UFISADI: The Making Of IPTL

UFISADI: The Making Of IPTL

Wapo ila .......... Dr Slaha hakufanya home work yake vizuri.

Upinzani style: KUKURUPUKA
Wapinzani sio Registrar wa mafisadi, hata kwa uchache wa hayo ambayo wameifanyia nchi wanastahili pongezi kwa sababu mlitegemea aina ya watu kama akina Membe awaambie ukweli?

Hii inatokana na wenye machungu wachache wasio na mamlaka ndiyo huwezesha kufichua uozo mbalimbali ndani ya mfumo.

Hivyo kuwaambia kwamba wamekurupuka ni kuto watendea haki fair play pls.
 
DAILYNEWS-Monday December 21, 2009

Liquidator uncovers fraud at IPTL

THE Provisional Liquidator of the Independent Power Tanzania Limited (IPTL), who was appointed by the High Court, Mr Theofil Rugonzibwa, has discovered fraud, corporate wastes, diversion of funds, oppression and mismanagement of the company.

In his second report filed before the court, the liquidator accused the company’s majority shareholder, Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard, of colluding with several other third parties to defraud the company of billions of shillings.

The liquidator says IPTL was made to pay more than 6 million US dollars for houses that were not built. He stated in his report that examination of the Engineering Procurement and Construction contract show that Wartsila Netherlands was supposed to build 102 units of staff houses.

However, he said, only 12 houses were built under a subcontract to Mechmar Heavy Industries, a subsidiary company of Mechmar Corporation, who issued a certificate of completion to Wartsila Netherlands, which built the power plant, while the work was not completed as per contract.

The liquidator also questions the rationale behind the Standard Chartered Bank to novate with Danaharta Managers Limited in 2005 the original IPTL Loan Facility Agreement dated June 28, 1997 and took over both contractual claims of the company and its obligations.

According to him, such move required leave of the court under the Companies Ordinance because in 2005 winding up proceedings involving IPTL had already commenced.

Therefore, he stated, the said novation between Danaharta and the Bank was illegal, null and void under the laws. Mr Rugonzibwa stated that the Bank had refused to provide to him evidence of its claims proving that the IPTL debt was more than 36.7 million US dollars.

He, therefore, requested the court to restrain the Bank from interfering with affairs of IPTL.

Furthermore, the liquidator discovered payments of 25,306,180 US dollars of premium on political risk insurance in which IPTL was not beneficiary. He stated that Mechmar Corporation has all along cheated IPTL on the matter as the beneficiary to that policy was herself and not the company.

He further discovered evidence showing conversion of assets of IPTL to Mechmar Corporation, like re-sale of 6697.30 metric tonnes of fuel worth 2,680,349.66 US dollars. Mr Rugonzibwa also said that 4,656,650 US dollars being refund from excise duty on fuel to IPTL was diverted to Mechmar’s private account.

He also says in his report that there was prima facie evidence of oppression and total deadlock against the company’s minority share holder, VIP Engineering and Marketing Limited and it appeared IPTL was being managed as a private property of Mechmar Corporation.

According to him, records of the company’s board meetings revealed that the VIP Engineering Company was not represented and, therefore, decisions concerning IPTL were taken when there was no quorum as required under Articles of Association of the company.

The liquidator pointed out further that as regard to members’ meetings, there was no record found at the registered office on the matter, meaning that none was conducted during the lifetime of the company and interests of the minority shareholder were not represented.

“If the minority shareholder was invited and opted not to attend all the time, it is clear evidence the marriage between the former friends had broken down. In such situation it is very difficult for them to sit and manage the company. The court has to decide when things are like this,” he said.

The filing of the report comes few days after the liquidator reported to the court on the failure by the parties of IPTL to reach any amicable solutions aimed at resolving disputes surrounding the company.

Judge Semistocles Kaijage, who is hearing the case at the moment has directed the liquidator to file in court in accordance with the law his applications as indicated in the interim report, if he has any, and set the case for mention on February 25, next year.
 
No Comment, hakuna ndani ya Tanzania ukigusa utakosa kupata Ufisadi ndio maana wageni wakija hawataki kuondoka kazi yao ni kuibia nchi tu, wadanganyika tumelala
 
Which is which?
Nasikia hawa vip engineering ndio waliokuwa wana own tritel...ambayo ilifilisika...then wakawa wanaown au sijui wana hisa na iptl

sasa iweje vip wanaishitaki iptl au usanii wa bwana mutalemwa?


Cha ajabu ni kuwa biashara zote ni lkucrative lakini huyu bwana ameshindwa kwenda mbali...tazama mobitel (tigo) walivyojizatiti kwenye market
 
Mbona unaonekana kukurupuka mkubwa maana hata hujui nani anamshtaki nani na kwa sababu gani. Unataka nani akupe majibu ya kukosa ufahamu wako?
 
Ahsante mkuu, lakini hii kitu ipo JF tangu 2006
 
ruge.jpg

Mmiliki kwa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira ameibuka na kukiri kuwa yeye ni miongoni mwa waliolipwa fedha hizo huku uongozi wa IPTL ukifafanua utata kuhusu mkataba wake na Tanesco na jinsi kampuni hiyo ilivyouzwa jumla kwa Pan African Energy.


SAKATA :

Maswali juu ya utaratibu uliotumika kutoa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye Akaunti ya Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutokana na mvutano baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na IPTL yameanza kupata majibu.

Wakati mmiliki kwa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira ameibuka na kukiri kuwa yeye ni miongoni mwa waliolipwa fedha hizo huku uongozi wa IPTL ukifafanua utata kuhusu mkataba wake na Tanesco na jinsi kampuni hiyo ilivyouzwa jumla kwa Pan African Energy.

Majibu ya Rugemalira

Katika ufafanuzi wake, Rugemalira alisema kati ya fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow, yeye akiwa mwanahisa wa IPTL alilipwa Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni), alizoziita ‘vijipesa vya ugoro' sawa na asilimia 30.

Alisema baada ya kuuza hisa zake kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP) aliruhusu pia asilimia 70 ya hisa za mbia mwenzake, Mechmar kutoka Malaysia ziuzwe pia kwa PAP.

Alisema kwenye akaunti hiyo kulikuwapo na Dola za Marekani 120 milioni, tofauti na kiwango kilichotajwa na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu aliyesema fedha hizo zilikuwa Dola 122 milioni.

Rugemalira alisema pia kuwa hatua ya kufikiwa kwa hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji John Utamwa Januari 17, mwaka 2014 saa 8:30 usiku, ilitokana na Waziri wa Nishati kumuomba wamalize kesi zilizokuwa mahakamani.

"Niliiambia Serikali kuwa nyie mmeibiwa na sisi tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the end justify the means' (jambo la muhimu ni matokeo, si njia ulikopitia), mwisho tulikubaliana kwamba kwa masilahi ya Taifa tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa hivyo vijipesa vya ugoro," alisema Rugemalira.

Hatua ya kutoa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow na kugawiwa kwa VIP Engineering na PAP, imefikiwa huku mkopeshaji wa IPTL, Benki ya Standard Charted ya Hong Kong (SCB-HK), inayodai Dola za Marekani 145 milioni (Sh234.456 bilioni), ikiwa haijalipwa na wala haijajulikana italipwa kwa kutumia kanuni gani.

Itakumbukwa kuwa, baada ya benki za Malaysia zilizokuwa zimeikopesha IPTL kuyumba kiuchumi, deni la benki hizo lilinunuliwa na SCB-HK.

"Tumeridhia kuwa hizo asilimia 70 zichukuliwe na PAP na Standard Charted anadai kwamba yeye ndiye mkopeshaji na dhamana yake ni hiyo mitambo, kitu ambacho siyo kweli. Lakini kama ni kweli aende mahakamani kuthibitisha," alisema Rugemalira.

Hukumu iliyotolewa Februari 12, 2014 na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Washington DC, Marekani, ilitaka pande hizo mbili zikae na kukubaliana namna ya kukokotoa gharama ambazo shirika hilo la umeme linapaswa kuilipa benki hiyo.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari jana, Rugemalira alionekana kujikanganya juu ya kuitambua SCB-HK, kuna wakati alisema haitambui na hivyo haikuwa na fedha zilizokuwa Escrow na wakati mwingine alisema bado anaidai benki hiyo na kesi ipo mahakamani.

Rugemalira alisema kwamba alikuwa Mkurugenzi wa IPTL hadi Januari 24, mwaka huu alipong'atuka, ingawa pia alisema baada ya kung'atuka alikuwa bado anaiwakilisha IPTL kwenye vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake kwa PAP.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari, Rugemalira alitumia muda mrefu kuipigia debe PAP akisema ni kampuni bora inayoweza kuzalisha umeme kwa bei nafuu.

"Swali la kujiuliza sasa, IPTL ni nani, jibu lake ni PAP," alisema Rugemalira.

Pia kuhusu suala la Mkataba wa IPTL na Tanesco kuanza 1995 na kutarajiwa kufikia kikomo 2015, Rugemalira alisema siyo sahihi na kuwa mkataba huo ulianza 2002 na ulitarajiwa kukamilika 2022.

Akizungumzia suala hilo, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa bado hana taarifa rasmi.

"Kwa sasa siwezi kusema chochote, hizi taarifa ndiyo kwanza nazisoma, lakini kama itagundulika kuna vitu vimekiukwa, kuna vyombo husika vitakavyochukua hatua," alisema Utouh.

Ufilisi IPTL wabatilishwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Philip Saliboko alisema ofisi yake ilikabidhiwa kazi ya ufilisi wa IPTL na Mahakama mwaka 2008 lakini mahakama hiyohiyo iliamuru Rita inyang'anywe ufilisi huo, Septemba 5, mwaka jana.

Saliboko alisema baada ya kunyang'anywa mamlaka ya ufilisi, IPTL ilikabidhiwa kwa Kampuni ya Pan African Energy Ltd (PAT) iliyoelezwa kuinunua.

"Hata hivyo, ofisi yangu haikupewa ufilisi wa muda mrefu, ilipewa wa muda mfupi, kwa hiyo majukumu yangu hayakufikia yale ya kuuza au kufilisi mitambo, bali kuuangalia kama IPTL ipo salama hadi hatua nyingine zitakapotajwa," alisema.

Kauli ya IPTL

Mwanasheria wa IPTL, Joseph Mwakandege alisema PAT ilinunua hisa kutoka kwa VIP Engineering na Nechmar kwa uwiano wa asilimia 70 kwa 30 na baada ya kununuliwa hisa hizo, Mahakama iliamuru kuwa PAT iwe mbia wa jumla wa Kampuni ya IPTL.

Mwakandege alipohojiwa kuhusu mkanganyiko wa mkataba kati ya Serikali na IPTL, alisema makubaliano baina ya pande hizo yalikuwa ni yale ya Kujenga, Kuendesha na Kumiliki (BOO), hivyo mali za IPTL zinabaki kuwa zake hadi baada ya mkataba kumalizika 2015.

Alisema mkataba huo haukuwa na kipengele cha kuiachia Serikali mitambo yake ya kuzalisha umeme.

Kuhusu Akaunti ya Escrow, mwanasheria huyo alisema haikuwa akaunti ya Serikali, bali fedha zilizokuwamo zilikuwa mali ya IPTL baada ya kuwapo kwa mgogoro baina ya wadau – IPTL na Tanesco.

"Kwanza ifahamike kuwa Escrow ilianzishwa kwa ajili ya wadau. Baada ya VIP Engineering na Nechmar kuuza hisa, akaunti ilikabidhiwa kwa PAT," alisema.

Alisema baada ya mgogoro huo kutokea, kila mdau aligawiwa kiasi chake cha hisa na kuondoka, hivyo fedha zilizobaki ni za IPTL.

Alikanusha kuwa Akaunti ya Escrow ilikuwa na Dola za Marekani 270 milioni, bali Dola 105 milioni na wala si zaidi ya hapo.

"Nyinyi mnafikiri Escrow ni ya Serikali. Mnafikiri Serikali ni wajinga na mafisadi kiasi hicho?" alisema.

Source: mwananchi.
 
Dar es Salaam. Maswali juu ya utaratibu
uliotumika kutoa fedha zilizokuwa
zimewekwa kwenye Akaunti ya Escrow katika
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutokana na
mvutano baina ya Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) na IPTL yameanza kupata
majibu.
Wakati mmiliki kwa Kampuni ya VIP
Engineering and Marketing, James Rugemalira
ameibuka na kukiri kuwa yeye ni miongoni
mwa waliolipwa fedha hizo huku uongozi wa
IPTL ukifafanua utata kuhusu mkataba wake
na Tanesco na jinsi kampuni hiyo ilivyouzwa
jumla kwa Pan African Energy.
Majibu ya Rugemalira
Katika ufafanuzi wake, Rugemalira alisema
kati ya fedha zilizokuwa katika Akaunti ya
Escrow, yeye akiwa mwanahisa wa IPTL
alilipwa Dola za Marekani 75 milioni (Sh120
bilioni), alizoziita ‘vijipesa vya ugoro’ sawa
na asilimia 30.
Alisema baada ya kuuza hisa zake kwa
Kampuni ya Pan African Power (PAP)
aliruhusu pia asilimia 70 ya hisa za mbia
mwenzake, Mechmar kutoka Malaysia ziuzwe
pia kwa PAP.
Alisema kwenye akaunti hiyo kulikuwapo na
Dola za Marekani 120 milioni, tofauti na
kiwango kilichotajwa na Gavana wa BoT,
Profesa Benno Ndulu aliyesema fedha hizo
zilikuwa Dola 122 milioni.
Rugemalira alisema pia kuwa hatua ya
kufikiwa kwa hukumu iliyotolewa na
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na
Jaji John Utamwa Januari 17, mwaka 2014 saa
8: 30 usiku, ilitokana na Waziri wa Nishati
kumuomba wamalize kesi zilizokuwa
mahakamani.
“Niliiambia Serikali kuwa nyie mmeibiwa na
sisi tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the
end justify the means’ (jambo la muhimu ni
matokeo, si njia ulikopitia), mwisho
tulikubaliana kwamba kwa masilahi ya Taifa
tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa
hivyo vijipesa vya ugoro,” alisema
Rugemalira.
Hatua ya kutoa fedha zilizokuwa kwenye
Akaunti ya Escrow na kugawiwa kwa VIP
Engineering na PAP, imefikiwa huku
mkopeshaji wa IPTL, Benki ya Standard
Charted ya Hong Kong (SCB-HK), inayodai
Dola za Marekani 145 milioni (Sh234.456
bilioni), ikiwa haijalipwa na wala
haijajulikana italipwa kwa kutumia kanuni
gani.
Itakumbukwa kuwa, baada ya benki za
Malaysia zilizokuwa zimeikopesha IPTL
kuyumba kiuchumi, deni la benki hizo
lilinunuliwa na SCB-HK.
“Tumeridhia kuwa hizo asilimia 70
zichukuliwe na PAP na Standard Charted
anadai kwamba yeye ndiye mkopeshaji na
dhamana yake ni hiyo mitambo, kitu ambacho
siyo kweli. Lakini kama ni kweli aende
mahakamani kuthibitisha,” alisema
Rugemalira.
Hukumu iliyotolewa Februari 12, 2014 na
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa
Migogoro ya Uwekezaji cha Washington DC,
Marekani, ilitaka pande hizo mbili zikae na
kukubaliana namna ya kukokotoa gharama
ambazo shirika hilo la umeme linapaswa
kuilipa benki hiyo.

Source. Mwananchi
 
vijipesa vya ugoro kweli kuna watu wanajua kuwatukana watu
Nimeishiwa hata la kucomment maana kuna watu wanaishi chini ya dola moja na kuna mtu ana 120 billion anaziita vijipesa vya ugoro
 
Matajiri wana matusi sana.Hivi Bilioni 120 ni 'vijipesa vya ugoro' kweli? Baada ya vijisenti sasa vipesa vya ugoro

Mzee Tupatupa
 
Inatia machungu sana, hivi sasa nadhani bomu litalipuka mda wowote ule.
 
hii nchi ina watu wana fedha bana sasa huyu Ruge kwa nini asiingie kwenye matajiri wa forbes, hapa serikali kwa nini isikaukiwe huko hazina, maana watu wanajichotea tu kwenye.kihenge.
 
Watu wanajua ni kiasi gani nchi hii imetafunwa mpaka $75m kuitwa vijipesa vya ugoro.Lazima kuna dili kubwa sana bado hazijafufuka
 
Back
Top Bottom