MkuuMi naona kuna mambo mawili hapa:
- Kenya wanahofia ujasusi maana huyo jamaa ni profesa wa mawasiliano. Lakini pia kuna ile hali ya 'kawaida' baina ya wakenya na watanzania-yaani love-hate relationship.
- Mi naona huyu profesa hayupo vizuri kivile kama tunavyoamini. Kwa taaluma yake, ilitakiwa awe mbali zaidi ya pale alipo. Sijaona sababu ya msingi ya kuwa dereva wa ubalozi wakati ni telco prof na amefanya miradi mikubwa kama ya Rwanda. Pia watu mtambue kuwa kutengeneza app kama ya profesa sio kitu cha ajabu. Ni app ya kawaida tu ambayo hata mtoto wa JK na mwenzake walitengeneza na wakashinda tunzo ya kimataifa wakati bado walikuwa sekondari. Ukienda vyuo vingi vya bongo (UDSM,NM-AIST, na UDOM) kuna app nyingi tu zinatengenezwa. Tena UDOM mwezi uliopita walikuwa runnersup katika Africa kwa app yao ya VICOBA. So app sio 'uvumbuzi' wa kutisha au kuhitaji afanye udereva ili afanikiwe. Zaidi naona ana tatizo katika personal life (ulevi, gambling, funds mismanagement, etc)
Kutengeneza apps/software ni kitu rahisi lakini apps/software iweze kukuingizia pesa kama jamaa waliogundua M-PESA mpaka Safaricom ya Kenya wanamlipa mwenye M-PESA pesa nyingi kwa kuwa ni mmiliki wa teknolojia hiyo ni habari nyingine.
Inabidi ucheze kama Profesa anavyokaba na kuingia kila kona mpaka kieleweke ili afanikiwe aingize pesa ndefu kama mfano M-PESA niliotaja jinsi wamiliki wa M-PESA wamejikalia ulaya wakisuburi kuvuna percentage ya income toka kila miamala (transactions) ya matumizi ya M-PESA kupitia platform ya Safaricom.