Ufisadi katika ununuzi wa jengo la TRA

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,416
Salaam wanajamvi,
Hivi karibuni yapata takribani miezi miwili iliyopita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilinunua jengo la ofisi kwa ajili ya mamlaka hiyo kanda ya Kimara. Jengo hilo lipo maeneo ya Kimara Baruti kandokando ya barabara ya Morogoro na kwa mujibu ya sheria ya mipaka ya barabara jengo hilo limo ndani ya hifadhi ya barabara. Kabla ya hapo jengo hilo lilikuwa likitumika kama bar iliyokuwa ikijulikana kama "Rovena Social Centre". Kuna tetesi kuwa jengo hilo liliigharimu mamlaka hiyo takribani Tshs 800M.

Cha ajabu ni kuwa siku chache tu baada ya ununuzi huo ndipo ukaja mpango wa bomoabomoa ya Magufuli ambayo pia imehusisha jengo hilo lote ambalo linatarajiwa kubomolewa pindi bomoabomoa itakapoanza rasmi.

Maswali yanabaki:
1. Je wakuu wa TRA hawakujua kuwa jengo hilo limo ndani ya hifadhi ya barabara na kwamba lingeweza kubomolewa siku za hivi karibuni? Ikizingatiwa kuwa TRA ni sehemu ya serikali hivyo tunatarajia kuwa sheria watakuwa wanazitambua?
2. Kwa nini ununuzi wa jengo hilo ulifanyika siku chache tu kabla ya bomoabomoa kutangazwa?

Hii inatoa taswira kuwa uuzaji na ununuzi wa jengo hilo ulifanyika kwa makusudi licha ya kujua athari zilizopo mbele yake, kwa madhumuni ya ama kumnufaisha aliyekuwa mmiliki wa hilo jengo au kuitia hasara serikali kupitia TRA au yote kwa pamoja.

Wasalaam.
 
Bongo tena?Unategemea nini zaidi ya ufisadi!
 
Watu waliishakula chao what do you expect yaani "Mtu unaambiwa usikojoe hapa halafu unavua na kukojoa hapo hapo walipobandika hilo tangazo"
 

It seems integrity is sold to the highest bidder.
 
mwenye baa alishakufa, zamani iliita ten night club, lakini mbona iko mbali sana na hifadhi ya barabara? ina maana hata petro station itaondoka, sasa dar kimara itakuwa uwanja wa ndege sio barabara tena maana ni pana mno mpaka njia saba inawezekana
 
mwenye baa alishakufa, zamani iliita ten night club, lakini mbona iko mbali sana na hifadhi ya barabara? ina maana hata petro station itaondoka, sasa dar kimara itakuwa uwanja wa ndege sio barabara tena maana ni pana mno mpaka njia saba inawezekana

Mkuu lile jengo lilipigwa X jamaa waka-repaint. Hiyo shell unayoongea imepigwa X tena kule nyuma kwenye maofisi na gim.
Angalia vizuri pale ubungo maji, mpaka wa barabara uko nyuma ya wizara ya maji, kuna bango kubwa la bluu linaloonesha mpaka wa barabara.
Upande wa pili mpaka wa barabara uko nyuma ya lililokuwa "kanisa la mizukule".
Kama sijakosea kwa Morogoro Road mpaka ni mita 33 hivi kutoka katikati ya barabara. Ndio maana Magufuli alisema hata ghorofa la tanesco na majengo ya wizara ya maji pale ubungo lazima yabomolewe.
Ofisi ya Tanroad mkoa wa Dar ilikuwa nyuma ya ghorofa la Tanesco na tayari imeshabomolewa
 
Sikumbuki vizuri eneo hilo likoje lakini nakumbuka wazi kwamba Magufuli akiwa waziri kabla ya kuanza kuhamishwa-hamishwa, maeneo ya Kimara yaliwekwa mabango left-right kuonyesha eneo la hifadhi ya barabara. Hata ukiwa ndani ya gari mabango hayo yanaonekana wazi.

Leo hii utawezaje kununua jengo lililo ndani ya eneo kama hilo. Hata hivyo Siku ipi au jambo lipi linalofanyika ktk nchi hii bila ufisadi?

Ni aibu lakini huyo ndo rais tuliyelaaniwa naye.
 
Kule TRA kuna masalia mengi sana ya PESAMBILI kwahiyo ufisadi ndio kama kazi vile; Jakaya ataishia kushangaa tu wakati nchi inaangamia!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…