Mr. Ngurudoto, good day. Habari ya huko amerika?
Inaelekea wewe ni mmoja wa watoto wa hao vigogo, unayetanua ughaibuni kwa vijisenti vitokanavyo na wapinda mgongo wa nchi yako. Hongera, ungekuwa mzalendo wa kweli usingejisifia kuishi ukimbizini. Wewe ni mkimbizi kama wakimbizi wengine, kuna wakimbizi wa vita, siasa, njaa, hali ngumu ya maisha n.k.
Kukazia hoja yangu, ni wamarekani wangapi wanapanga foleni usiku na mchana katika balozi zetu huko kuomba viza za kuja kutafuta elimu, kazi au maisha afrika? Hebu kumbuka mlivyosoteshwa kwenye mistari mirefu kwenye ubalozi wa marekani, na kupigishwa kwata za nenda rudi ili kupata viza ya kwenda kuishi huko? Una tofauti gani na mrundi au mnyarwanda anayepanga foleni huko biharamuro?
Sasa ulichokikimbia huku wenzio wanapambana kukiondoa, hao ndio mashujaa wa kweli. Mwoga hata siku moja hawezi kuitwa shujaa. Mnaoishi ugenini kujifanya mnatafuta maisha bila kuimarisha nyumbani ni waoga. Tuachieni tulioamua kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye hili janga tupambane.
Tulipambana kuondoa ukoloni sasa tunapambana kuondoa ufisadi.
Tafakari: Nchini marekani na nchi zote zilizoendelea ni aibu na kosa kubwa mtu kukwepa kodi, hapa nchini ni hao unaowatetea ndo wanaongoza kukwepa kodi. Labla utuambie katika vijisenti alivyonavyo Chenge, ni kiasi gani cha kodi amelipa kwa serikali? Je kuna chombo chochote cha serikali kimewahi kuhoji hilo? Na Viongozi mabilionea wengine je?
Utakataaje kwamba serikali inaungana na wahalifu?
Labda huko ulikokimbilia kunafanyika negotiations kati ya mwivi na mwenye mali kuhusu kurudisha mali iliyoibwa. Is that so? Huku kwetu ndivyo ilivyo, tena negotiations zinafanywa na AG, IGP na DG PCCB. Upo hapo? Halafu umekazana nyenyenye!!!!!
Hivi una habari kwamba wakati wewe na watoto wa vigogo wenzako, mnalipiwa starehe zenu kwa kodi za walala hoi huku, watoto wa hao walipa kodi hizo wamenyimwa hata fursa ya kukopeshwa tu pesa wanazotozwa baba zao ili waweze angalau kulipia ada tu za vyuo vikuu vya hapa nchini, huku sembe na maharage wakibangaiza wenyewe?
Wajua kwamba watoto wa shule za msingi wanafukuzwa kufanya mitihani kwa kukosa dola sents 3 ambayo ni shilingi mia tano. Najua unaogelea kwenye midola, lugha ya dola ndo utaielewa.
Una habari kwamba watoto wa Tanzania wanatembea kilomita 15 asubuhi 15 jioni kwenda na kurudi kazini kutafuta riziki kwa kukosa nauli ya basi? Katika hali hiyo unategemea tuongeze uzalishaji? Hivi wewe unayajua mateso ya nchi hii??? Ama!
Huna tofauti na kiongozi wetu mmoja wa juu ambaye aliulizwa swali na mtangazaji wa BBC kwamba licha ya utajiri mlionao kwanini watanzania watanzania ni masikini. Akajibu hata yeye anashangaa ni kwanini watanzania ni masikini. Halafu wanaposimama kuomba kura wanatoa ahadi nyingi za kuondoa umasikini. Nonsense, utaondoaje umasikini wakati hujui sababu za huo umasikini? Badala yake mnatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo ambao ni trading concerns, hawazalishi ati, matokeo yake boosting inflation. Tufanye upembuzi yakinifu kwanza. Matatizo ya mtanzania yapo kwenye uzalishaji. Hatuzalishi au tunazalisha kwa ajili ya matumbo yetu tu, mnasema "visious cycle of poverty". Huo sio wimbo au theories za vitabuni kama mlivyozoea watoto wa vigogo, it is a real thing. Poverty eradication is not the matter of sitting at Ngurudoto enjoying food, drinks and fresh air, it means real hard working.
What if hiyo mipesa wanayospend kianasa ingenunua matrekta, harvesters n.k halafu yakakodishwa kwa wanavijiji, malipo yakafanywa wakati wa mavuno, tungeshindwa kuwa na surplus?
Je badala ya kujenga BOT, tungehodhi mgodi wa mererani kwa ubia kati ya serikali na wananchi, tungesimamia/ control bei ya vito au kiwango tunachozalisha refer OPEC tungeongea lugha gani leo?
Je Watswana ni bora kiakili kuliko sisi? Mbona nchi yao ni jangwa na wanategemea zaidi almasi lakini wako juu? Tena kwa taarifa yako, idadi ya wananchi wote wa botswana haipishani na wakazi wa Dar Es Salaam, lakini wako juuu.
Kwa mawazo ya kitumwa kama yako, nchi haiwezi kuendelea. Tunahitaji fikra za kimapunduzi.
Vyombo vya dola vimekuwa vikipambana zaidi na wapigania haki, ambao wamekuwa wakiitwa wachochezi mfano Jambo Forum n.k, lakini kwa hakika ni katika kulinda mafisadi.
Nadhani umefika wakati vyombo hivyo vifanyiwe mabadiliko makubwa kimuundo. Vyombo kama PCCB, Police Force, Mahakama n.k.
Tuwe na fikra mpya wananchi, ule wakati wa zidumu fikra umepita sasa, mtu apimwe kwa kazi na utu wake na si itikadi yake.
Mapambazo dhidi ya mafisadi yanaendelea!!!!!!