Msabato Mwema
New Member
- Apr 23, 2014
- 2
- 0
Habari Wana JamiiForum na Wasabato wote Tanzania!
Kwa neema yake Mungu naomba tushirikiane na kuwaza kwa pamoja kama wakristo wano heshimu neno la Mungu kuhusiana na ubadhirifu wa unaofanywa na Mweka Hazina wa Adventist Tanzania Union Mission Ndugu Denis Wairaha.
Ndugu Denisi Wairaha, ndani ya miaka mitatu ya utumishi wake kama mweka hazina amefanikiwa kupata utajiri wa kupindukia wakati watumishi na waumini wa kanisa wakiendelea kuishi katika maisha duni. Kiongozi huyu ametumia muda wake mwingi kuchumia tumbo na si kuibua miradi itakayo leta ufanisi katika shughuli na kazi za kanisa.
Kwa mfano, ndani ya kipindi hicho kifupi, Denis Wairaha amefanikiwa kununua shamba kubwa la ekari 40 lenye thamani isiyopungua TZS 600,000,000/- milioni mia sita sawa na US$ 375,000/- lililopo Arusha maeneo ya Nduruma. Si kwamba hatupendi yeye kufanya ununuzi huu, LA HASHA! kwani ni kwa manufaa yake binafsi na familia yake, pia kama mtanzania ana kila haki ya kufanya maendeleo yake binafis, LAKINI, swali la kujiuliza, Kipatao chake kama mweka hazina kinamwezesha kufanya manunuzi hayo bila ya kuwa na njia za giza na rushwa? Katika kipindi hicho mpaka sasa Denisi Wairaha anapokea mshahara usiozidi TZS 700,000/- sawa na US$ 438/-
Vilevile, ndugu Denis Wairaha, amefadhiliwa na kanisa kujiendeleza kielimu katika level ya Masters ili kuongeza ufanisi katika kazi, lakini cha kushangaza baada tu ya kumaliza elimu hiyo ameamua kufanya uamuzi wa kuacha kazi. Hii inamaanisha kuwa, amelidanganya kanisa na wauumini wake au/na kutapeli pesa/sadaka za waumini kwa malengo yake binafsi yanayoshabiiana na hulka ya ubinafsi.
Pia, mtajwa hapo juu anamiliki daladala tano zilizopo katika jiji la Dar es Salaam.
Akiwa bado anaongozwa na pepo la kujimbikizia mali kwa manufaa yake binafsi na familia yake huku akiwa amejivika joho la kondoo mtakatifu wa bwana, mnamo mwaka 2013, ndugu Denis Wairaha chini ya mamlaka yake alifanya malipo ya Plot za kanisa zenye ukubwa wa ekari 9 jijini Dar es Salaam. Waumini na kanisa kwa ujumla tukaendelea kuaminishwa kuwa tuna ekari 9 Dar es Salaam kumbe SIVYO. Imekuja kugundulika kuwa ekari zilizo nunuliwa ni 5 TU na si 9.
Swali la kumuuliza ndugu yetu Denis Wairaha, ziko wapi ekari zingine 4? zilizogharamiwa na fedha/sadaka za waumini wa kanisa?
Pia Denis Wairaha amekuwa akihusishwa na kulalamikiwa mara kwa mara kwa kushiriki moja kwa moja katika kushawishi na kutoa ajira katika mazingira ya ukabila..yaani amekuwa akipendelea sana kuajiri watu wanotoka katika kabila lake la Wakurya na wakati mwingine kutokana na mazingira ya kazi yake na his God fathers amekuwa pia akitoa upendeleo kwa watu wa kabila la Wapare. Ukimuona machoni kama mtu lakini ndani ya moyo wake amejaa visasi, chuki, fitina na ubinafsi.
Ni bora ukutane na mchawi usiku kuliko kukutana na denis Wairaha mchana.
Maoni: Ninaelewa mfumo wa kulindana uliopo ndani ya kanisa letu, lakini ningependa kupendekeza kuwa Ndugu Denis Wairaha achunguzwe kabla ya kuacha kazi rasmi. Tupo tayari kutoa ushahidi usiopingika kuhusiana na maswala yote tajwa hapo juu.
Na kwa kuwa yeye, ambaye miaka nenda rudi amekuwa akijikweza na kujifananisha na kondoo safi kuliko wote, namuomba aje atoe ufafanuzi wa yote haya na/au kukanusha kwa uthibitisho.
Nawasilisha