Ufisadi wa kutisha vodacom

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
2,441
Reaction score
652
Wana jf hebu tusaidiane ni kwa nini hii nchi makampuni yanapora mali za wanyonge kwa jeuri kubwa na hakuna wa kuwasemesha? Ni hivi, nilkuwa na salio la tshs. 2,943,040 kwenye line yangu ya voda; natumia lain hii kwa miamala ya kibenki,kununua huduma, kuongea na jamaa zangu nje hata masaa matano mfulizo, nk. Lakini ghafla wamekwiba pesa zote hizi na kuniwekea salio la zero zero;ni siku tano sasa tangu jumatano sipigi simu wala kufanya miamala yoyote. Nimewaripotia tangu alhamisi na wanachofanya ni kunitumia mimeseji eti wanachunguza, ni hadi lini? hivi mtu anaingia kwenye akaunt ya mtu kwa jeuri na kuiba masalio na pasiwepo na la kufanya? au hizi ndio pesa wanazofanyia mapromosheni ya uongo na kweli? kampuni gani inaweza kutoa zawadi bilioni moja lakini inaiba salio la milioni mbili? namba yangu ni 0754 843388 na mwenye wazo la kunisaidia tuwasiliane
 
Mkuu pole hii mitandao si ya kuiamini ushauri wangu nenda PHYSICALLY uwawashie moo hapo hapo ofisini kwao tena siku uhakikishe hakuna atakayefanya kazi mpaka warudishe hela yako. Kisha ushauri ni kuwa AKAUNTI YENYE PESA hivyo usii-connect na mabo ya MOBILE MONEY ni rahisi mtu kuiba tafuta benki ya Kiluga luga (analogue) ndo ukaweke pesa huko
 
Vodacom hawawezi kukuibia hela yako hata cku moja ilo futa akilini mwako nina uhakika ni mobile banking kwenda mpesa hili ni tatizo la mabenk yetu nenda vodashop yeyote ile iliyokaribu na ww watakwambia!!usipende kutumia lugha kali hvy wakati uhakika mwingine ww mwenyewe unaweza kujua sorce ya hili tatizo lako
 
Waibukie ofisini kwao makao makuu kalianzishe. Kuna siku nilikuta mteja muhindi pale posta jingo la kioo anawafokea wakawa ka watoto. Alikuwa analalamika pesa yake haioni. Sijui iliishia wapi ila walinywea mpaka meneja wao!
 
Kwenye upande wa huduma za kibenki kupitia simu Tanzania bado sana. Usalama wa pesa za wateja ni mdogo sana, ulinzi wa kuzuia wezi wa mitandaoni bado sana. Pesa zinaibiwa kwa namna ambayo hata wao wanabaki kuduwaa imekuwaje kitu ambacho hakitakiwi. Mimi hizi huduma za kibenki kutumia simu situmii kabisa na hata benki natumia akaunti ambayo haina kadi ya ATM wala nini. Pole sana.
 

Mkuu unataka aanze kubembeleza wezi?
Katika hali ya kawaida kama ni hitilafu hutokea kwa zaidi ya account moja. Sasa mtu tangu hiyo J5 hadi.keo anaambiwa wanafuatilia, system yao kama ingekuwa well secured haya yote yasingetokea, huo ni uzembe wao na wanatakiwa wawajibishwe. Hakuna lugha raini ya kuwabembeleza zaidi ya hy aliyoitoa.

Huu upole wetu sometime unakuwa ni ujinga.

Amevumilia tangu Jumatano leo ni Jumamosi bado unataka awe mpole?, Are u serious?

Hata katika vitabu vya Mungu haviruhusu upole unaosabisha kuwa mjinga.
 
Mi nina RB yao navizie nikutane na twisa nimkamate
 
Mkuu imeibiwa Salio la airtime au Salio la e-money? Hapo sijskuelewa mkuu.
Kama ni Salio la pesa iko kwenye line yani moesa au kwenye Akaunti ya Benki? Nashindwa kujua nikupe ushauri UPI.

Naasume iko kwenye Akaunti, then nenda benki waambie pesa iko wapi? Lakini kwa ulivoeleza ni ishu ya Vodacom ila kama ilikuwa kwenye akaunti na ikapotea, nina ihakika ungeenda benki badala ya Vodacom...kwa maana iyo kuna kitu haujaweka wazi apa na mwishowe tutalaumu bila kumjua mchawi!

Ni ayo mkuu
 


Jamaa yako kapigwa hela kwenye bank kaka kwenda mpesa yeye mwenyewe hajielewi tu hapo tatizo ni bank na huwa nawashanga sana mnapohangaika na mobile banking poleni sana
 
Hapana voda watendaji wake ni wezi tena sana watakuwa wamempiga hao jamaa.
Ata mimi wananipga sana kupitia airtime,ukiweka salio kaa kidogo alafu angalia salio,hujapga,hujatuma sms ila unakuta salio limekatwa,kimbembe sasa wapgie kitengo cha huduma kwa wateja Majibu yao utatamani kurudi kwenyeenzi za kuandika barua.
 
Ni hatari kubwa kutumia simu kwenye miala mikubwa ya benki. Hakuna usalama kabisa
 
Iliyoibiwa ni airtime mkuu, pesa ya vocha nilizoingiza kwa ajili ya maongezi sio bank balance
 
Jamaa yako kapigwa hela kwenye bank kaka kwenda mpesa yeye mwenyewe hajielewi tu hapo tatizo ni bank na huwa nawashanga sana mnapohangaika na mobile banking poleni sana
Walicholamba ni airtime au pesa ya vocha nilizojaza kwa ajili ya maongezi sio bank balance
 

Ni akaunt ya airtime sio bank account
 
Kuna wezi wa kila namna mitandaoni na jua kuwa kila atumiaye mtandao kwa kuiba kasoma sana jinsi ya kutoa pesa kupitia mitandao.
Hata wao Voda com wanaibiwa sana kwa watu kuongea bure kwa kutumia laini zao lakin ndo hivyo.
Cha msingi nenda voda com makao makuu watafuatilia simu yako kwa siku salio lipo na jinsi lilivyotoka na hapo watalirejesha tu naamini bila wasiwasi wowote.
Sasa tuna vijana wa Dot com wanataka magari kwa haraka, nyumba kwa haraka, amnunulie demu wake nyumba au gari ndani ya mwaka mmoja! Yote haya yanahitaji wizi ndo ufanikishe yote kwa muda unaotaka.
Ushauri
Vodacom fuatilieni vijana wenu ili kunusuru shirika na mwenye tatizo aende katika ofisi kuu (Dar es salaam) watajua mapema kuliko ofisi za vijiweni au wilayani au mikoani!!!
 
Mimi nikiwa Wakala nimeibiwa 500,000 nimetembea hadi viatu vimeisha .
Ni hivi :- alikuja mteja kuweka pesa nikamwamishia 500,000 . Hesabu ikapungua sawia kwenye acount yangu kuonyesha kua pesa zimeenda kwa mteja husika lkn mteja hakupata msg wala hela kwenye ac yake hazikuingia. Nikapiga simu wakataka niende morogoro pale wakakiri kua kuna tatizo na kwamba hela zingerudi baada ya siku Saba .
Siku Saba zikaisha nikatakiwa niende Dar. (Ninaishi turiani morogoro ) pale Huduma kwa wateja Mlimani center , nikaenda Safari hii nikaambiwa inabidi nije na yule mteja ambapo licha ya kua ni Jirani yangu lkn yeye hakupata msg wala hela hivyo hakulipa ile 500,000 kwa hiyo hakuathirika kwa vyovyote , licha ya gharama na muda lkn Hana sababu . Hivyo nimerudi kuendelea na shughuli zangu!
 
Mimi niliinunua muda wa maongezi tsh, 2000 nilipo taka kupiga simu nikaambiwa salio halitoshelezi kuangalia salio linasoma 0 NIMETUPA LINE YAO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…