalika ameagiza makampuni na maofisa waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria na fedha hizo zirejeshwe.
(ii) Serikali imechukua hatua dhidi ya kashfa ya Richmond Development Company (RDC) ambapo Novemba 13 2007 kamati teule iliundwa na Bunge la Jamhuri ya Tanzania kuchunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampundi ya Richmond. Uchunguzi huo ulipelekea aliyekuwa Waziri Mkuu EDWARD LOWASA kujiuzulu pamoja na waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini Dk. IBRAHIMU MSABAHA na NAZAR KARAMAGI kujiuzulu. Hatua hiyo ilikwenda sambamba na uamuzi wa Rais wa kulivunja Baraza la Mawaziri na kutangaza jipya tarehe 12 Februari, 2008.
(iii) Serikali imeunda timu maalum ya kuchunguza mapendekezo 23 ya taarifa ya Kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. HARRISON MWAKYEMBE na imekabidhiwa nyaraka zote muhimu kutoka bungeni na imeshaanza kuzipitia kwa kina ili kubaini makosa yoyote yaliyofanywa na wahusika katika mkataba huo wa Richmond.
(iv) Novemba 13, 2007 aliunda kamati ya madini yenye wajumbe kumi na mbili (12), jaji MARK BOMANI akiwa mwenyekiti wa kamati hiyo; lengo likiwa kuzipitia upya (kuhakiki) sheria za madini ili kuiokoa sekta ya madini nchini.
Kutokana na hali hiyo ni vizuri tusubiri hizo hatua anazochukua Rais ili tuweze kutoa maoni ipasavyo.
....... ni vizuri tusubiri hizo hatua anazochukua Rais ili tuweze kutoa maoni ipasavyo.
Kubwaj...., point taken lakini ukifuatilia kwenye posti hiyo na maelezo (referenced) ni kwamba kuna mushkeli mahali..... Pia msisitizo umewekwa kwenye hiyo last part ambayo imekuwa BOLD!!(angalia quote hapo last 3 lines za quote)