Salaam wanajamvi,
Hivi karibuni yapata takribani miezi miwili iliyopita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilinunua jengo la ofisi kwa ajili ya mamlaka hiyo kanda ya Kimara. Jengo hilo lipo maeneo ya Kimara Baruti kandokando ya barabara ya Morogoro na kwa mujibu ya sheria ya mipaka ya barabara jengo hilo limo ndani ya hifadhi ya barabara. Kabla ya hapo jengo hilo lilikuwa likitumika kama bar iliyokuwa ikijulikana kama "Rovena Social Centre". Kuna tetesi kuwa jengo hilo liliigharimu mamlaka hiyo takribani Tshs 800M.
Cha ajabu ni kuwa siku chache tu baada ya ununuzi huo ndipo ukaja mpango wa bomoabomoa ya Magufuli ambayo pia imehusisha jengo hilo lote ambalo linatarajiwa kubomolewa pindi bomoabomoa itakapoanza rasmi.
Maswali yanabaki:
1. Je wakuu wa TRA hawakujua kuwa jengo hilo limo ndani ya hifadhi ya barabara na kwamba lingeweza kubomolewa siku za hivi karibuni? Ikizingatiwa kuwa TRA ni sehemu ya serikali hivyo tunatarajia kuwa sheria watakuwa wanazitambua?
2. Kwa nini ununuzi wa jengo hilo ulifanyika siku chache tu kabla ya bomoabomoa kutangazwa?
Hii inatoa taswira kuwa uuzaji na ununuzi wa jengo hilo ulifanyika kwa makusudi licha ya kujua athari zilizopo mbele yake, kwa madhumuni ya ama kumnufaisha aliyekuwa mmiliki wa hilo jengo au kuitia hasara serikali kupitia TRA au yote kwa pamoja.
Wasalaam.